KEPTENI JOHN TERRY BAIBAI CHELSEA, MWENYEWE NA KLABU ZATHIBITISHA!

TERRY-KEPTENI-CHELSEANAHODHA wa Chelsea John Terry ataondoka Klabuni hapo baada ya kudumu kwa Miaka 20.

Mkataba wa Terry ulimalizika Mwaka Jana na akapewa Nyongeza ya Mwaka Mmoja Mwezi Mei 2016.

Terry, mwenye Miaka 36, pamoja na Chelsea, zimethibitisha kung’atuka kwa Mchezaji huyo ambae ndie ametwaa Mataji mengi kupita Mchezaji yeyote katika Historia ya Klabu hiyo.

Terry ameshinda Ubingwa wa England mara 4, UEFA CHAMPIONZ LIGI 1, FA CUP 5, EUROPA LIGI 1 na Kombe la Ligi mara 3.

Alianza kuichezea Chelsea kwa mara ya kwanza 1998 na kucheza Mechi 713 na kati ya hizo 578 kama Nahodha.

Terry ameeleza: “Najisikia bado naweza kucheza lakini hapa Chelsea sitapata nafasi nyingi!”

Terry, ambae ni Sentahafu, amefunga Bao 66 akiwa na Chelsea alikoanza kucheza akiwa na Miaka 14 lakini Msimu huu ameanza Mechi 4 tu za EPL, Ligi Kuu England.

Beki huyo ndie anaeshika nafasi ya 3 kwa kucheza Mechi nyingi hapo Chelsea katika Historia akiwa nyuma ya Ron Harris na Peter Bonetti.

Terry alistaafu kuichezea Timu ya Taifa ya England Mwaka 2012 alipoichezea Mechi 78.

TUZO MCHEZAJI BORA: KANE, LUKAKU, IBRAHIMOVIC, SANCHEZ, HAZARD, KANTE WAGOMBEA!

PFA-TUZOCHAMA CHA WACHEZAJI WA KULIPWA huko England PFA, Leo kimetoa orodha ya Wachezaji 6 ambao watagombea Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Msimu huu.
6 hao ni Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic, Alexis Sanchez, Eden Hazard na N'Golo Kante.
Msimu uliopita Riyad Mahrez wa Leicester City alishinda Tuzo hii.
Kane na Lukaku pia wamo kwenye Listi ya Wgombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Vijana pamoja na Michael Keane, Leroy Sane, Jordan Pickford na Dele Alli ambae ni Mshindi wa Tuzo hii kwa Msimu uliopita.
Washindi wa Tuzo hizi 2 watatangazwa Aprili 23.
WAGOMBEA:
Tuzo Mchezaji Bora
Eden Hazard - Chelsea
Zlatan Ibrahimovic - Manchester United
Harry Kane - Tottenham Hotspur
N'Golo Kante - Chelsea
Romelu Lukaku - Everton
Alexis Sanchez - Arsenal
Tuzo Mchezaji Bora Vijana
Dele Alli - Tottenham Hotspur
Harry Kane - Tottenham Hotspur
Michael Keane - Burnley
Romelu Lukaku - Everton
Jordan Pickford - Sunderland
Leroy Sane - Manchester City

PALACE YAINYUKA ARSENAL NA KUITUPA NAFASI YA 6, MASHABIKI WALIA WENGER ATIMUE!

PALACE-WENGERJANA huko Selhurst Park Jijini London Crystal Palace iliwatandika Arsenal Bao 3-0 na kuzidi kujiweka salama kubakia EPL, Ligi Kuu England na kuwaacha Arsenal wakigalagala Nafasi ya 6 wakiiota 4 Bora.

Kipigo hicho kimeamsha tena hisia za baadhi ya Mashabiki wa Arsenal wakitaka Meneja wao Arsene Wenger aondoke Klabuni hapo katika Msimu huu ambao ni wa 20 kwake na ambao kwa mara ya kwanza katika Kipindi chote hicho wapo hatarini kuikosa 4 Bora na hivyo kukosa kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.

