RIPOTI SPESHO

SERENGETI BOYS: HAFLA KUCHANGIA TIMU IJUMAA APRILI 28 HOTELI SERENA!

=LENGO KUKUSANYA BILIONI 1!
PRESS RELEASE NO. 289 APRILI 23, 2017
SERENGETI-CHANGIA-APR7HAFLA YA KUCHANGIA SERENGETI BOYS IJUMAA 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeandaa hafla maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya timu ya Serengeti Boys inayojiandaa kucheza fainali za kuwania Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini Gabon. 
Fainali hizi zitafanyika kufanyika kuanzia Mei 14 hadi 28, 2017. 
TFF inatambua kuwa wadau mbalimbali wamekuwa wakichangia timu hiyo kupitia mitandao ya simu kama vile namba 0687 333 222 kadhalika Selcom kwa namba 22 33 44 pia kuweka fedha kwenye akaunti Na. 00 866 280 03 katika Benki ya Diamond Trust (DTB). 
Sasa siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017 TFF imeandaa hafla maalumu ya kupokea michango hiyo, lakini pia kuchangisha fedha zaidi maana lengo ni kukusanya shilingi bilioni moja (Sh. 1 Bil.) 
Hafla hiyo itafanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni. 
TFF imeamua kutumia fursa kuwakaribisha wawakilishi wa makundi mbalimbali ili wawasilishe michango yao na kumkabidhi mgeni rasmi. 
Kwa kutambua michango mbalimbali ambayo imekusanywa kupitia makundi ya mitandao ya jamii kama WhattsApp, facebook hivyo TFF inaomba wawakilishi wa makundi yote ya mitandao ya jamii (admins) ambao wamekusanya michango hii wajiorodheshe ili wapate fursa ya kukabidhi michango ya makundi yao kwa mgeni rasmi katika hafla hii. 
Admins hawa wanaombwa wajiorodheshe kwa kutuma email kwenda This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., kwa kupiga simu 0787 176767 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 0787 176767 ambayo pia inapatikana kwenye mawasiliano ya WhattsApp. 
Aidha wawakilishi wa makundi mengine kama idara za Serikali, mashirika ya umma na binafsi kadhalika watu binafsi ambao nao wamechangia nao pia tunaomba wajioredheshe ili wapewe fursa pia ya kukabidhi michango yao siku hiyo ya Ijumaa. 
TFF inashukuru sana kwa ushirikiano.Mungu Ibariki TanzaniaMungu ibariki Serengeti Boys
……………………………………………………………………………
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

IBRAHIMOVIC, ROJO – MSIMU WAO UMEISHA! WATHIBITISHWA KUUMIA VIBAYA MAGOTI!

MANUNITED-ROJO-IBRAWACHEZAJI wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic na Marcos Rojo wamethibitika kuumia vibaya Magoti yao na wanatarajiwa kuwa nje kwa muda mrefu.

Wawili hao waliumia katika Mechi ya Alhamisi Usiku ambayo Man United waliifunga RSC Anderlecht 2-1 na kutinga Nusu Fainali ya UEFA EUROPA LIGI ambayo watacheza na Celta Vigo ya Spain.

Klabu ya Man United imethibitisha kuumia Magoti kwa Wawili hao lakini haikusema watakuwa nje kwa muda gani.

Ibrahimovic, ambae ndie Mfungaji Bora wa Man United Msimu huu akiwa na Bao 28, aliumia Goti lake baada kuurukia Mpira juu na kutua vibaya.

Rojo aliumia na kutolewa katika Dakika ya 23.

Ibrahimovic, mwenye Miaka 35, alijiunga na Man United kama Mchezaji Huru mwanzoni mwa Msimu huu akitokea Paris St-Germain na kusaini Mkataba wa Mwaka Mmoja ambao sasa kulikuwa na mchakato wa kumuongezea Mwaka mwingine Mmoja.

Lakini kuumia kwa Rojo ndiko ambako kutaleta wasiwasi kwa Meneja Jose Mourinho kwani ana upungufu wa Masentahafu kwa vile Phil Jones na Chris Smalling nao ni Majeruhi.

Masentahafu waliobaki na ambao ni gfiti ni Eric Bailly na Daley Blind.

Mechi zinazofuata kwa Man United ni za Ugenini za EPL, Ligi Kuu England, dhidi ya Burnley hapo Jumapili na Alhamisi ni huko Etihad dhidi ya Man City.

