UEFA CHAMPIONZ LIGI: LEO ARSENAL NA LUDOGORETS, WENGER AONYA!

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Ratiba:

Jumatano Oktoba 19

**Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku

KUNDI A

Arsenal v Ludogorets Razgrad              

Paris St Germain v Basel             

KUNDI B

Dynamo Kiev v Benfica               

Napoli v Besiktas              

KUNDI C

Barcelona v Man City                 

Celtic v Borussia Monchengladbach                 

KUNDI D

Bayern Munich v PSV Eindven               

FC Rostov v Atletico Madrid        

++++++++++++++++++++++++++++++

ARSENAL-LUDOGORETSUSIKU huu Arsenal wanacheza Mechi yao ya 3 ya Kundi A la UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, wakiwania ushindi dhidi ya Mabingwa wa Bulgaria Ludogorets Razgrad ambayo watacheza nao tena huko Sofia Mechi ifuatayo.

Baada ya kutoka Sare na Paris St-Germain katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi A, Arsenal waliichapa FC Basel 2-0 na ushindi dhidi ya Ludogorets kwenye Mechi hii na ijayo utakikisha wao kufuzu hatua ya Mtoano kwenye Kundi hili ambalo wao na PSG ndio wanapewa nafasi kubwa kufuzu.

Hivi sasa Arsenal wapo kwenye wimbi zuri la ushindi kwani tangu wafungwe 4-3 na Liverpool kwenye Mechi yao ya kwanza ya EPL, Ligi Kuu England, wameshinda Mechi zao 6 zilizopita katika Mashindano yote.

++++++++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-Arsenal na Ludogorets Razgrad hazijawahi kukutana hata mara moja!

++++++++++++++++++++++++++++++

Ingawa si jina kubwa huko Ulaya, Ludogorets ni Timu ngumu kufungika na Arsenal inabidi wakaze buti kuifunga na pia kumtupia jicho Straika wao hatari kutoka Brazil Jonathan Cafu.

Hilo limemfanya Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, awahimize Wachezaji wake kujituma na si kubweteka kwa kupambana na Timu isiyo na jina.

Mechi nyingine ya Kundi A hii Leo ni huko Paris, France kati ya PSG na FC Basel.

UCL-GROUPA-OKT19

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

Arsenal: Cech; Bellerin, Mustafi, Koscielny, Monreal; Xhaka, Cazorla; Walcott, Ozil, Iwobi; Sanchez

Ludogorets: Vladislav Stoyanov, Yordan Minev, Cosmin Mo, Jose Luis Palomino, Natanael, Svetoslav Dyakov, Anicet Abel, Marcelinho, Virgil Misidjan, Wanderson, Jonathan Cafu

REFA: Artur Dias [Portugal]

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Matokeo:

Jumanne Oktoba 18

KUNDI E

Bayer Leverkusen 0 Tottenham 0          

CSKA 1 Monaco 1            

KUNDI F

Real Madrid 5 Legia Warsaw 1              

Sporting Lisbon 1 Borussia Dortmund 2           

KUNDI G

Club Brugge 1 FC Porto 2           

Leicester1 FC Copenhagen 0                

KUNDI H

Dinamo Zagreb 0 Sevilla 1          

Lyon 0 Juventus 1                          

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MAKUNDI:

Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba

Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba

Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba

Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba

Mechi ya Sita: 22 na 23 Novemba

Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba

MECHI ZA MTOANO:

11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza

18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

 

 

 

ARSENE WENGER ATAKA ARSENAL IKWEPE ‘VIRUSI’!

WENGER-OUT-NEWMENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesema kipigo toka kwa Swansea City Msimu uliopita ndio kilimaliza ndoto yao ya Ubingwa wa EPL, Ligi Kuu England, na kilieneza ‘Virusi’ vya upinzani miongoni mwa Mashabiki wao.

