EPL: LIVERPOOL ‘DORO’ YAZOA 3 ANFIELD, YAJICHIMBIA NAFASI YA 4!

>MECHI IJAYO NI ETIHAD CITY v LIVERPOOL!

LIVER-BURNLEYKWENYE Mechi pekee ya EPL, Ligi Kuu England, hii Leo Liverpool wakiwa kwao Anfield wakicheza ‘kigoigoi’ walitanguliwa Bao 1 na Burnley lakini wakaibuka Washindi kwa Bao 2-1.

Ushindi huu umezidi kuwachimbia Liverpool Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 55 kwa Mechi 28 na juu yao wapo Man City wenye Pointi 56 kwa Mechi 27 na Nafasi ya Pili ni Tottenham waliocheza Mechi 27 na wana Pointi 56 huku Vinara ni Chelsea waliocheza Mechi 27 na wana Pointi 66.

Chini ya Liverpool, kwenye Nafasi ya 5, wapo Arsenal wenye Pointi 50 kwa Mechi 26 na kisha Man United wenye Pointi 49 kwa Mechi 26.

Burnley walitangulia kufunga Dakika ya 7 kwa Bao la Ashley Barnes na Georginio Wijnaldum akaipa Liverpool Bao katika Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza.

Bao la ushindi la Liverpool lilifungwa Dakika ya 61 na Emre Can

Mechi ijayo kwa Liverpool ni huko Etihad dhidi ya Man City hapo Jumapili Machi 19.EPL-MAR12

VIKOSI:

Liverpool (Mfumo 4-3-3) Mignolet; Clyne, Matip, Klavan, Milner; Can, Wijnaldum, Lallana; Mane, Origi [Lucas, 79'], Coutinho [Woodburn, 60']
Akiba: Karius, Moreno, Lucas, Woodburn, Wilson, Alexander-Arnold, Gomez.

Burnley (Mfumo 4-4-2) Heaton; Lowton, Keane, Mee, Ward; Boyd [Brady, 73'], Barton, Hendrick, Arfield [Agyei, 90'], Gray [Vokes, 80'], Barnes
Akiba: Vokes, Brady, Westwood, Agyei, Tarkowski, Robinson, Darikwa

REFA: Craig Pawson

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba/Matokeo:

Jumapili Machi 12

Liverpool 2 Burnley 1                 

Jumamosi Machi 18

1530 West Bromwich Albion v Arsenal             

1800 Crystal Palace v Watford              

1800 Everton v Hull City             

1800 Stoke City v Chelsea          

1800 Sunderland v Burnley         

1800 West Ham United v Leicester City 

2030 Bournemouth v Swansea City                 

Jumapili Machi 19

1500 Middlesbrough v Manchester United                 

1715 Tottenham Hotspur v Southampton                  

1930 Manchester City v Liverpool          

Jumamosi Aprili 1

1430 Liverpool v Everton            

1700 Burnley v Tottenham Hotspur                 

1700 Chelsea v Crystal Palace               

1700 Hull City v West Ham United          

1700 Leicester City v Stoke City            

1700 Manchester United v West Bromwich Albion                

1700 Watford v Sunderland                  

1930 Southampton v Bournemouth                 

Jumapili Aprili 2

1530 Swansea City v Middlesbrough                

1800 Arsenal v Manchester City            

Jumanne Aprili 4

2145 Burnley v Stoke City           

2145 Leicester City v Sunderland           

2145 Watford v West Bromwich Albion            

2200 Manchester United v Everton                  

Jumatano Aprili 5

2145 Arsenal v West Ham United          

2145 Hull City v Middlesbrough             

2145 Southampton v Crystal Palace                 

2145 Swansea City v Tottenham Hotspur          

2200 Chelsea v Manchester City            

2200 Liverpool v Bournemouth              

Jumamosi Aprili 8

1430 Tottenham Hotspur v Watford                 

1700 Manchester City v Hull City           

1700 Middlesbrough v Burnley              

1700 Stoke City v Liverpool                  

1700 West Bromwich Albion v Southampton              

1700 West Ham United v Swansea City           

1930 Bournemouth v Chelsea                

Jumapili Aprili 9

1530 Sunderland v Manchester United            

1800 Everton v Leicester City                

Jumatatu Aprili 10

2200 Crystal Palace v Arsenal     

EPL: BOURNEMOUTH, EVERTON, HULL ZAPETA!

