STAA WA TOTTENHAM MOUSSA SISSOKO ‘KUFUNGWA’ MECHI 3!

SPURS-SISSOKOMCHEZAJI alienunuliwa na Tottenham kwa Dau la juu kabisa katika Historia yao, Moussa Sissoko, anangojea tu kushushiwa Rungu lake la Kufungiwa Mechi 3 baada ya kukiri kosa la Uchezaji wa Vurugu.
Sissoko alifunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, baada ya kunaswa kwenye TV akimpiga Kiwiko Mchezaji wa Bournemouth Harry Arter Jumamosi iliyopita wakati Tottenham na Bournemouth zilipotoka 0-0 Uwanjani Vitality kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Tukio hilo halikuonwa na Refa na ndipo FA ikalipeleka kwenye Jopo Huru na likaamua kumfungulia Mashitaka ya Uchezaji wa Vurugu.
Bosi wa Spurs, Mauricio Pochettino, amesisitiza tukio hilo si la makusudi lakini wao wameamua kukiri Kosa.
Nae Kiungo wa Bournemouth, Arter, alitoboa kuwa alikuwa akiomba Sissoko asifungiwe kwa vile alimuomba msamaha mwishoni mwa Mechi hiyo.
Arter ameeleza: "Ilionyesha amenipiga kiwiko lakini aliniomba msamaha na kusema ni bahati mbaya hakukusudia, kwangu huo ni mwisho!”
Aliongeza: “Mwishoni mwa Gemu aliomba radhi na mie siweki kinyongo. Ameomba msamaha, hakukusudia, huo ni mwisho. Wakati ule nilidhani atapewa Kadi Nyekundu lakini Refa alisema hakuona. Kwangu mie nimefurahi kuombwa msamaha!”

EPL: CITY SARE NA SAINTS LAKINI WAKAMATA USUKANI!

 EPL - LIGI KUU ENGLAND

Ratiba/Matokeo:

Jumapili Oktoba 23

Man City 1 Southampton 1 ­­

1800 Chelsea v Man United

++++++++++++++++++++++++++++++++

CITY-Kelechi-IheanachoMAN CITY wamerejea kileleni mwa EPL, Ligi Kuu England, kufuatia Sare ya 1-1 kwenye Mechi iliyochezwa Etihad mapema Leo.

Matokeo haya yamewaweka City kwenye wimbi la Mechi 5 bila ya ushindi lakini wapo juu kwenye EPL kwa Ubora wa Magoli wakifungana kwa Pointi na Arsenal na Liverpool wote wakiwa na Pointi 20 kila mmoja baada ya Mechi 9.

Dakika ya 27 Southampton walifunga Bao lao baada ya Difensi ya City kujichanganya wenyewe pale Pasi ya mbovu ya Stones kwa Kompany kunaswa na Nathan Redmond aliemzunguka Kipa Claudio Bravo na kufunga.

Hadi Mapumziko City 0 Southampton 1.

Kipindi cha Pili Pep Guardiola alimtoa Kevin De Bruyne na kumwingiza Mnigeria Kelechi Iheanacho ambai ndie alisawazisha Bao katika Dakika ya 55 akiunganisha Krosi ya Leroy Sane.

Hadi mwisho City 1 Southampton 1.

VIKOSI:

Manchester City: Bravo; Stones, Kompany, Kolarov; Fernandinho, Gundogan; Sane, Silva, De Bruyne, Sterling; Aguero.

Akiba: Fernando, Nolito, Caballero, Jesus Navas, Clichy, Otamendi, Iheanacho.

Southampton: Forster; Martina, Fonte, van Dijk, McQueen;

Clasie, Romeu, Davis; Tadic, Redmond, Austin.

Akiba: Yoshida, Rodriguez, McCarthy, Ward-Prowse, Boufal, Hojbjerg, Stephens.

REFA: Mark Clattenburg

EPL - LIGI KUU ENGLAND

**Saa za Bongo

Jumamosi Oktoba 29

1430 Sunderland v Arsenal         

1700 Man United v Burnley

1700 Middlesbrough v Bournemouth                

1700 Tottenham v Leicester        

1700 Watford v Hull

1700 West Brom v Man City       

1930 Crystal Palace v Liverpool             

Jumapili Oktoba 30

1630 Everton v West Ham 

1900 Southampton v Chelsea                

Jumatatu Oktoba 31

2300 Stoke v Swansea                

         

EPL: BOURNEMOUTH, SPURS SARE!

