EPL: LEO MECHI 4, JUMAPILI MAN UNITED UGENINI NA BURNLEY, LIVERPOOL NA PALACE HUKO ANFIELD!

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Jumamosi Aprili 22

1700 Bournemouth v Middlesbrough               

1700 Hull City v Watford            

1700 Swansea City v Stoke City            

1700 West Ham United v Everton

++++++++++++++++++++++++    

EPL-2016-17-LOGO2WAKATI Nusu Fainali za EMIRATES FA CUP zikipigwa Leo na Kesho, EPL, Ligi Kuu England, itaendelea kwa Mechi 6 Leo na Jumapili.

Hii Leo zipo Mechi 4 ambapo Bournemouth watakuwa Wenyeji wa Middlesbrough, Hull City kuikaribisha Watford, Swansea City kuialika Stoke City na West Ham kuwa Wenyeji wa Everton.

Hapo Kesho zipo Mechi 2 na Burnley watakuwa Wenyeji wa Man United na kisha huko Anfield ni Liverpool na Crystal Palace.

EPL inaongozwa na Chelsea wenye Pointi 75 wakifuata Spurs wenye 74 kisha ni Liverpool wenye 66, Wa 4 ni Man City wenye 64 na Man United ni wa 5 wakiwa na Pointi 60.

EPL, LIGI KUU ENGLANDEPL-APR18

Jumapili Aprili 23

1615 Burnley v Manchester United                 

1830 Liverpool v Crystal Palace             

Jumanne Aprili 25

2145 Chelsea v Southampton               

Jumatano Aprili 26

2145 Arsenal v Leicester City                

2145 Middlesbrough v Sunderland                  

2200 Crystal Palace v Tottenham Hotspur                 

Alhamisi Aprili 27

2200 Manchester City v Manchester United               

Jumamosi Aprili 29

1700 Southampton v Hull City              

1700 Stoke City v West Ham United                

1700 Sunderland v Bournemouth          

1700 West Bromwich Albion v Leicester City              

1930 Crystal Palace v Burnley               

Jumapili Aprili 30

1400 Manchester United v Swansea City         

1605 Everton v Chelsea              

1605 Middlesbrough v Manchester City           

1830 Tottenham Hotspur v Arsenal                 

Jumatatu Mei 1

2200 Watford v Liverpool

KEPTENI JOHN TERRY BAIBAI CHELSEA, MWENYEWE NA KLABU ZATHIBITISHA!

TERRY-KEPTENI-CHELSEANAHODHA wa Chelsea John Terry ataondoka Klabuni hapo baada ya kudumu kwa Miaka 20.

Mkataba wa Terry ulimalizika Mwaka Jana na akapewa Nyongeza ya Mwaka Mmoja Mwezi Mei 2016.

Terry, mwenye Miaka 36, pamoja na Chelsea, zimethibitisha kung’atuka kwa Mchezaji huyo ambae ndie ametwaa Mataji mengi kupita Mchezaji yeyote katika Historia ya Klabu hiyo.

Terry ameshinda Ubingwa wa England mara 4, UEFA CHAMPIONZ LIGI 1, FA CUP 5, EUROPA LIGI 1 na Kombe la Ligi mara 3.

Alianza kuichezea Chelsea kwa mara ya kwanza 1998 na kucheza Mechi 713 na kati ya hizo 578 kama Nahodha.

Terry ameeleza: “Najisikia bado naweza kucheza lakini hapa Chelsea sitapata nafasi nyingi!”

Terry, ambae ni Sentahafu, amefunga Bao 66 akiwa na Chelsea alikoanza kucheza akiwa na Miaka 14 lakini Msimu huu ameanza Mechi 4 tu za EPL, Ligi Kuu England.

Beki huyo ndie anaeshika nafasi ya 3 kwa kucheza Mechi nyingi hapo Chelsea katika Historia akiwa nyuma ya Ron Harris na Peter Bonetti.

Terry alistaafu kuichezea Timu ya Taifa ya England Mwaka 2012 alipoichezea Mechi 78.

TUZO MCHEZAJI BORA: KANE, LUKAKU, IBRAHIMOVIC, SANCHEZ, HAZARD, KANTE WAGOMBEA!

PFA-TUZOCHAMA CHA WACHEZAJI WA KULIPWA huko England PFA, Leo kimetoa orodha ya Wachezaji 6 ambao watagombea Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Msimu huu.
6 hao ni Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic, Alexis Sanchez, Eden Hazard na N'Golo Kante.
Msimu uliopita Riyad Mahrez wa Leicester City alishinda Tuzo hii.
Kane na Lukaku pia wamo kwenye Listi ya Wgombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Vijana pamoja na Michael Keane, Leroy Sane, Jordan Pickford na Dele Alli ambae ni Mshindi wa Tuzo hii kwa Msimu uliopita.
Washindi wa Tuzo hizi 2 watatangazwa Aprili 23.
WAGOMBEA:
Tuzo Mchezaji Bora
Eden Hazard - Chelsea
Zlatan Ibrahimovic - Manchester United
Harry Kane - Tottenham Hotspur
N'Golo Kante - Chelsea
Romelu Lukaku - Everton
Alexis Sanchez - Arsenal
Tuzo Mchezaji Bora Vijana
Dele Alli - Tottenham Hotspur
Harry Kane - Tottenham Hotspur
Michael Keane - Burnley
Romelu Lukaku - Everton
Jordan Pickford - Sunderland
Leroy Sane - Manchester City

PALACE YAINYUKA ARSENAL NA KUITUPA NAFASI YA 6, MASHABIKI WALIA WENGER ATIMUE!

