RIPOTI SPESHO

SIMBA MWENDOKASI ‘KUJIUZA KWA MO’, MKUTANO MKUU WA DHARURA DESEMBA 11 KUBADILI KATIBA!

SIMBA-MOSIMBA Leo imetoa tamko rasmi kuthibitisha kuwa watafanya Mkutano Mkuu wa Dharura wa Wanachama wao hapo Desemba 11 katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam ili kubadilisha Katiba yao kwa kile kinachodhaniwa ni kupitisha njia Klabu hiyo kuuzwa Hisa zake.

Mfanyabiashara Mohamed Dewji, maarufu kama Mo, ana nia ya kununua Hisa za Simba za Asilimia 51 kwa Thamani ya Shilingi Bilioni 20 mpango ambao ulikubaliwa na Wanachama kwenye Mkutano wao wa Klabu.

Mara baada ya hatua hiyo, Yanga nao wakaanza mchakato wao wa kubadili mfumo wao wa uendweshaji.

Lakini zoezi hilo likaingia dosari baada ya Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania, BMT, Mohamed Kiganja, kusimamisha michakato ya Simba na Yanga ‘kubinafsishwa’ hadi Katiba za Klabu hizo zinazotambulika na Mamlaka husika kubadilishwa.

Baada ya Simba kukubaliana na Mo kuhusu kuuziwa Hisa, Yanga nao walikubaliana kumkodisha Mwenyekiti wao Yusuf Manji Klabu hiyo aiendeshe Kibiashara chini ya Kampuni yake kwa Miaka 10.

Mipango hiyo ya Vigogo hawa wa Soka Nchini pia iligonga mwamba TFF ambao pia walihoji kufuatwa kwa Katiba hizo.

Lakini nao Yanga waligonga mwamba kuitisha Mkutano Mkuu wa Wanachama wao ili kubariki kukodishwa Klabu kwa Manji baada ya wale waliodaiwa kuwa Wanachama wao kutinga Mahakamani na kupata Amri ya kuzuia Mkutano huo.

Tamko hili la Simba limetolewa Leo baada ya Kamati ya Utendaji yao kukaa Majuzi.

TAARIFA YA SIMBA IMESEMA:

SIMBA-TAARIFA