YAYA TOURE ASAINI MKATABA MPYA MANCHESTER CITY

KIUNGO wa Manchester City Yaya Toure amesaini Mkataba Mpya wa Mwaka Mmoja.

Toure, mwenye Miaka 34, ameichezea Man City Mechi 299 na kufunga Bao 81 tangu ajiunge nao Mwaka 2010 akitokea Barcelona.

CITY-PEP-YAYAMapema mwanzoni mwa Msimu huu uliokwisha Mwezi uliopita Toure alitemwa toka Kikosi cha City kilichosajiliwa kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya Meneja Pep Guardiola kukwaruzana na Wakala wa Toure, Dimitri Seluk.

Hilo pia lilimfanya Toure asipewe namba kwenye Mechi nyingine hadi pale Toure alipomwomba msamaha Guardiola mwanzoni mwa Novemba na Staa huyo toka Ivory Coast kupangwa Mechi na Crystal Palace baadae Mwezi huo na akafunga Bao 2 kwenye mechi hiyo.

Kuanzia hapo Toure akarudi Kikosini kwa kudumu na kucheza Mechi 31 akiisaidia City kumaliza Nafasi ya 3 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND.

Akiongea baada ya kusaini Mkataba huu Mpya, Toure ameeleza: “Nina bahati kuwa sehemu yah ii Klabu kubwa yenye Wachezaji wakubwa ambao wananisaidia kutimiza malengo!”

Nae Mkurugenzi wa Soka wa City Txiki Begiristain amsema: "Yaya amekuwa Mtumishi mwema kwa Manchester City na ni sehemu muhimu kwa Kikosi cha Pep Guardiola.”

Mkataba wa Toure ulikuwa umalizike Mwezi huu Juni na huu Mpya unambakiza hadi Mwakani.

Hivi karibuni City imewaacha Kipa Willy Caballero, Jesus Navas, Pablo Zabaleta, Gael Clichy na Bacary Sagna wote wakiwa wamemaliza Mikataba yao.

Tayari Wiki hii City imenunua Wachezaji Wawili Wapya ambao ni Kiungo kutoka AS Monaco Bernardo Silva waliemnunua kwa Pauni Milioni 43 na Kipa kutoka Benfica Ederson Moraes alielipiwa Pauni Milioni 35.

SILVA KUTUA CITY, VALENCIA AONGEZA MAN UNITED, ZABALETA ATUA WEST HAM!

EPL, LIGI KUU ENGLAND, imemaliza Msimu wake wa 2016/17 na sasa Klabu zake zinajijenga kwa Msimu Mpya wa 2017/18 unaoanza Agosti 12 na tayari Klabu kadhaa zashaanza kuanika mapya yao.

FUATILIA YALIYOJIRI LEO:

SILVA KUTUA CITY

BERNARDO-SILVABernardo Silva Kiungo wa AS Monaco anaetoka Portugal, yuko mbioni kukamilisha Dili ya kutua Manchester City inayosemekana itagharimu Pauni Milioni 43.

Msimu huu, Silva, mwenye Miaka 22, aliisaidia sana Monaco kutwaa Ubingwa wa Ligi 1 huko France na pia kuifikisha Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Silva ameichezea Timu ya Taifa ya Portugal mara 12 na kufunga Bao 1 na kukipiga Mechi 58 na Monaco akifunga Bao 11.

VALENCIA

Mchezaji wa Manchester United Antonio Valencia amesaini nyongeza ya Miaka Miwili kwenye Mkataba wake ambao pia una Kipengele cha kubaki Mwaka Mmoja zaidi ya 2019.

Valencia, mwenye Miaka 31 na ni Mchezaji wa Kimataifa kutoka Ecuador, ameichezea Man United Mechi 43 Msimu huu nan die alikuwa Kepteni Juzi Jumatano wakati Man United MANUNITED-VALENCIAinaichapa Ajax 2-0 kwenye Fainali na kubeba UEFA EUROPA LIGI huko Stockholm, Sweden.

Valencia alijiunga na Man United Mwaka 2009 akitokea Wigan.

ZABALETA

West Ham wapo njiani kumsaini Beki Pablo Zabaleta kama Mchezaji Huru kutoka Manchester City mara tu baada ya Mchezaji huyo kutoka Argentina kumalizika Julai 1.

Zabaleta aliagwa rasmi na Man City Mei 17 baada ya kuitumikia Klabu hiyo kwa Miaka 9 akiwa Mchezaji wa 3 kudumu kwa Miaka mingi akiwafuata Joe Hart na Vincent Kompany.

Zabaleta, mwenye Miaka 32, alijiunga na City kutoka Espanyol ya Spain Mwaka 2008 kwa Dau la Pauni Milioni 6.5 na kuichezea Klabu hiyo Mechi 333 akitwaa Ubingwa wa England mara 2, Kombe la Ligi mara 2 na FA CUP.