EPL-2016-17-LOGO2EPL – Ligi Kuu England

Matokeo:

Jumamosi Machi 11

Bournemouth 3 West Ham United 2      

Everton 3 West Bromwich Albion 0                 

Hull City 2 Swansea City 1

++++++++++++++++++++
LEO zilichezwa Mechi 3 tu za EPL, Ligi Kuu England, Chelsea, na Bournemouth, Hull City na Everton, waote wakicheza kwao, kuibuka kidedea.

Bournemouth waliichapa West Ham Bao 3-2

Nao Hull City waliifunga Swansea City 2-1 kwa Bao za Fowadi wa Senegal Oumar Niasse ambae yuko hapo kwa Mkopo kutoka Everton na Leo hii kuanzia Benchi.EPL-MAR11

Msenegal huyo alifunga Bao hizo Dakika za 69 na 78.

Bao pekee la Swansea lilifungwa na Alfie Mawson katika Dakika ya 92.

Nao Everton waliichapa WBA Bao 3-0 kwa Bao za Kevin Mirallas, Morgan Schneideirlin na Romelu Lukaku kwenye Mechi iliyochezwa Goodison Park.

Bournemouth wameibwaga West Ham 3-2 kwa Hetitriki ya Joshua King akipachika Bao hizo 3 Dakika za 31, 48 na 90 huku west Ham wakifunga Dakika za 10 na 83 kupitia Antonio na Andre Ayew.

EPL itaendelea Jumapili kwa Mechi 1 tu huko Anfield kati ya Liverpool na Burnley.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

Jumapili Machi 12

1900 Liverpool v Burnley            

Jumamosi Machi 18

1530 West Bromwich Albion v Arsenal             

1800 Crystal Palace v Watford              

1800 Everton v Hull City             

1800 Stoke City v Chelsea          

1800 Sunderland v Burnley         

1800 West Ham United v Leicester City 

2030 Bournemouth v Swansea City                 

Jumapili Machi 19

1500 Middlesbrough v Manchester United                 

1715 Tottenham Hotspur v Southampton                  

1930 Manchester City v Liverpool          

 

 

KISAGO CHA BAO 10: WENGER ‘ACHEFULIWA’ NA REFA!

WENGER-KILIO-OLDTRAFFORDArsene Wenger amesema Refa amemtia kichefuchefu baada ya Jana Arsenal kutwangwa 5-1 na Bayern Munich Uwanjani Emirates na kutupwa nje ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Jana Refa kutoka Greece Anastasios Sidiropoulos aliwapa Penati Bayern wakati Arsenal ikiongoza 1-0 na hapo hapo kumtoa nje kwa Kadi Nyekundu Sentahafu Laurent Koscielny na Bayern kusawazisha kwa Penati hiyo na kisha kushindilia Bao nyingine 4 na kushinda 5-1.

Katika Mechi ya Kwanza huko Germany Arsenal pia ilipigwa 5-1 na Bayern na hivyo kutupwa nje ya Hatua ya Mtoano ya Timu 16 kwa Jumla ya Bao 10-2.

Hii ni mara ya 7 mfululizo kwa Arsenal kushindwa kuivuka Hatuai hii ya UCL.

Wenger ameeleza: “Penati na Kadi Nyekundu havielezeki na ni kashfa. Ni uchezeshaji ovyo wa Refa. Nimekasirika na kuhuzunika sana!”

Vile vile Wenger alidai Refa huyo Mgiriki aliwanyima Penati katika Kipindi cha Kwanza wakati  Xabi Alonso alipomchezea Faulo Theo Walcott huku pia akidai Straika wa Bayern Lewandowski alikuwa Ofsaidi katika muvu ambayo Koscielny alimchezea Rafu Straika huyo na kuzaa Penati na Kadi Nyekundu.