Mkataba wa Wenger na Arsenal unakwisha Juni nab ado hamna uthibitisho kama kasaini Nyongeza ya Miaka Miwili ambayo Arsenal imeshampa.

Katika Mechi hiyo, Crystal Palace, chini ya Meneja wa zamani wa England Sam Allardyce, maarufu kama Big Sam, walipachika Bao la Kwanza Dakika ya 17 kupitia Andros Townsend na Bao hilo kudumu hadi Haftaimu.EPL-APR11

Kipindi cha Pili Palace walipiga Bao 2 zaidi Wafungaji wakiwa Yohan Cabaye, Dakika ya 63, na Luka Milivojevic, kwa Penati ya Dakika ya 68.

VIKOSI:

Crystal Palace:Hennessey, Ward, Kelly, Sakho, Schlupp, Milivojevic, Cabaye, Zaha, Puncheon, Townsend, Benteke.
Akiba: Speroni, Flamini, McArthur, Fryers, KaiKai, Sako, Delaney.

Arsenal:Martinez, Bellerín, Mustafi, Gabriel, Monreal, Xhaka, Elneny, Walcott, Özil, Welbeck, Sánchez.
Akiba:Gibbs, Mertesacker, Ramsey, Giroud, Oxlade-Chamberlain, Coquelin, Macey.
REFA:Michael Oliver

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:

Jumamosi Aprili 15

1430 Tottenham Hotspur v Bournemouth                  

1700 Crystal Palace v Leicester City                

1700 Everton v Burnley     

1700 Stoke City v Hull City

1700 Sunderland v West Ham United              

1700 Watford v Swansea City               

1930 Southampton v Manchester City             

Jumapili Aprili 16

1530 West Bromwich Albion v Liverpool 

1800 Manchester United v Chelsea        

Jumatatu

2200 Middlesbrough v Arsenal              

PIGO KUU LIVERPOOL: JURGEN KLOPP ATOBOA SADIO MANE KUTOCHEZA TENA LIVERPOOL MSIMU HUU!

LIVERPOOL-MANE-GONJWALiverpool wamethibitisha kuwa Fowadi wao Sadio Mane hatocheza tena Msimu huu uliobaki baada ya Jumamosi iliyopita kuumia Goti kwenye Mechi waliyowachapa Everton 3-1.

Fowadi huyo kutoka Senegal mwenye Miaka 24 na ambae ndie tegemeze kubwa la Liverpool na ambae ndie aliewafungia Bao la Kwanza kwenye Mechi hiyo na Everton aliumia baada kuvaana na Leighton Baines wa Everton.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ana hakika Mane anahitaji upasuaji na itakuwa ngumu kwake kucheza tena Msimu huu unaokwisha Mwezi ujao.

Mane, aliesainiwa kutoka Southampton kwa Dau la Pauni Milioni 34, amecheza Mechi zote za Liverpool Msimu huu kasoro 5 tu.

Kati ya Mechi hizo, 3 zilikuwa Sare na 2 wamefungwa na kuwaacha Liverpool wakiwa Nafasi ya 3 kwenye EPL, Ligi Kuu England, wakiwa na Pointi 60 kwa Mechi 31 wakiwa Pointi 12 nyuma ya Vinara Chelsea.

Fowadi huyo anaungana na Majeruhi wengine Jordan Henderson na Adam Lallana ambao wamepelekwa huko USA kwa matibabu zaidi.

Mchezaji mwingine alieumia kwenye Mechi hiyo na Everton ni Kiungo Emre Can ambae ameshindwa kufanya hata Mazoezi kutokana na maumivu ya Goti.

Lakini habari njema kwa Liverpool ni kuanza tena Mazoezi kwa Straika wao Daniel Sturridge ambae kitambo yuko nje kwa maumivu na upo uwezekano akawepo Benchi Jumatano wakiivaa Bournemouth.

JESUS ARUDI CITY, SHAW KUNDINI MAN UNITED LEO NA EVERTON!