EPL - LIGI KUU ENGLAND
Ratiba/Matokeo:
Jumamosi Oktoba 22
**Saa za Bongo
Bournemouth  0 Tottenham 0         
1700 Arsenal v Middlesbrough              
1700 Burnley v Everton              
1700 Hull v Stoke            
1700 Leicester v Crystal Palace             
1700 Swansea v Watford            
1700 West Ham v Sunderland               
1930 Liverpool v West Brom
++++++++++++++++++++++++++++++++
BOURNE-SPURSBOURNEMOUTH na Tottenham zilicheza Mechi ya kwanza kabisa hii Leo ya EPL, Ligi Kuu England, huko Vitality Stadium Mjini Bournemouth na matokeo kuwa 0-0.
Hadi Mapumziko Bournemouth 0 Tottenham 0.
Kipindi cha Pili kila Timu ilipata nafasi kadhaa lakini walishindwa kuzitumua.
Kwa Spurs, licha ya kutoshinda angalau wamedumisha rekodi ya kuwa bado ndio Timu pekee ambayo haihapoteza mchezo wa EPL Msimu huu.
VIKOSI:
Bournemouth: Boruc; Adam Smith, Francis, Steve Cook, Daniels; Surman, Arter, Wilshere; King(Fraser, 88'), Ibe (Gradel, 60'), Callum Wilson (Afobe, 82')
Akiba: Gosling, Aké, Afobe, Gradel, Federici, Fraser, Mings. 
Tottenham: Lloris; Walker, Dier, Vertonghen, Rose; Wanyama, Dembélé; Alli (Sissoko, 72'), Lamela, Eriksen; Son (Janssen)
Akiba: Janssen, Vorm, Trippier, Sissoko, Wimmer, Winks, Davies.
REFA: Craig Pawson
EPL - LIGI KUU ENGLAND
**Saa za Bongo
Jumapili Oktoba 23
1530 Man City v Southampton    
1800 Chelsea v Man United
Jumamosi Oktoba 29
1430 Sunderland v Arsenal          
1700 Man United v Burnley
1700 Middlesbrough v Bournemouth                
1700 Tottenham v Leicester        
1700 Watford v Hull
1700 West Brom v Man City       
1930 Crystal Palace v Liverpool             
Jumapili Oktoba 30
1630 Everton v West Ham 
1900 Southampton v Chelsea                
Jumatatu Oktoba 31
2300 Stoke v Swansea

EPL: JUMAMOSI ARSENAL KUIVAA BORO, KUTWAA UONGOZI?

>>WENGER AONYA TIMU YAKE -  CHUNGA LIGI NI ‘PORI’!

ARSENAL-WENGER-KIDOLEJUMAMOSI Arsenal wapo kwao Emirates kuivaa Middlesbrough, maarufu kama Boro, kwenye EPL, Ligi Kuu England, na hiyo ni nafasi poa kwao kutwaa uongozi wa Ligi hiyo.

Hivi sasa Arsenal wako Pointi sawa na Vinara Man City ambao wako juu tu kwa Ubora wa Magoli na wanacheza Jumapili na Suthampton na hii ni nafasi kwa Arsenal kuandika ushindi wao wa 8 mfululizo tangu wafungwe 4-3 na Liverpool kwenye Mechi yao ya kwanza kabisa ya EPL Msimu huu.

Lakini akiongea hii Leo na Wanahabari kwa ajili ya Mechi yao hiyo ya Kesho Jumamosi, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, alisema: “Naamini ni utu kutambua unaanza toka sifuri. Tunaishi kwenye Pori ambalo kila Mtu anataka kukula wewe, inabidi ujihami ili uishi. Huo ndio ushindani!”

Wenger pia amedokeza hali za Wachezaji wake na kusema Santi Cazorla ana hatihati EPL-OKT17kucheza baada ya kupata maumivu Juzi walipoibonda Ludogorets Razgrad 6-0 kwenye Mechi ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, wakati Kiungo Granit Xhaka hatakuwepo kabisa akianza Kifungo chake cha Mechi 3 baada ya Kadi Nyekundu aliyopata kwenye Mechi iliyopita walipocheza na Swansea City.

Kuhusu Majeruhi Olivier Giroud na Aaron Ramsey, Wenger alisema Giroudanaweza akacheza Jumanne ijayo kwenye Mechi ya EFL CUP dhidi ya Reading wakati Ramsey huenda akaonekana huko Stadium of Light Wikiendi ijayo wakicheza na Sunderland.