BIG SAM ANG'ATUKA PALACE!

BIG-SAMSam Allardyce, maarufu kama Big Sam, amejiuzulu kama Meneja wa Crystal Palace mara baada ya kuinusuru kushuka Daraja ikiwa ni Miezi Mitano tu tangu ajiunge nao.
Allardyce alijiunga na Palace Mwezi Desemba kumrithi Alan Pardew na kupewa Mkataba wa Miaka Miwili na Nusu.
Wakati huo Palace walikuwa nafasi za mkiani kwenye Msimamo wa EPL, LIGI KUU ENGLAND wakiwa Pointi 1 tu juu ya zile Timu 3 za mwisho ambazo hushushwa Daraja.
Lakini Big Sam, ambae kabla alikuwa Meneja wa Timu ya Taifa ya England kwa Gemu 1 tu na kulazimika kujiuzulu kutokana na kashfa, aliweza kuiongoza Palace ishinde Gemu 8 kati ya 21 na kujikita Nafasi ya 14 katika EPL yenye Timu 20 na hivyo kuinusuru kushushwa Daraja.
Hilo lilimfanya Big Sam, ambae ashawahi kuwa Meneja kwenye Klabu za Bolton, Blackburn, Newcastle na West Ham, kudumisha Rekodi yake safi ya kutowahi kushushwa Daraja akiwa na Klabu yeyote.
Akiongea mara baada ya uamuzi huu wa kuondoka Palace ukitangazwa, Big Sam alisema: "Sina haja kushika kazi nyingine. Nataka nifurahie maisha!"
Huyu anakuwa Meneja wa pili Wiki hii kuondoka Klabuni kwa hiari yake baada Juzi David Moyes kuamua kuondoka Sunderland ambayo imeshushwa Daraja kutoka EPL.
 
 
 
 
 

‘MALAIKA MPYA’ MAN UNITED: MPWA WA WINGA NANI, ANGEL GOMES, MIAKA 16, AZUA GUMZO ULAYA!

MANUNITED-ANGELGOMESJOSE MOURINHO alishatoboa kuwa kwenye Mechi yao ya mwisho kabisa ya EPL, LIGI KUU ENGLAND, hapo jumapili dhidi ya Crystal Palace ambayo haina maana yeyote kwao atachezesha Kikosi mchanganyiko chenye Chipukizi kadhaa na mmoja kati ya hao ni Angel Gomes ambae Juzi alizoa Tuzo ya Klabu ya Manchester United ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Vijana.

Uamuzi huo wa Mourinho wa uteuzi wa Kikosi cha Mechi hiyo ya EPL ambayo matokeo yake yeyote hayatabadili Nafasi yao ya 6 hasa unalenga kulinda Mastaa wao kwa ajili Fainali ya Jumatano ya huko Stockholm, Sweden ya UEFA EUROPA LIGI ambayo watapambana na Ajax Amsterdam ya Netherlands.

Miongoni mwa Chipukizi ambao wametajwa Kikosini:

MAKIPA: Kieran O'Hara (Miaka 21), Joel Castro Pereira (20).

BEKI: Demetri Mitchell (20).

VIUNGO: Zachary Dearnley (19), Angel Gomes (16), Josh Harrop (21), Scott McTominay (20), Matthew Willock (20).

Kati ya wote hao, huko Uingereza, Angel Gomes, Kijana wa Miaka 16, Mpwa wa Winga wa zamani wa Man United Nani, ndie amezua gumzo kubwa hasa baada ya Juzi kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Vijana.

++++++++++++++++

WASIFU:

Jina: Angel Gomes

Umri: 16

Kuzaliwa: London

Pozisheni: Attacking midfielder

Klabu: Manchester United

Kimataifa: England U-16 na U-17

++++++++++++++++

Kwa kuzoa Tuzo ya Man United ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Vijana, ambayo inaitwa Jimmy Murphy Youth Team Player of the Year, Angel Gomes ameweka Historia ya kuwa Kijana mwenye Umri mdogo kabisa kuibeba.

Miongoni mwa Wachezaji maarufu waliowahi kuchukua Tuzo hii ni pamoja na Paul Scholes na Ryan Giggs.

++++++++++++++++

Washindi wenye Umri Mdogo kutwaa Tuzo ya Man United ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Vijana:

Angel Gomes – Miaka 16 Miezi 9 - 2017

Mats Daehli – Miaka 17 Miezi 2 -2012

Will Keane – Miaka 17 Miezi 4 - 2010

Phil Neville – Miaka 17 Miezi 4 - 1994

Axel Tuanzebe - Miaka 17 Miezi 6 - 2015

Ryan Giggs – Miaka 17 Miezi 6 - 1991

Danny Welbeck – Miaka 17 Miezi 6 - 2008

Federico Macheda - Miaka 17 Miezi 9 - 2009

++++++++++++++++

Gomes hucheza kama Kiungo Mshambuliaji na Msimu huu amepiga Bao 12 katika Mechi 19 alizoanza.