CITY-JESUSWAKATI Straika wa Manchester City Gabriel Jesus akiripotiwa kuanza tena Mazoezi baada kuuguza Kidole cha Mguu wake kilichovunjika, Fulbeki wa Manchester United Luke Shaw yumo kundini kwenye Kikosi cha Leo ambacho kitaivaa Everton licha Juzi kupondwa hadharani na Meneja wake.

PATA RIPOTI KAMILI:

JESUS ARUDI CITY

Straika wa Manchester City Gabriel Jesus ameripotiwa kuanza tena Mazoezi baada kuuguza Kidole cha Mguu wake kilichovunjika katika Dakika ya 14 ya Mechi ya City na Bournemouth hapo Februari 13.

Awali ilihofiwa kuwa Mbrazil huyo ataukosa Msimu wote uliobakia lakini Jana, wakati akitimiza Miaka 20 ya Kuzaliwa kwake, alirejea Mazoezini kwenye Klabu yake.

Fowadi huyo alianza kwa makeke hapo City baada kujiunga nao Mwezi Januari kwa Dau la Pauni Milioni 27 akitokea Palmeiras ya Brazil na kufunga Bao 3 katika Mechi zake 4 za kwanza.

Moto huo ulizusha uvumi kuwa sasa ni mwisho wa Muargentina Sergio Aguero umefika licha ya Straika huyo kuwa hapo City tangu 2011 na kupachika Mabao 154.

Bilas haka Jesus akiwa fiti kabisa, Aguero atarejea tena Benchi.

SHAW KUNDINI MAN UNITED LEO NA EVERTON!

Luke Shaw amejiunga na Kikosi cha Manchester United ambacho Leo kitacheza Uwanjani Old Trafford na Everton kwenye Mechi ya EPL, Ligi KuuMANUNITED-SHAW-AUMIZWA-PSV England, licha ya Juzi kupondwa na Meneja wa Timu hiyo Jose Mourinho kwamba hajitumi.

Shaw, Fulbeki wa Kushoto mwenye Miaka 21, ameichezea Man United mara 15 Msimu huu na hajaonekana Uwanjani tangu walipotoka 1-1 na Bournemouth Mwezi uliopita.

Juzi Mourinho alidai Shaw hawezi kulinganishwa vizuri na Mabeki wengine kama kina Ashley Young, Matteo Darmian na Daley Blind.

Mourinho amefunguka: “Siwezi kulinganisha jinsi anavyofanya Mazoezi, anavyojituma, mkazo na nia yake. Yuko nyuma mno!”

Mourinho alihojiwa kama Shaw, Mchezaji wa Kimataifa wa England, anahitaji kujisukuma zaidi na akajibu: “Joe Hart ni Mchezaji wa Kimataifa wa England na yupo kwa Mkopo Italy!”

Shaw alijiunga na Man United Juni 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 27 na Septemba 2015 alivunjika Mguu wake sehemu 2 na kuwa nje kwa karibu Mwaka mzima.

Mwezi Novemba, Mourinho alimponda Beki huyo aliposema yeye mwenyewe hayuko tayari kucheza Mechi ya Ligi dhidi ya Swansea City.

Inaaminika Jana Mourinho alikutana na Shaw huko Carrington, Kituo cha Mazoezi cha Man United, na baadae Mchezaji huyo akaonekana akiingia Hotelini Jijini Manchester ambako Kikosi cha Man United hupiga Kambi kabla ya Mechi zao.

Kupondwa kwa Shaw hadharani kulizua mjadala mkali huko England na Mchambuzi wa Kituo cha TV cha Sky Sports ambae ni Beki wa zamani wa Man United, Gary Neville, alisema hatima ya Mchezaji huyo kubakia Klabuni hapo kutategemea na jinsi atakavyoibuka baada ya lawama hizo.

Neville amesema kwa Mchezaji wa Kulipwa kuambiwa hujitumi Mazoezini ni kipondo kikubwa na unabidi ujitume kwa kuongeza bidii na kuonyesha uwezo Uwanjani ukiptaka nafasi.

 

 

 

Habari MotoMotoZ