PALACE-WENGERJANA huko Selhurst Park Jijini London Crystal Palace iliwatandika Arsenal Bao 3-0 na kuzidi kujiweka salama kubakia EPL, Ligi Kuu England na kuwaacha Arsenal wakigalagala Nafasi ya 6 wakiiota 4 Bora.

Kipigo hicho kimeamsha tena hisia za baadhi ya Mashabiki wa Arsenal wakitaka Meneja wao Arsene Wenger aondoke Klabuni hapo katika Msimu huu ambao ni wa 20 kwake na ambao kwa mara ya kwanza katika Kipindi chote hicho wapo hatarini kuikosa 4 Bora na hivyo kukosa kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.

Mkataba wa Wenger na Arsenal unakwisha Juni nab ado hamna uthibitisho kama kasaini Nyongeza ya Miaka Miwili ambayo Arsenal imeshampa.

Katika Mechi hiyo, Crystal Palace, chini ya Meneja wa zamani wa England Sam Allardyce, maarufu kama Big Sam, walipachika Bao la Kwanza Dakika ya 17 kupitia Andros Townsend na Bao hilo kudumu hadi Haftaimu.EPL-APR11

Kipindi cha Pili Palace walipiga Bao 2 zaidi Wafungaji wakiwa Yohan Cabaye, Dakika ya 63, na Luka Milivojevic, kwa Penati ya Dakika ya 68.

VIKOSI:

Crystal Palace:Hennessey, Ward, Kelly, Sakho, Schlupp, Milivojevic, Cabaye, Zaha, Puncheon, Townsend, Benteke.
Akiba: Speroni, Flamini, McArthur, Fryers, KaiKai, Sako, Delaney.

Arsenal:Martinez, Bellerín, Mustafi, Gabriel, Monreal, Xhaka, Elneny, Walcott, Özil, Welbeck, Sánchez.
Akiba:Gibbs, Mertesacker, Ramsey, Giroud, Oxlade-Chamberlain, Coquelin, Macey.
REFA:Michael Oliver

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:

Jumamosi Aprili 15

1430 Tottenham Hotspur v Bournemouth                  

1700 Crystal Palace v Leicester City                

1700 Everton v Burnley     

1700 Stoke City v Hull City

1700 Sunderland v West Ham United              

1700 Watford v Swansea City               

1930 Southampton v Manchester City             

Jumapili Aprili 16

1530 West Bromwich Albion v Liverpool 

1800 Manchester United v Chelsea        

Jumatatu

2200 Middlesbrough v Arsenal              

PIGO KUU LIVERPOOL: JURGEN KLOPP ATOBOA SADIO MANE KUTOCHEZA TENA LIVERPOOL MSIMU HUU!

LIVERPOOL-MANE-GONJWALiverpool wamethibitisha kuwa Fowadi wao Sadio Mane hatocheza tena Msimu huu uliobaki baada ya Jumamosi iliyopita kuumia Goti kwenye Mechi waliyowachapa Everton 3-1.

Fowadi huyo kutoka Senegal mwenye Miaka 24 na ambae ndie tegemeze kubwa la Liverpool na ambae ndie aliewafungia Bao la Kwanza kwenye Mechi hiyo na Everton aliumia baada kuvaana na Leighton Baines wa Everton.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ana hakika Mane anahitaji upasuaji na itakuwa ngumu kwake kucheza tena Msimu huu unaokwisha Mwezi ujao.

Mane, aliesainiwa kutoka Southampton kwa Dau la Pauni Milioni 34, amecheza Mechi zote za Liverpool Msimu huu kasoro 5 tu.

Kati ya Mechi hizo, 3 zilikuwa Sare na 2 wamefungwa na kuwaacha Liverpool wakiwa Nafasi ya 3 kwenye EPL, Ligi Kuu England, wakiwa na Pointi 60 kwa Mechi 31 wakiwa Pointi 12 nyuma ya Vinara Chelsea.

Fowadi huyo anaungana na Majeruhi wengine Jordan Henderson na Adam Lallana ambao wamepelekwa huko USA kwa matibabu zaidi.

Mchezaji mwingine alieumia kwenye Mechi hiyo na Everton ni Kiungo Emre Can ambae ameshindwa kufanya hata Mazoezi kutokana na maumivu ya Goti.

Lakini habari njema kwa Liverpool ni kuanza tena Mazoezi kwa Straika wao Daniel Sturridge ambae kitambo yuko nje kwa maumivu na upo uwezekano akawepo Benchi Jumatano wakiivaa Bournemouth.