Mwezi Machi, Bao za Wayne Routledge na Ashley Williams, ndizo ziliwapa EPL-OKT1Cushindi wa 2-1 Swansea Uwanjani Emirates na kufuatia kichapo cha 3-2 huko Old Trafford mikononi mwa Manchester United na kuwatupa Pointi 6 nyuma ya Vinara Leicester City ambao hatimaye wakatwaa Ubingwa wakiwaacha Arsenal Pointi 10 nyuma.

Vipigo hivyo viliamsha hasira za Mashabiki wa Arsenal waliomponda sana Wenger.

Akiongea hapo Jana kuelekea Mechi yao ya Leo Uwanjani Emirates dhidi ya Swansea, Wenger ameeleza: “Lazima niseme upinzani na upondaji huibuka haraka sana. Ni Kirusi kinachosambaa haraka mno na kuondoka polepole sana!”

Hii Leo Arsenal wataivaa Swansea wakitoka kwenye wimbi la ushindi wa Mechi 5 katika Mashindano yote na kwenye EPL wako Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 2 tu nyuma ya Vinara Manchester City.

Wenger amesema: “Naamini hali ya ushwari imerejea na imani ipo. Tumepunguza pengo na Timu za juu. Lazima tuendelee kufika hatua nyingine. Mashabiki ni sehemu ya Gemu na wana haki ya kuwa na furaha. Kazi yangu ni kutilia mkazo kazi yangu na kujaribu kuwaletea furaha!”

EPL - LIGI KUU ENGLAND

**Saa za Bongo

Jumamosi 15 Oktoba 2016

1430 Chelsea v Leicester City               

1700 Arsenal v Swansea             

1700 Bournemouth v Hull           

1700 Man City v Everton            

1700 Stoke v Sunderland            

1700 West Brom v Tottenham               

1930 Crystal Palace v West Ham

Jumapili 16 Oktoba 2016

1530 Middlesbrough v Watford             

1800 Southampton v Burnley                

Jumatatu 17 Oktoba 2016

2200 Liverpool v Man United      

 

ENGLAND - BAADA KUEPUKA KICHAPO, KOCHA SOUTHGATE AUNGAMA KARITHI 'UOZO'!

ENGLAND-SOUTHGATEKOCHA wa muda wa England Gareth Southgate ameungama kuwa amerithi 'uozo' baada ya Timu yao Jana kunusurika kipigo.na kuambua Sare ya bahati walipocheza na Slovenia Ugenini ikiwa ni Mechi ya Kundi F la Nchi za Ulaya zinazowania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Southgate, ambae alikuwa Kocha wa England U-21, amechukuwa wadhifa wa muda wa Timu ya Kwanza ya England baada kuondoka kwa Sam Allardyce na Mechi yake ya kwanza ilikuwa pia ua Kundi F la IMG 20161012 123724Kombe la Dunia Jumamosi iliyopita walipoifunga Malta huku Uwanjani Kepteni Wayne Rooney alicheza.

Lakini Jana, wakicheza huko Ljubljana na bila Rooney, England wanapaswa kumshukuru Kipa wao Joe Hart kwa kuwapa Pointi 1 baada ya kuokoa Goli za wazi kadhaa.

Hata Rooney alipoingizwa zikibaki Dakika 18, England ilibaki goigoi.

Hata hivyo, Sare hiyo imewaweka England kileleni mwa Kundi F.

Akiongea baada ya Mechi hiyo, Southgate aliungama: "Tumerithi uozo hasa na inabidi tuliweke sawa Jahazi. Nia ni kufuzu kucheza Fainali lakini inabidi tucheze vizuri zaidi!"

Mechi ijayo kwa England ni dhidi ya Wapinzani wao wakubwa kihistoria, Scotland, ikiwa pia ni ya Kundi F itakayochezwa Novemba 11 Uwanjani Wembley.

