JUAN MATA, CHRIS SMALLING, PHIL JONES NJE MAN UNITED!

>>MATA AFANYIWA OPERESHENI!

MANUNITED-CARRINGTON-APR1Mbali ya kukabwa na Ratiba ngumu ambapo Mwezi Aprili watacheza Mechi 9, Manchester United sasa inakabiliwa na safu inayoongezeka ya Majeruhi baada ya Kiungo Juan Mata kuungana na Mabeki Chris Smalling na Phil Jones kuwa nje.

Man United ilitangaza Jana kuwa Mata, mwenye Miaka 28, anapaswa kufanyiwa Upasuaji ili kutibu Nyonga yake.

Jones, mwenye Miaka 25, ameripotiwa kuumia Kidole cha Mguu wakati Smalling, mwenye Miaka 27, ana tatizo la Mguu na Meneja wa Man United Jose Mourinho amesema Masentahafu hao watakuwa nje kwa ‘muda mrefu’.

Mchezaji mwingine Majeruhi ni Paul Pogba anaesumbuliwa na tatizo la Musuli za Pajani.EPL-MAR18C

Lakini Kepteni Wayne Rooney, mwenye Miaka 31, anarejea baada ya kukosa Mechi 4 zilizopita akiuguza Goti lake na Leo anaweza kuikabili West Brom kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

Hata hivyo, Man United hii Leo itawakosa Straika Zlatan Ibrahimovic na Kiungo Ander Herrera ambao wako Kifungoni lakini ndio Mechi ya mwisho ya Vifungo vyao Vya Mechi 3 na 2.

MAN UNITED – Ratiba Aprili 2017:

**Saa za Bongo

01 APR:Man United v West Bromwich Albion, EPL, Saa 1700

04 APR:Man United v Everton, EPL, 2200

09 APR:Sunderland v Man United, EPL, 1530

13 APR:Anderlecht v Man United, Europa Ligi Robo Fainali, 2205

16 APR:Man United v Chelsea, EPL, 1800

20 APR:Man United v Anderlecht, Europa Ligi Robo Fainali, 2205

23 APR:Burnley v Man United, EPL, 1615

27 APR:Man City v Man United, EPL, 2200

30 APR:Man United v Swansea City, EPL, 1400

FIFA LISTI UBORA DUNIANI: BRAZIL KUSHIKA NAMBARI WANI, EGYPT JUU AFRIKA, TANZANIA KUPANDA JUU!

1441555 full-lndWAKATI Brazil ikitarajiwa kuwa Nambari Wani Duniani, Tanzania inategemewa kupanda juu kutoka Nafasi ya 157 iliyoshikilia Mwezi uliopita.

FIFA inatarajiwa kuitoa Listi ya Ubora Duniani Wiki ijayo Alhamisi Aprili 6 kuibadili ile ya Mwezi uliopita ambayo itaboreshwa kwa Matokeo ya Mechi za Kimataifa za hivi karibuni.
Listi hiyo mpya itairejesha Brazil kileleni kwa mara ya kwanza baada ya Miaka 6 na hilo limekuja baada ya mafanikio makubwa chini ya Kocha wao Tite ambae ameshinda Mechi 9 mfululizo tangu atwae wadhifa Mwaka Jana wakifunga Bao 25 na kufungwa 2 tu.
Ndani ya Wiki hii moja Brazil imeshinda Mechi zake zote 2 za Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini na kuwa Nchi ya Kwanza kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Ijumaa iliyopita Brazil iliifunga Uruguay 4-0 huko Montevideo na Juzi kuichapa 3-0 Paraguay huko Sao Paolo, Brazil.
Brazil wataitoa Argentina kwenye Namba 1 ya Listi ya Ubora baada ya Argentina kushinda Mechi 1, walipoifunga Chile 1-0, na kisha kuchapwa 2-0 na Bolivia.
Argentina sasa watashika Namba 2 baada kukaa kileleni kwa Miezi 12 walipowang'oa Mabingwa wa Dunia Germany ambao sasa watakuwa Nafasi ya 3.
Katika 10 Bora Nchi pekee mpya ni Switzerland ambayo sasa itakuwa wa 9 baada ya kuifunga Latvia 1-0 kwenye Mechi ya Kundi lao la Ulaya la kusaka kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018.
Nao Vigogo Netherlands, baada ya Wiki hii kuchapwa na Bulgaria na Italy, wamezidi kuporomoka kwa Nafasi 11 na kuangukia Nafasi ya 32 ikiwa ndio Nafasi ya chini kabisa katika Historia yao.
Wengine walioporomoka mno ni Uruguay walioshuka Nafasi 6 na kuangukia Nafasi ya 15 baada Wiki hii kuchapwa na Brazil na Peru.
Wakati Egypt ndiyo Timu ya juu kabisa kwa Afrika ikitarajiwa kushika Nafasi ya 19, Tanzania ambayo ipo Nafasi ya 157 inategemewa kupanda juu Nafasi kadhaa baada ya kuzifunga Botswana na Burundi Nchi ambazo ziko juu yake zinazoshika Nafasi za 116 na 139.
FIFA - LISTI YA UBORA - 20 ZA JUU:
6 Aprili 2017
1. Brazil
2. Argentina
3. Germany
4. Chile
5. Colombia
6. France
7. Belgium
8. Portugal
9. Switzerland
10. Spain
11. Poland
12. Italy
13. Wales
14. England
15. Uruguay
16. Mexico
17. Peru
18. Croatia
19. Egypt
20. Costa Rica

BLIND AFUKUZWA!

