LIGI KUU ENGLAND: ARSENAL WASHINDA, WAJICHIMBIA YA 4!

>MECHI NYINGINE LEO OLD TRAFFORD NI MAN UNITED-WEST HAM, SOUTHAMPTON-EVERTON!

EPL - LIGI KUU ENGLAND

Ratiba/Matokeo:

Jumapili Novemba 27

Watford 0 Stoke City 1                  

Arsenal 3 Bournemouth 1              

1930 Manchester United v West Ham United         

1930 Southampton v Everton

+++++++++++++++++++++++++++++

ARSE-BOURNEWAKIWA kwao Emirates, Arsenal Leo wameshinda Mechi yao ya EPL, Ligi Kuu England, kwa kuichapa Bourmouth Bao 3-1 na kuzidi kujichimbia Nafasi ya 4.

Arsenal sasa wana Pointi 28 na juu yao wapo Man City na Liverpool wenye Pointi 30 wakati Vinara Chelsea wana Pointi 31 baada ya Mechi 13 kwa kila Timu.

Arsenal walitangulia kupata Bao baada ya kosa kubwa la Beki wa Bournemouth Steve Cook kutoa pasi fyongo kwa Kipa wake na Alexis Sanchez kuinasa na kufunga kirahisi katika Dakika ya 12.

Bournemouth walirudi kwenye Mechi Refa Mike Jones alipowapa Penati katika Dakika ya 23 kutokana na Nacho Monreal kumwangusha Callum Wilson kwenye Boksi na Wilson kupiga na kufunga Penati hiyo.

Hadi Mapumziko Arsenal 1 Bournemouth 1.

Dakika ya 53, kazi nzuri ya Mesut Ozil na Nacho Monreal ilimfikia Theo Walcott alieipa Arsenal Bao la Pili kwa Kichwa na Bao la 3 kufungwa Dakika ya 91 na Alexis Sanchez alipolishwa na Olivier Giroud.

VIKOSI:

Arsenal: Cech. Debuchy [Gabriel16'], Mustafi, Koscielny, Monreal, Elneny, Xhaka, Walcott [Giroud 76'], Özil, Oxlade-Chamberlain [Ramseyat 75'], Sanchez

Akiba: Gibbs, Gabriel, Ramsey, Giroud, Ospina, Iwobi, Coquelin.

Bournemouth: Federici, A Smith, Francis, S Cook, B Smith [Mousset 81’], Gosling, Ake, Arter, King, C Wilson [Afobe 63'], Stanislas [Ibe 71']

Akiba: Pugh, Afobe, Allsop, Fraser, Mings, Mousset, Ibe

REFA: Mike Jones

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumamosi Desemba 3

1530 Manchester City v Chelsea      

1800 Crystal Palace v Southampton          

1800 Stoke City v Burnley              

1800 Sunderland v Leicester City              

1800 Tottenham Hotspur v Swansea City             

1800 West Bromwich Albion v Watford                

2030 West Ham United v Arsenal              

Jumapili Desemba 4

1630 Bournemouth v Liverpool                

1900 Everton v Manchester United            

Jumatatu Desemba 5

2300 Middlesbrough v Hull City       

         

BAADA KUTUPWA NJE UEFA CHAMPIONZ LIGI SPURS KUUKACHA UWANJA 'NUKSI' WEMBLEY!

WEMBLEYTottenham Hotspur sasa wanatafakari kutoutumia tena Uwanja wa Wembley Jijini London kwa ajili ya Mechi zao za Nyumbani za Mashindano ya Klabu ya UEFA Barani Ulaya.
Jana Spurs walifungwa 2-1 na Monaco huko France katika Mechi yao ya Kundi lao la UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI na kipigo hicho kuhakikisha wamo nje ya Mashindano licha ya kubakisha Mechi 1 ya Kundi.
Desemba 7 Spurs watacheza hiyo Mechi yao ya mwisho ya Kundi lao dhidi ya CSKA Moscow Uwanjani Wembley na ikiwa hawatofungwa Mechi hiyo basi watatupwa kucheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.
Kutupwa nje kwa Spurs kutoka UCL kumechangiwa hasa na Vipigo Viwili walivyoshushiwa na AS Monaco na Bayer Leverkusen Uwanjani Wembley.
Spurs walilazimika kutumia Wembley kutokana na UEFA kutoupasisha Uwanja wao wa Nyumbani White Hart Lane kutokana na Ujenzi wa Uwanja wao mpya ambao unapakana na hiyo White Hart Lane.
Baadhi ya Wadau wa Spurs, akiwemo Mchezaji wao Moussa Sissoko, wametaja sababu za kushindwa huko Wembley ni kutojisikia Nyumbani kikweli wakicheza humo.
Sasa wanataka Mechi zao za Nyumbani za UEFA EUROPA LIGI zichezwe huko White Hart Lane kitu ambacho UEFA wanaweza kukibariki tu ikiwa Uwanja huo utabanwa na kuzuia uwezo wake wa kuchukua Washabiki uwe Watazamaji 32,000 tu badala ya uwezo wake halisi wa Watu 36,284.