Gomes pia huzichezea Timu za Taifa za Vijana za U-16 na U-17.

Kijana huyu alizaliwa Jijini London na Baba yake pia aliwahi kuwa Mchezaji ambae alitwaa Ubingwa wa Ulaya wa U-17 akiichezea FC Porto ya Ureno Mwaka 1989 na kisha kuhamia Klabu kadhaa Duniani ikiwemo Salford City ya huko Jijini Manchester.

Gomes alisainiwa na Man United akiwa na Miaka 13 na uwezo na kipaji chake kilimfanya amudu kuchezea Kikosi cha U-18 akiwa na Miaka 14 tu.

Mwaka 2015, Gomes alishinda Tuzo ya Mchezaji wa Thamani kwenye Premier Cup ambako huko England hushindaniwa na Vikosi vya Chipukizi vya Klabu kubwa.

Nicky Butt, Kiungo wa zamani wa Man United ambae sasa ndie anasimamia Kikosi cha Vijana cha Man United, ameeleza: “Angel Gomes ni Kijana mwenye Kipaji kikubwa mno na tuna matumaini makubwa mno kwake!”

TOTAL U-17 AFCON GABON 2017: MABINGWA MALI WAFUNGANA NA SERENGETI BOYS KILELENI KUNDI B!

TOTAL AFCON U17 GABON2017>NUSU FAINALI, FAINALI KOMBE LA DUNIA HIZOOO!

MARA baada ya Serengeti Boys kuichapa Angola 2-1 hapo Jana huko Stade de L’Amitle, Mjini Libreville Nchini Gabon, kwenye Mechi ya Kundi B la Mashindano ya TOTAL U-17 AFCON GABON 2017, ikafuatia Mechi nyingine ya Kundi hilo na Mabingwa Watetezi Mali kuipiga Niger 2-1.

Awali Jana Tanzania, maarufu kama Serengeti Boys, iliibwaga Angola 2-1 ikiwa ni Mechi yao ya Pili ya Kundi B baada kuanza kwa Sare ya 0-0 na Maabingwa Watetezi Mali.

Matokeo ya Mechi 2 za kwanza za Kundi B zimeziweka Serengeti Boys na Mali juu kileleni zote zikiwa na Pointi 4 kila moja zikifuatia Niger na Angola zenye Pointi 1 kila moja.

Hii inamaanisha, ili kutinga Nusu Fainali ya Mashindano na hivyo pia kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za U-17 huko India Mwezi Oktoba, Serengeti Boys wanahitaji Sare tu kwenye Mechi yao ya mwisho na Niger.

++++++++++++++++++++++

**FAHAMU:

-Washindi Wawili wa kila Kundi watatinga Nusu Fainali na Timu hizo 4 zitakazocheza Nusu Fainali ndizo hizo hizo zitafuzu kucheza Fainali za FIFA za Kombe la Dunia kwa Vijana U-17 huko Nchini India Mwezi Oktoba.

++++++++++++++++++++++

Toka Kundi A, Timu hatari ya Ghana tayari ishatinga Nusu Fainali, na hivyo pia kwenda India, huku ikiwa na Mechi 1 mkononi.

Serengeti Boys watamaliza Mechi zao za Kundi B hapo Jumapili Mei 21 kwa kucheza na Niger huko Stade de POG, Port Gentil.

TOTAL U-17 AFCON GABON 2017

MSIMAMO:

AFCON-U17-TEBO-2MATCHES

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

***KUNDI A Mechi kuchezwa Mjini Port Gentil KUNDI B Mjini Libreville

MAKUNDI:

Jumapili Mei 14

KUNDI A

Gabon 1 Guinea 5

Cameroun 0 Ghana 4

Jumatatu Mei 15

KUNDI B

Mali 0 Tanzania 0

Angola 2 Niger 2

Jumatano Mei 17

KUNDI A

Guinea 1 Cameroun 1

Ghana 5 Gabon 0

Alhamisi Mei 18

KUNDI B

Tanzania 2 Angola 1

Niger 1 Mali 2

MECHI ZA MWISHO ZA MAKUNDI

Jumamosi Mei 20

KUNDI A

2030 Gabon v Cameroun [Stade de POG, Port Gentil]

2030 Guinea v Ghana [Stade de L’Amitle, Libreville]

Jumapili Mei 21

KUNDI B

2030 Mali v Angola [Stade de L’Amitle, Libreville]

2030 Tanzania v Niger [Stade de POG, Port Gentil]

NUSU FAINALI:

Jumatano Mei 24

Stade de POG, Port Gentil

1730 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B

Stade de L’Amitle, Libreville

2030 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A

Jumapili Mei 28

Stade de L’Amitle, Libreville

1730 KUGOMBEA MSHINDI WA 3

2030 FAINALI