BLIND-BABA-MWANANETHERLANDS imemtimua Kocha wake Mkuu Danny Blind aliedumu kazini kwa Miaka Miwili.

Hatua hiyo inafuatia Netherlands kuchapwa 2-0 na Bulgaria Juzi Jumamosi na kuwaacha wakigalagala Nafasi ya 4 kwenye Kundi A la Nchi za Ulaya kusaka kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.

Baada ya Nusu ya Mechi zote za Kundi A, Netherlamds wapo Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 6 huku France wakuiongoza kwa kuwa na Pointi 13.WC-EURO-A

Blind, mwenye Miaka 55 na ambae Mwanawe ni Daley Blind anaechezea Manchester United na Netherlands, aliteuliwa Kocha kumrithi Guus Hidink Mwaka 2015.

Chama cha Soka cha Netherlands kimesema Matokeo yamewaacha mahala pabaya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia.

++++++++

JE WAJUA?

-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia

-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia

-Washindi wa Pili 8 Bora toka Makundi hayo 9 watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia

++++++++

Jumanne Netherlands itacheza Kirafiki na Italy na Timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Fred Frim.

Mara baada tamko hilo la FA ya Udachi, Daley Blind alimtumia ujumbe wa kumsapoti Baba yake Danny Blind.

DELE ALLI ‘JELA’ MECHI 3 ULAYA!

>>UEFA YAZIPIGA FAINI ARSENAL, BAYERN NA ST-ETIENNE!

DELE-ALLI-JINAKIUNGO wa Tottenham Dele Alli amefungiwa Mechi 3 za Ulaya baada ya kutolewa kwa Kadi Nyekundu Timu yake ilipocheza na KAA Gent ya Belgium Uwanjani Wembley Mwezi Februari kwenye Mechi ya UEFA EUROPA LIGI.

Alli alitolewa alipomvaa Mchezaji wa Gent Brecht Dejaegere kwenye Droo ya 2-2 na sasa UEFA imdethibitisha Adhabu yake.

Ikiwa Spurs watafuzu ndani ya 3 Bora ya EPL, Ligi Kuu England, basi Alli hatacheza Mechi 3 za Makundi ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Msimu ujao na hizo ni Nusu za Mechi za Awamu hiyo.

Wakati huo huo, Arsenal nayo imepigwa Faini ya Pauni 4,300 na UEFA kwa kosa la Mashabiki wao kuvamia Uwanja wa Kuchezea walipodundwa 5-1 na Bayern Munich Uwanjani Emirates.

UEFA pia imeipiga Faini Bayern Munich ya Pauni 2,600 baada ya Mashabiki wao kusababisha Mechi hiyo na Arsenal kuchelewa kuanza waliporusha Uwanjani Mabunda ya Karatasi za Chooni wakilalamikia Bei ya Juu ya Tiketi za Viingilio.

Timu nyingine iliyopigwa Faini na UEFA ni Saint-Etienne ya France ambayo itapaswa kulipa Pauni 43,000 baada ya Mashabiki wao kufyatua Fataki za Moto Uwanjani Old Trafford Mwezi uliopita walipofungwa na Manchester United kwenye Mechi ya UEFA EUROPA LIGI.

ARSENAL: SANCHEZ, OZIL KUBAKI, KUNG’OKA KUJULIKANA MWISHONI MWA MSIMU!

ARSENAL-SANCHEZ-OZILArsenal imesimamisha mazungumzo yao ya kuongeza Mikataba na Wachezaji wao Alexis Sanchez na Mesut Ozil hadi mwishoni mwa Msimu huu kwa mujibu wa Meneja Arsene Wenger.

Wachezaji hao wamabakisha Miezi 15 tu ya Mikataba yao ya sasa na Arsenal na wote wamehusishwa na kuhama.

Wakati Sanchez akiwa kimya kuhusu hatima yake, Ozil alikaririwa Mwezi Januari kuwa kubaki kwake Arsenal kunategemea kama Wenger atabakia Arsenal.

Nae Wenger Mkataba wake na Arsenal unakwisha mwishoni mwa Msimu huu na hadi sasa hamna uhakika kama atabaki au la ingawa zipo habari thabiti Arsenal ishamwekea Mezani Mkataba mpya wa Miaka Miwili.

Msimu huu, Sanchez ameifungia Arsenal Bao 22 na Ozil kupiga 9.

Juzi Wenger alitoboa ameshafikia uamuzi wake kuhusu hatima yake hapo Arsenal na kutamka atautangaza hivi karibuni.

Akiongea na beIN Sports, Wenger amesema: “Kwa sasa hatujafikia makubaliano na Wachezaji hao Wawili. Tumeamua kutilia mkazo tunamaliza vipi Msimu huu na kuzungumza kuhusu wao mwishoni mwa Msimu.”

Huko nyuma, Wenger aliwahi kusema yuko tayari kuwabakisha Arsenal Ozil na Sanchez hadi 2018 watakapomaliza Mikataba yao na kuondoka bure bila Senti kulipwa kuliko kuwauza mwishoni mwa Msimu huu.