MOURINHO AUNGAMA KUTOMFIKIA SIR ALEX!

SIRALEXvMOURINHOJose Mourinho ameungama kutoifikia Rekodi ya Sir Alex Ferguson ya kutwaa Mataji 13 ya Ligi Kuu England na kukiita ni kitu 'kisichowezekana.'

Jumapili, Jose Mourinho aliiongoza Chelsea kutwaa Ubingwa wake wa 3 wa Ĺigi Kuu England akiwa na Klabu hiyo baada ya kuifinga Crystal Palace 1-0.

Sir Alex alikuwa na Miaka 51 alipoanza kuiongoza Manchester United kutwaa Taji la kwanza la Ligi Kuu England Msimu wa 1992/93 na kuendelea kubeba mengine 12 baada ya hapo.

Hivi sasa Mourinho ana Miaka 52 na pamoja na Taji la Msimu huu alishatwaa Mataji mengine mawili akiwa na Chelsea katika kipindi chake cha kwanza katika Misimu ya 2004/05 na 2005/06.

Akiongea na BT Sport, Mourinho alisema: "Nina safari ndefu ya kwenda lakini Sir Alex ameacha kiwango cha juu ambacho hakiwezekani kwa yeyote. Siwezi kutwaa Mataji 13 ya Ligi Kuu England!"

Aliongeza: "Naweza kutwaa Ubingwa mara 13. Naweza. Ninayo Mataji 8. Naweza kufikia 13. Lakini Mataji 13 ya Ligi Kuu England, hapana, haiwezekani!"

Mourinho ameshatwaa Ubingwa huko Portugal mara 2 akiwa na FC Porto, mara 2 huko Italy akiwa na Inter Milan, mara 1 Nchini Spain akiwa na Real Madrid na hizi 3 za Chelsea.

MOURINHO- UBINGWA NI ZAWADI YA KUKABILI HATARI!

MOURINHO-MIMACHOJose Mourinho, Meneja wa Mabingwa wapya wa England Chelsea, amesema kuutwaa Ubingwa huo hapo Jana ni zawadi yake kwa kuikabili hatari ya kurudi tena kuiongoza Chelsea kwa mara ya pili.

Mourinho alitwaa Ubingwa mara mbili katika Misimu ya 2004/5 na 2005/6 alipokuwa Meneja wa Chelsea kwa mara ya kwanza kati ya 2004 na 2007 na sasa kurudi tena 2013 na kuiwezesha Chelsea kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya 4 na mara ya kwanza tangu 2010.

Akiongea Jana baada ya Chelsea kuifunga Crystal Palace Bao 1-0 Uwanjani Stamford Bridge kwa Bao la Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA, Eden Hazard, na kutwaa Ubingwa huku wakiwa na Mechi 3 mkononi, Mourinho alisema: "Ukirudi kule ulikopata mafanikio unahatarisha mafanikio na historia yako lakini mimi nimeikabili hatari hiyo na sasa naweza kusema nimeshinda!"

Aliongeza: "Ningeweza kwenda Nchi nyingine yenye Ligi laini lakini nliamua kurudi kwenye Ligi ngumu ambako kabla nlikuwa na furaha!"

Kuhusu kubaki kwake Chelsea, Mourinho alisema hilo ataamua Mmiliki wa Klabu Roman Abramovitch.

YANGA NJE!

YANGA-TEAMMABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, Jana Usiku walitolewa nje ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho baada kufungwa 1-0 na Etoile Du Saheli huko Sousse, Tunisia katika Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Yanga wametupwa nje kwa Jumla ya Mabao 2-1 baada ya kutoka Sare 1-1 kwenye Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Bao la ushindi la Etoile Du Sahel lilifungwa na Ammar Jemal katika Dakika ya 24 na licha ya Yanga kucheza vizuri walishindwa kufunga.
Etoile Du Sahel sasa wanasonga Raundi ijayo ya Mtoano ambapo watapangiwa moja ya Timu 8 zitakazotolewa CAF CHAMPIONZ LIGI na Washindi wa Raundi hiyo watacheza Mechi za Makundi.
CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:
RATIBA/MATOKEO
**Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Matokeo katika Mechi Mbili.
Ijumaa Mei 1
Etancheite -Congo DR 0 Wari Wolves - Nigeria 1 [1-3]
Club Africain - Tunisia 1 Association Sportive Olympique de Chlef - Algeria 0 [2-1] 
Jumamosi Mei 2
E.S. Sahel 1 Yanga 0 [2-1]
Mechi nyingine:
ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast v Onze Createurs - Mali [1-0] 
Hearts of Oak - Ghana v Djoliba AC - Mali [2-1]
Orlando Pirates - South Africa 3 CF Mounana - Gabon 0 [5-2]
Fath Union Sport de Rabat - Morocco v Al Zamalek - Egypt [0-0]
AS Vita Club Congo DR v Royal Leopards - Swaziland [0-1]
 

LEO USIKU YANGA WAKO SOUSSE, KUIBWAGA ETOILE DU SAHEL?