Kuhusu Majeruhi wa muda mrefu, Danny Welbeck, Wenger amesema anaendelea vizuri mno kuuguza Goti lake aliloumia vibaya na anaweza kurejea Mwezi Januari.

EPL - LIGI KUU ENGLAND

**Saa za Bongo

Jumamosi Oktoba 22

1430 Bournemouth v Tottenham           

1700 Arsenal v Middlesbrough              

1700 Burnley v Everton              

1700 Hull v Stoke            

1700 Leicester v Crystal Palace             

1700 Swansea v Watford            

1700 West Ham v Sunderland               

1930 Liverpool v West Brom                 

Jumapili Oktoba 23

1530 Man City v Southampton    

1800 Chelsea v Man United                  

         

KISAGO CHA BARCA: GUARDIOLA HABADILI FALSAFA YA MBINU ZAKE!

>”MPAKA SIKU YA MWISHO UKOCHA TUTAANZA KWA PASI YA KIPA WETU!”

CITY-BRAVO-RCPep Guardiola amesema hatabadili Falsafa ya Mbinu zake licha ya Manchester City Jana kutwangwa 4-0 na Klabuyake ya zamani Barcelona huko Nou Camp kwenye Mechi ya Kundi C la UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Kwenye Mechi hiyo Lionel Messi alipiga Hetitriki na moja kufungwa na Neymar huku Kipa wa City Claudio Bravo, Mchezaji wa zamani wa Barca, aliefanya kosa kubwa na kuzawadiwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 54.

Guardiola ameeleza: “Hamna mabadiliko. Mpaka Siku yangu ya mwisho kama Kocha ntajaribu kuanza kwa kucheza toka kwa Kipa wetu!”

Huku Barca wakiongoza Bao 1, mapema Kipindi cha Pili, Kipa Bravo aliinasa Pasi ndefu na alipotaka kuanza Mpira kwa Beki wake kama ilivyo kawaida yake badala ya kupiga mbele, Pasi yake hiyo ikanaswa na Luis Suarez ambae alipiga juu Mpira kumvuka Bravo na Kipa huyo akaruka juu na kuucheza Mpira kwa Mikono wakati akiwa nje ya Boksi.

Kwa kosa hilo, Bravo akapewa Kadi Nyekundu na City kubaki Mtu 10.

Kuhusu kosa hilo la Bravo ambae aliletwa City kutoka Barca kumbadili Kipa Namba Wani wa England Joe Hart kwa sababu tu hutumia miguu kuanzisha Gemu toka Golini na kuwapasia Mabeki wake badala ya kubutua mbele, Guardiola ameeleza: “Wakati mwingine kuna makossa ana wakati mwingine unalazimika kupiga Mpira nje lakini mara nyingi, tukicheza vizuri, Mpira huanzia kwa Pasi ya Kipa.”

Aliongeza: “Ni wazi anajua alichofanya kwa sababu ana uzoefu mkubwa nay eye ni mmoja kati ya Makipa Bora katika Miaka 10 iliyopita, sina wasiwasi nae!”

Hivi sasa City hawajashinda katika Mechi zao 4 zilizopita lakini bado wapo kileleni mwa EPL, Ligi Kuu England, na kipigo hiki ni cha kwanza kwa Guardiola katika Mechi zake 11 tangu ashike hatamu Msimu huu.

+++++++++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

- Pep Guardiola ataifikia Rekodi yake ya kwenda Mechi nyingi bila kushinda, ya Mechi 5, ikiwa Jumapili watashindwa kuifunga Southampton.

+++++++++++++++++++++++++++

Akiongelea Timu yake kuifikia kiwango cha Barcelona, Guardiola amefafanua: “Tumefungwa 4-0 lakini sie ni Klabu mpya, ndio tunaanza kujuana. Kwa Miaka 35 hatukuwepo Ulaya! Siku zote ni ngumu kucheza na Barceloana ukiwa na 11. Tulipokuwa 10 Gemu ilikwisha!”

Msimamo hivi sasa kwenye Kundi C ni kuwa Barca wako kileleni wakiwa Pointi 5 mbele ya City walio Nafasi ya Pili na wa 3 ni Borussia Monchengladbach na mkiani ni Celtic.

UCL-C-OKT20

MAN CITY – Mechi zijazo:

Jumapili Oktoba 23

EPL   

1530 Man City v Southampton        

Jumatano Oktoba 26

EFL Cup – Raundi ya 4

2200 Man Utd v Man City       

Jumamosi Oktoba 29

EPL

1700 West Brom v Man City            

Jumanne Novemba 1

UCL - Kundi C      

Man City v Barcelona