PELLE ATUPWA NJE ITALY, ALIGOMEA MKONO KWA KOCHA ALIPOTOLEWA MECHI NA SPAIN!

PELLE-MKONOSTRAIKA wa Italy Graziano Pelle ameondolewa kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa ya Italy ambacho Jumapili kitacheza na Macedonia kwenye Mechi ya Kundi la Nchi za Ulaya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia baada ya kukataa kumpa Mkono Kocha alipobadilishwa kwenye Mechi yao ya Alhamisi na Spain.

Pelle, mwenye Miaka 31 na ambae alikuwa England akiichezea Southampton kabla kuhamia China Msimu huu, alitolewa nje na Kocha Giampiero Ventura katika Dakika ya 60 na kugoma kumpa mkono Kocha wake alienyosha mkono wake wakati akirudi Benchi toka Uwanjani.

Wakati huo Spain walikuwa wakiongoza 1-0 na Pelle alipwaya na nafasi yake kuchukuliwa na Ciro Immobile.

Wakitangaza uamuzi huu wa kumwondoa Pelle Kikosini, Shirikisho la Soka la Italy, FIGC, limetamka kuwa kuwemo miongoni mwa Timu ya Taifa kunaanzia na kuonyesha heshima kwa Makocha, Wachezaji na Mashabiki.

Kabla ya tamko hilo la FIGC, Kocha Giampiero Ventura, mwenye Miaka 68 na ambae amemrithi Antonio Conte aliehamia Chelsea, alieleza: “Sidhani Pelle alikasirika kwa sababu ya kutolewa bali uchezaji wake. Nishaona vitu kama hivi katika maisha yangu ya Soka. Ndio Soka lakini ukivaa Jezi ya Italy unapaswa kuwa mwangalifu.”

Hivi sasa Pelle, ambae aliomba radhi mapema kabla hajaenguliwa Kikosi cha Italy, anatarajiwa kurejea China kujiunga tena na Klabu yake Shandong Luneng.

Kwenye Mechi hiyo na Spain Vitolo alitangulia kufunga Bao kwa Spain na Italy kusawazisha kwa Penati ya Daniele de Rossi.

MAWAKALA NI 'KANSA' KWENYE SOKA!

MAWAKALAMMILIKI wa Klabu ya Soka ya Italy, Napoli, Aurelio De Laurentiis, amesema Mawakala wa Wachezaji ni 'Kansa' kwenye Soka.
De Laurentiis alitoa kauli hiyo huko London kwenye Mkutano wa Viongozi wa Michezo wa Kibiashara huku akisisitiza Wachezaji hawahitaji Watu hao.
De Laurentiis, mwenye Miaka 67 na ambae pia ni Mtengeneza Filamu, ameweka bayana kilio cha Maneneja na Vilabu vingi wanavyoendeshwa puta na kunyonywa na Mawakala hao na kuwasema sasa wamekuwa kama Kodi na kutaka walipwe mbele ya Dili yeyotem
Amesema: "Huko Hollywood, Mwigizaji Filamu humlipa Wakala yeye mwenyewe. Mie simlipi Wakala. Kwanini kwenye Soka nimlipe Wakala?"
De Laurentiis pia ametoboa kuna baadhi ya Uhamisho wa Wachezaji hukwama baada ya Mawakala kugomea mgao wa Haki za Wachezaji za Umiliki wao wa Picha na Matangazo yao.
Ameeleza: "Unajua hii ni Kansa ya shughuli zetu. Si Mawakala wote. Lakini sielewi kwa nini unahitaji Wakala!"
Hata hivyo, Mel Stein, Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Soka (Association of Football Agents), amesems kauli hiyo pia inawahusu Wamiliki wa Vilabu na Wenyeviti wao.
Amesema: "Ukweli ni kwamba wapo Watu wabaya lakini huwezi kuwaita ni Kansa. Tunataka kusafisha hili na tunajua lipi la kufanya!"