VPL: SIMBA YANASA KWA TOTO AFRICAN KIRUMBA!!

VPL-DTB-SITVINARA wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Simba Leo wametoka Sare ya 0-0 walipocheza na Toto African huko Mwanza Uwanjani CCM Kirumba.

Sare hii imewapa Simba Pointi 1 na sasa wamezoa Pointi 62 kwa Mechi 27 wakifuatwa na Mabingwa Watetezi Yanga ambao wana Pointi 56 kwa Mechi 25.

Kwenye Mechi zingine za VPL hii Leo JKT Ruvu na Azam FC zilitoka 2-2, Stand United na Mtibwa Sugar 0-0 na Ruvu Shooting kuichapa Maji Maji FC 4-1.

VPL itaendelea Jumapili kwa Mechi Mwadui FC kuikaribisha Ndanda FC na Mbao FC kuwa Wenyeji wa Tanzania Prisons.

VPL – LIGI KUU VODACOM

Jumamosi Aprili 15

Toto African 0 Simba 0

Stand United 0 Mtibwa Sugar 0

JKT Ruvu 2 Azam FC 2

Ruvu Shooting 4 Maji Maji FC 1

Jumapili Aprili 16

Mwadui FC v Ndanda FC

Mbao FC v Tanzania Prisons

MSIMAMO [Toka SOKA_App]:

VPL-APR15

 

 

 

 

 

TOKA TFF: VPL ALHAMISI MBEYA CITY KUIKWAA LYON, JUMAMOSI RUMBA KALI TOTO NA SIMBA KIRUMBA!

VPL-APR13-RATIBALigi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kuanzia kesho Alhamisi Aprili 13, 2017 kwa timu ya Mbeya City itaikaribisha African Lyon ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni.

Jumamosi ya Aprili 15, mwaka huu kutakuwa na michezo minne ambako Stand United itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga wakati Toto Africans ya Mwanza itaialika Simba SC ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Mechi hizi, zitachezwa kuanzia saa 10.00 jioni.

Kadhalika siku hiyo ya Jumamosi, Majimaji ya Songea itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani - mchezo utakaoanza saa 8.00 mchana ilihali JKT Ruvu ikiwa kwenye Uwanja wake mpya wa nyumbani - Mkwakwani jijini Tanga itaialika Azam ya Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni.

Kwa mujibu wa ratiba, Jumapili Aprili 6, mwaka huu Mbao itacheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza huku Mwadui ikiwa mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Mwadui mkoani Shinyanga. Kadhalika, mechi hizo zitaanza saa 10.00 jioni.

IMETOLEWA NA TFF

BAUZA ATIMULIWA ARGENTINA!

ARGENTINA-LOSSArgentina imemfukuza Menejabwao wa Timu ya Taifa Edgardo Bauza kufuatia matokeo mabovu yanayohatarisha.kufuzu kwao kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Bauza alisimamia Mechi 8 za Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini CONMEBOL za kusaka WC-2018-SA-TEBO-MAR24kwenda Fainali za huko Russia na wameshinda 3 tu kati ya hizo.
Hivi sasa Argentina wapo Nafasi ya 5 ya Nchi za Kanda ya Marekani ya Kusini nafasi ambayo itawanyima kufuzu moja kwa moja kwenda Russia.
Timu 4 za juu ndizo zinazofuzu moja kwa moja kwenda Fainali za Kombe la Dunia za huko Russia.
Timu inayomaliza Nafasi ya 5 hulazimika kucheza Mechi ya Mchujo na Nchi kutoka Kanda ya OCEANIA na Mshindi kutinga Russia.
Mbali ya kusuasua kwenye Mechi hizo za kwenda Russia, Argentina pia wapo kwenye pigo kubwa kutokana na Kifungo cha Mechi 3 cha Nahodha wao Lionel Messi kitakachomfanya acheze Mechi ya mwisho tu ya Kanda yao kwani wamebakiza Mechi 4 tu.
Bauza alishika Umeneja wa Argentina Agosti Mwaka Jana baada ya kujiuzulu kwa Gerardo "Tata" Martino alieng'oka baada ya Argentina kufungwa na Chile kwenye Fainali ya Copa America Centenario.
Muargentina ambae ni Kocha wa Sevilla ya Spain Jorge Sampaoli anatajwa kushika wadhifa huu.