Wenger pia alishangazwa na kitendo cha Refa huyo kwanza kumpa Kadi ya Njano Koscielny na kisha kuibadili kuwa Kadi Nyekundu baada ya ushauri wa Refa Msaidizi aliekuwa nyuma ya Goli.

Mbali ya janga na aibu ya kushushiwa kipigo kitakatifu, kabla ya Mechi hiyo kuanza Wenger pia alikumbana na adha ya Mashabiki wa Arsenal waliomtaka ajiuzulu na kuinua Mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kumtaka ang’oke.

Alipohojiwa kuhusu Washabiki hao, Wenger alijibu hana la kusema.

WENGER AWAPONDA MAMENEJA VIJANA, AJIBATIZA YEYE 'PADRI WA SOKA'!

WENGER-ATAFAKARIArsene Wenger amewaponda Mameneja Vijana kwa kukosa uvumilivu na kujiita yeye "Padri wa Soka' mara tu baada ya Luis Enrique kutangaza yeye atang'atuka Barcelona mwishoni mwa Msimu huu.
Kauli ya Enrique imeleta fikra kuwa huenda Wenger nae akatimkia huko Spain kujiunga na Barcelona mwishoni mwa Msimu kwa vile Mkataba wake na Arsenal unakwisha wakati huo.
Enrique amedai amechoka baada ya Miaka Mitatu tu akiwa na Barca akifuata nyayo za Pep Guardiola ambae nae aling'atuka kwa staili hiyo.
Wenger, mwenye Miaka 67, anahisi Rika la sasa la Mameneja Vijana linakosa uvumilivu na moyo wa kujituma na kutumikia kwa Miaka mingi kama yeye alivyofanya akidumu Arsenal kwa Miaka 20.
Wenger amenena: "Mie ni spesho kwa ukatili. Ukiwa Meneja unapata Kero Asilimia 90 na furaha na kuridhika kwa hali ya juu kwa Asilimia 10 tu!"
"Siku zote nawaambia hawa Vijana wanaotaka kazi hii: 'Uko tayari kujitoa muhanga, kuyadhuluma maisha yako?' Ni sawa kuwa kama Padre, wewe ni Padri wa Soka!"
Kuhusu yeye kwenda Barca kama anavyotuhumiwa Wenger amekataa katakata kuzungumzia hilo mbali ya kudai bado hajaamua kama atasaini Mkataba wa kubakia na Arsenal au la.

LUIS ENRIQUE KUNG'OKA BARCELONA!

LUIS-ENRIQUEBOSI wa Barcelona Luis Enrique ataachia ngazi mwishoni mwa Msimu huu akidai anahitaji mapumziko.
Enrique, mwenye Miaka 46, yupo kwenye Msimu wake wa 3 na Barca.
Kocha huyo alitangaza uamuzi wake huo hapo Jana mara tu baada ya Barca kuitwanga Sporting Gijon 6-1 na kutwaa uongozi wa La Liga wakiwa Pointi 1 mbele ya Real waliocheza Mechi 1 pungufu.
Akiwa na Barca, alitwaa Ubingwa wa UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI kwenye Msimu wake wa kwanza tu ikiwa ni moja ya Mataji Matatu aliyotwaa Msimu huo na Msimu uliopita kutwaa Ubingwa wa La Liga na Copa del Rey.
Lakini Msimu huu wako Mguu mmoja nje ya UCL baada kuchapwa 4-0 na Paris St-Germain huko Paris, France katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 wakiombea miujiza ili kupindua kipigo hicho katika Mechi ya Marudiano itakayochezwa Nou Camp hapo Machi 8.
Enrique alikuwa Mchezaji wa Kimataifa wa Spain ambae alikuwa Real Madrid kati ya 1991 na 1996 na pia aliichezea Barca kati ya 1996 na 2004 alipostaafu Soka.
Kati ya 2008 na 2011 alikuwa Kocha wa Barcelona B na kisha kwenda kuzifundisha Klabu za AS Roma huko Italy na Celta Vigo ya Spain na 2014 kurejea Barca kuchukua nafasi ya Gerardo Martino kama Kocha Mkuu.
Show more