YANGA-TEAMMABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, Leo hii wako Stade Olympique Sousse Mjini Sousse Nchini Tunisia kurudiana na Etoile Du Sahel kwenye Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Yanga na Etoile Du Sahel zilitoka Bao 1-1 na Bao hizo zilifungwa na Kepteni wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' kwa Penati na Etoile kusawazisha kwa Bao la Mohamed Amine Ben Amor.
Mechi hii ya Leo itaanza Saa 3 Usiku, kwa Saa za Bongo, na ili kusonga mbele Yanga wanahitaji ushindi au Sare ya Bao nyingi kuanzia 2-2.
Wakati Kocha wa Yanga kutoka Holland, Hans van der Pluijm, akisisitiza wana kazi ngumu na wanahitaji kupigana, Kocha wa Etoile du Sahel, Faouzi Benzarti, ametamba kazi yao ni nyepesi.
Kikosi cha Yanga kilichokwenda Tunisia ni:
Makipa: Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’
Mabeki : Pato Ngonyani, Oscar Joshua, Edward Charles, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ’Juma Abdul, Rajab Zahir, Mbuyu Twite na Kevin Yondan.
Viungo: Nizar Khalfan, Andrey Coutinho, Salum Telela na Said Juma ‘Makapu’
Mastraika: Hussein Javu, Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Mrisho Ngasa, Jerry Tegete na Simon Msuva.
CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:
RATIBA/MATOKEO
**Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Matokeo katika Mechi Mbili.
Ijumaa Mei 1
Etancheite -Congo DR 0 Wari Wolves - Nigeria 1 [1-3]
Club Africain - Tunisia 1 Association Sportive Olympique de Chlef - Algeria 0 [2-1] 
Jumamosi Mei 2
 **Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
2100 E.S. Sahel v Yanga
Mechi nyingine:
ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast v Onze Createurs - Mali [1-0] 
Hearts of Oak - Ghana v Djoliba AC - Mali [2-1]
Orlando Pirates - South Africa v CF Mounana - Gabon [2-2]
Fath Union Sport de Rabat - Morocco v Al Zamalek - Egypt [0-0]
AS Vita Club Congo DR v Royal Leopards - Swaziland [0-1]
 

YANGA KUPEWA KOMBE LA UBINGWA MEI 6 KWENYE MECHI NA AZAM FC!

>>PATA KIKOSI KILICHOENDA TUNISIA KUIVAA ETOILE DU SAHEL!

YANGA MJENGO-2MABINGWA wa Soka Tanzania Bara, Yanga, watakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom hapo Mei 6 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam watakapocheza na Mabingwa wa zamani Azam FC katika Mechi ya Ligi.

Yanga walitwaa Ubingwa wa Msimu huu wa 2014/15 Juzi huku wakiwa na Mechi 2 mkononi baada ya kuichapa Polisi Moro na kufikisha Pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na Timu ya Pili Azam FC.

Kwa mujibu wa TFF, Yanga watakabidhiwa Kombe lao na Waziri wa Habari, Vijana Utamuduni na Michezo, Dokta Fennela Mukangara.

Yanga hivi sasa wameelekea Nchini Tunisia ambako Wikiendi hii Mjini Sousse watacheza Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho na Etoile Du Sahel.

Timu hizi zilitoka Sare 1-1 Mjini Dar es Salaam na ili Yanga wafuzu wanahitaji ushindi au Sare yeyote ya kuanzia 2-2.

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema kutwaa Ubingwa ni jambo la kujivunia kwake na Wachezaji lakini bado wana kazi kubwa kwenye michuano ya Klabu Afrika.

Kikosi cha Yanga kilichokwenda Tunisia ni:

Makipa: Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’

Mabeki : Pato Ngonyani, Oscar Joshua, Edward Charles, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ’Juma Abdul, Rajab Zahir, Mbuyu Twite na Kevin Yondan.

Viungo: Nizar Khalfan, Andrey Coutinho, Salum Telela na Said Juma ‘Makapu’

Mastraika: Hussein Javu, Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Mrisho Ngasa, Jerry Tegete na Simon Msuva.