UCL: BEKI PSG AZUIWA KUINGIA UINGEREZA KUIVAA ARSENAL JUMATANO!

PSG-SERGE-AURIERBEKI wa Paris St Germain Serge Aurier amezuiwa kuingia Uingereza ambako Jumatano watacheza huko Emirates na Arsenal kwenye Mechi muhimu mno ya Kundi A la UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.

PSG imedai Beki huyo Raia wa Ivory Coast amezuiwa licha awali kupewa Viza kufuatia kupatikana na Hatia Makamani huko France Mwezi Mei kwa kosa la kumshambulia Afisa wa Polisi nje ya Naiti-Klabu na kuadhibiwa Miezi Miwili Jela lakini Kifungo hicho kikasitishwa.

Ingawa Arsenal na PSG zote zimefuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zikiwa na Mechi 2 mkononi, Mechi hii ni muhimu kuamua nani atatwaa Ushindi wa Kundi A.

++++++++++++++++++++++++++++

Timu 5 ambazo zimefuzu – Bado 11:

-Arsenal, Paris St Germain, Atletico Madrid, Bayern Munich, Borussia Dortmund

Timu ambazo zinaweza kufuzu Wiki hii zikibakiza Mechi 1 mkononi:

-Benfica, Napoli, Beşiktaş, Barcelona, Manchester City, Monaco, BayerLeverkusen,Real Madrid, Leicester City, Porto, Sevilla, Juventus

++++++++++++++++++++++++++++

Leo PSG imetoa Taarifa ambayo imeeleza Serge Aurier awali alipewa Viza ya Uingereza Oktoba 21 lakini hapo Novemba 16 Viza hiyo ikafutwa kwa sababu ya Hukumu hiyo ya Mwezi Mei.

++++++++++++++++++++++++++++++++

KUNDI A – Mahesabu yake kufuzu: Arsenal (Pointi 10, Imeshafuzu) v Paris Saint-Germain (10, Imeshafuzu), Ludogorets Razgrad (1) v Basel (1)

Yeyote atakaeshinda kati ya Arsenal na PSG atatwaa ushindi wa Kundi.

Yeyote atakaeshinda kati ya Ludogorets na Basel atatwaa ushindi wa 3.

++++++++++++++++++++++++++++++++

PSG imedai walipoomba Viza kwa Mchezaji wao huyo waliweka kinabagaubaga Kesi yake hiyo na pia licha ya Kifungo kusitishwa, Mchezaji huyo yupo kwenye Rufaa akipinga Hukumu hiyo ya Kifungo cha miezi Miwili kilichosimamishwa.

PSG, ikidai UEFA inawasapoti kwenye ishu hii, wameilaani Uingereza kwa kukosa heshima kwao licha ya juhudi zao kwa Wiki nzima kutaka msimamo huo ufutwe na wao kujulishwa hii Leo uamuzi wa mwisho kwa kumzuia Mchezaji huyo kuingia Uingereza.

Kwenye Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Parc des Princes Jijini Paris hapo Septemba 13, PSG ilifunga Bao Dakika ya Kwanza tu kupitia Edinson Cavani na Arsenal kusawazisha Dakika ya 78 kwa Bao la Alexis Sanchez.

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Ratiba Mechi za 5 za Makundi

***Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa

Jumanne 22 Novemba 2016

KUNDI E

2000 CSKA Moscow v Bayer 04 Leverkusen               

Monaco v Tottenham Hotspur

KUNDI F

Borussia Dortmund v Legia Warsaw                

Sporting Lisbon v Real Madrid               

KUNDI G

FC Copenhagen v FC Porto         

Leicester City v Club Brugge

KUNDI H

Dinamo Zagreb v Lyon               

Sevilla v Juventus             

Jumatano 23 Novemba 2016

KUNDI A

Arsenal v Paris Saint Germain               

Ludogorets Razgrad v FC Basel             

KUNDI B

2045 Besiktas v Benfica              

Napoli v Dynamo Kiev                

KUNDI C

Bor Monchengladbach v Manchester City

Celtic v Barcelona

KUNDI D

2000 FC Rostov v Bayern Munich           

Atlético Madrid v PSV Eindhoven           

Ratiba Mechi za 6 na za mwisho za Makundi

***Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku

Jumanne 6 Desemba 2016

KUNDI A

FC Basel v Arsenal

Paris Saint Germain v Ludogorets Razgrad                

KUNDI B

Benfica v Napoli               

Dynamo Kiev v Besiktas             

KUNDI C

Barcelona v Borussia Monchengladbach           

Manchester City v Celtic

KUNDI D

Bayern Munich v Atlético Madrid           

PSV Eindhoven v FC Rostov                  

Jumatano 7 Desemba 2016

KUNDI E

Bayer 04 Leverkusen v Monaco             

Tottenham Hotspur v CSKA Moscow                

KUNDI F

Legia Warsaw v Sporting Lisbon           

Real Madrid v Borussia Dortmund         

KUNDI G

Club Brugge v FC Copenhagen              

FC Porto v Leicester City

KUNDI H

Juventus v Dinamo Zagreb         

Lyon v Sevilla         

++++++++++++++++++++++++++++

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MAKUNDI:

Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba

Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba

Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba

Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba

Mechi ya Sita: 22 na 23 Novemba

Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba

MECHI ZA MTOANO:

11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza

18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

 

 

 

NINI WAMESEMA - TOURE NA GUARDIOLA, MOURINHO NA ROONEY!

CITY-TOUREBAOMARA baada ya Mechi za Jana za EPL, Ligi Kuu England, baadhi ya Wadau wa Mechi hizo walitoa matamshi mbalimbali yenye mvuto kwa Washabiki.
Baadhi ya hao ni Mameneja wa Man City Pep Guardiola na Mchezaji wake Yaya Toure aliempiga marufuku kucheza na ghafla Jana kumchezesha na Staa huyo kupiga Bao zote 2 na kuwapa ushindi City wa 2-1 dhidi ya Crystal Palace.
Pia Jose Mourinho, Meneja wa Man United ambae Jana walipokwa ushindi baada Arsenal kusawazisha Dakika ya 89 na kupata Sare 1-1 lakini hilo limeendeleza Rekodi ya Mourinho kutofungwa na Arsene Wenger katika Mechi 15 za EPL ambazo ameshinda 8 na Sare 7.
Vile vile, Nahodha wa Man United Wayne Rooney ambae pia ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya England aliongea kuhusu kusakamwa sana kwake.
NINI WAMESEMA?
-WAYNE ROONEY: 
Wayne Rooney amedai amekuwa akisakamwa mno wakati akiichezea England na hilo ni tendo la fedheha kubwa.
Rooney ameichezea England Mechi 119 akiwa ni wa pili katika Historia kwa kucheza Mechi nyingi nyuma ya Kipa Peter Shilton aliecheza Mechi 125 na pia ndie Mfungaji Bora katika Historia ya Nchi hiyo.
Hivi karibuni Jarida moja huko England lilitoa Picha za Rooney akinywa Pombe Hotelini waliyokuwa wakikaa Timu ya England ingawa Siku hiyo Kikosi chote kilikuwa kimepewa Ofu na Meneja Gareth Southgate.
Akiongea hapo Jana mara baada ya Mechi ya Man United na Arsenal, Rooney aliwashambulia wanaomsakama na kudai wanakosa heshima.
Alisema: "Inaonyesha kama Wanahabari wanaandika Wasifu wa Kifo changu na hilo sitaruhusu litokee. Yanayotokea ni fedheha. Napenda kuchezea Nchi yangu na naskia fahari mafanikio yangu. Bado sijaisha!"
Nao Wachezaji wa zamani wa England, Ian Wright na Alan Shearer, wamejitokeza kumpa sapoti Rooney.
Akiongea hapo Jana, Ian Wright, alisema: "Kwa Miaka Mitatu au Minne wamekuwa wakimshambulia. Nimefurahi mno sasa anajibu mapigo. Pigana Wayne!"
Nae Nahodha wa zamani wa England Alan Sherer amesema: "Siku zote amejitolea kwa nguvu zote kuichezea England. Kama alipewa Ofu na kuamua kubaki Hotelini na kupata kinywaji hakufanya kosa labda ingekuwa ameenda kinyume na Meneja!"
-YAYA TOURE:
Mara baada ya Jana kuchezeshwa kwa mara ya kwanza baada Miezi Mitatu baada kupigwa stopu na Meneja Pep Guardiola kufuatia ugomvi na Wakala wake, Yaya Toure ambae alifunga Bao zote 2 wakati Man City inaifunga Crystal Palace 2-1 amefunguka na kusema hakushangazwa kuitwa kuichezea tena Timu hiyo.
Toure, mwenye Miaka 33, ameeleza: "Nilikuwa tayari kiakili na nilijua ipo Siku Meneja ataniita!"
Toure, ambae ameiwezesha City kutwaa Ubingwa EPL mara 2, Jana alipokewa vizuri na Mashabiki wa Timu hiyo waliokuwa wakimuimba Mechi nzima.
Mwishoni mwa Mechi hiyo na Palace Wachezaji wote wa City walimshangilia Toure na kumsindikiza kwa Makofi hadi nje ya Uwanja.
-JOSE MOURINHO:
Kwa mujibu wa Meneja wa Man United Jose Mourinho Timu yao ndio Timu ambayo haina bahati baada ya Jana Arsenal kusawazisha Dakika ya 89 na kupata Sare ya 1-1.
Mourinho ameeleza: "Sina la kusema kuhusu Wachezaji wangu lakini nawaonea ruhuma kwani hiyo ni kama tumefungwa wakati Arsenal wanaona wameshinda!"
Aliongeza: "Sare hizi na Burnley, Stoke na Arsenal ni kupoteza Pointi 9. Tungepata Pointi 6 tu tuko 4 Bora na karibu ya kileleni! Tunajua hivi sasa sie ndio Timu isiyo na bahati kwenye EPL!"
Man United wameshapambana na Manchester City, Liverpool, Chelsea na Arsenal bila ushindi wakitoka Sare 3 na kufungwa na Chelsea tu.
Hivi sasa wapo Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 5 nyuma ya Arsenal ambao wako Nafasi ya 4 na ambao wapo Pointi 2 nyuma ya Vinara Liverpool.

PATASHIKA MWAKA MPYA, LIVERPOOL WAGOMEWA KUBADILI RATIBA MECHI ZAO 2 ZA NDANI YA SIKU 2!

>>JURGEN KLOPP ‘ALIA’!!

NI KAWAIDA England kucheza Mechi zao za Ligi Majira ya Baridi tofauti na La Liga ya Spain, Bundesliga ya Germany na KLOPP-LIVER-1STSerie A ya Italy ambazo huenda Vakesheni kipindi hicho.

Na ni kawaida sana kwa Mechi za Ligi Kuu England kuchezwa Krismasi, Mkesha wa Mwaka Mpya na hata Mwaka Mpya wenyewe.

Msimu huu Liverpool watacheza na Man City Desemba 31 wakiwa kwao Anfield na Januari 2 kutembelea huko Stadium of Light kuikwaa Sunderland.

Mechi yao ya Anfield na City itaanza Saa 2 na Nusu Usiku hiyo Desemba 31 na ile ya Januari 2 Filimbi itapulizwa 12 Jioni, zote Saa za Bongo.

Liverpool waliiomba Ligi Kuu England ibadili Ratiba hiyo na kukataliwa na kisha kuomba angalau Mechi yao na Sunderland isianze mapema ili angalau wapate Masaa kadhaa ya ziada ya kupumzika.

Maombi yote hayo yamekataliwa kwa misingi kwamba wakikubaliwa basi kila Klabu itakuja na ombi lake la aina hiyo hiyo.

Vile vile, Liverpool wanaona kama wanakandamizwa kwani Mechi yao na Stoke City ambayo ilipangwa kuchezwa Desemba 26 ikasogezwa hadi Desemba 27.

++++++++++++++++++++++

EPL, Ligi Kuu England

Ratiba ya Kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya

**Saa za Bongo

Jumatatu 26 Desemba 2016

1530 Watford v Crystal Palace

1800 Arsenal v West Brom          

1800 Burnley v Middlesbrough              

1800 Chelsea v Bournemouth               

1800 Leicester v Everton            

1800 Man United v Sunderland             

1800 Swansea v West Ham                  

2015 Hull v Man City

Jumanne 27 Desemba 2016

2015 Liverpool v Stoke

Jumatano 28 Desemba 2016

2245 Southampton v Tottenham

Ijumaa 30 Desemba 2016

2300 Hull v Everton                             

Jumamosi 31 Desemba 2016

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke                 

1800 Leicester v West Ham                  

1800 Man United v Middlesbrough                  

1800 Southampton v West Brom           

1800 Swansea v Bournemouth

2030 Liverpool v Man City          

Jumapili 1 Januari 2017

1630 Watford v Tottenham

1900 Arsenal v Crystal Palace

Jumatatu 2 Januari 2017

1530 Middlesbrough v Leicester

1800 Everton v Southampton               

1800 Man City v Burnley             

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Brom v Hull               

2015 West Ham v Man United

Jumanne 3 Januari 2017

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea

2300 Stoke v Watford

Jumatano 4 Januari 2017

2300 Tottenham v Chelsea          

++++++++++++++++++++++

Meneja wa Liverpool kutoka Germany, Jurgen Klopp, amelalama: “Masaa 48 ni mtihani lakini chini ya Masaa 48 ni kitu huwezi kuamini. Masaa 48 kati ya Mechi 2? Hili linawezekanaje? Unatayarisha vipi Timu?”

Aliongeza: “Kila Mtu anauliza kwanini England haifanikiwi Mashindano makubwa? Uliza Nchi nyingine kubwa zinafanya nini kipindi hicho – wapo miguu juu, wamelala kwenye Sofa kutazama Soka la England!”