WENGER AWAPONDA MAMENEJA VIJANA, AJIBATIZA YEYE 'PADRI WA SOKA'!

WENGER-ATAFAKARIArsene Wenger amewaponda Mameneja Vijana kwa kukosa uvumilivu na kujiita yeye "Padri wa Soka' mara tu baada ya Luis Enrique kutangaza yeye atang'atuka Barcelona mwishoni mwa Msimu huu.
Kauli ya Enrique imeleta fikra kuwa huenda Wenger nae akatimkia huko Spain kujiunga na Barcelona mwishoni mwa Msimu kwa vile Mkataba wake na Arsenal unakwisha wakati huo.
Enrique amedai amechoka baada ya Miaka Mitatu tu akiwa na Barca akifuata nyayo za Pep Guardiola ambae nae aling'atuka kwa staili hiyo.
Wenger, mwenye Miaka 67, anahisi Rika la sasa la Mameneja Vijana linakosa uvumilivu na moyo wa kujituma na kutumikia kwa Miaka mingi kama yeye alivyofanya akidumu Arsenal kwa Miaka 20.
Wenger amenena: "Mie ni spesho kwa ukatili. Ukiwa Meneja unapata Kero Asilimia 90 na furaha na kuridhika kwa hali ya juu kwa Asilimia 10 tu!"
"Siku zote nawaambia hawa Vijana wanaotaka kazi hii: 'Uko tayari kujitoa muhanga, kuyadhuluma maisha yako?' Ni sawa kuwa kama Padre, wewe ni Padri wa Soka!"
Kuhusu yeye kwenda Barca kama anavyotuhumiwa Wenger amekataa katakata kuzungumzia hilo mbali ya kudai bado hajaamua kama atasaini Mkataba wa kubakia na Arsenal au la.

LUIS ENRIQUE KUNG'OKA BARCELONA!

LUIS-ENRIQUEBOSI wa Barcelona Luis Enrique ataachia ngazi mwishoni mwa Msimu huu akidai anahitaji mapumziko.
Enrique, mwenye Miaka 46, yupo kwenye Msimu wake wa 3 na Barca.
Kocha huyo alitangaza uamuzi wake huo hapo Jana mara tu baada ya Barca kuitwanga Sporting Gijon 6-1 na kutwaa uongozi wa La Liga wakiwa Pointi 1 mbele ya Real waliocheza Mechi 1 pungufu.
Akiwa na Barca, alitwaa Ubingwa wa UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI kwenye Msimu wake wa kwanza tu ikiwa ni moja ya Mataji Matatu aliyotwaa Msimu huo na Msimu uliopita kutwaa Ubingwa wa La Liga na Copa del Rey.
Lakini Msimu huu wako Mguu mmoja nje ya UCL baada kuchapwa 4-0 na Paris St-Germain huko Paris, France katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 wakiombea miujiza ili kupindua kipigo hicho katika Mechi ya Marudiano itakayochezwa Nou Camp hapo Machi 8.
Enrique alikuwa Mchezaji wa Kimataifa wa Spain ambae alikuwa Real Madrid kati ya 1991 na 1996 na pia aliichezea Barca kati ya 1996 na 2004 alipostaafu Soka.
Kati ya 2008 na 2011 alikuwa Kocha wa Barcelona B na kisha kwenda kuzifundisha Klabu za AS Roma huko Italy na Celta Vigo ya Spain na 2014 kurejea Barca kuchukua nafasi ya Gerardo Martino kama Kocha Mkuu.
Show more

KEPTENI ROONEY ATOA TAMKO, AIKANA UCHINA!

MANUNITED-ROONEY-TUZOKEPTENI wa Manchester United Wayne Rooney ametoa Taarifa rasmi kukanusha kuwa yuko mbioni kuhamia China kabla Dirisha la Uhamisho la Nchi hiyo halijafungwa Jumanne ijayo Februari 28.

Habari za kuhama kwa Rooney zilishika hatamu mara baada ya kuripotiwa kuwa Wakala wake, Paul Stretford, yuko huko China kukamilisha Dili ya Uhamisho.

Leo hii, Rooney, mwenye Miaka 31 na ambae Mkataba wake na Man United unamalizika 2019, amesisitiza yupo na atabaki Man United kwenye Vita yao ya Mstari wa Mbele kwenye Mashindano Manne.

Jumapili Man United wako huko Wembley Jijini London kucheza Fainali ya Kombe la Ligi, EFL CUP, na Southampton, na pia wamefuzu kutinga Robo Fainali ya FA CUP huku pia Jana wakifanikiwa kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI wakati pia kwenye EPL, Ligi Kuu England, bado wamo mno kwenye kinyang’anyiro cha kutinga 4 Bora.

TAMKO LA ROONEY:

“Ingawa Klabu kadhaa zimeonyesha nia, ambapo nashkuru, mie nataka kumaliza haya na kusema nabakia Manchester United. Natumaini nitashiriki kikamilifu kuisaidia Timu kufanikiwa katika vita yake ya pande 4! Ni wakati wa kufurahisha kwa Klabu na nataka niwe moja ya sehemu yake!”

Nyuma ya Pazia

Hivi sasa Rooney hana namba kwenye Kikosi cha Kwanza cha Man United na hajacheza tangu Februari 1 akidaiwa kuwa na maumivu ya Musuli.

Wiki hii Rooney alirejea Mazoezini lakini hakujumuika kwenye Kikosi kilichoenda France ambacho Jana kiliifunga Saint-Etienne 1-0 na kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI.

Jumapili Man United wapo huko Wembley Jijini London kucheza Fainali ya Kombe la Ligi, EFL CUP, dhidi ya Southampton na hadi sasa hamna uhakika kama Rooney atakuwemo miongoni ma Wachezaji kwa ajili ya Mechi hiyo.

Inaaminika kuwa chaguo la Rooney ni kubakia Man United hadi 2019 ambapo Mkataba wake utamalizika ili apate fursa kuichezea Timu ya Taifa ya England Mechi 7 zaidi ili aweke Rekodi ya kuwa ndie Mchezaji alieichezea Nchi hiyo Mechi nyingi zaidi katika Historia yake.

Akiwa na Man United, Rooney ametwaa Ubingwa wa England mara 5 na UEFA CHAMPIONZ LIGI mara 1 tangu ajiunge nao Mwaka 2004 akiwa na Miaka 18 kutoka Everton kwa Dau la Pauni Milioni 27.

ROONEY: UCHINA KWANUKIA!

FA-CUP-16-17-ROONEY-KOMBEDIRISHA LA UHAMISHO huko China linafungwa Jumanne Februari 28 na Wakala wa Kepteni wa Manchester United Wayne Rooney ametua huko.
Paul Stretford yuko huko China kukamilisha dili ya Rooney kuhamia huko ingawa hamna uhakika dili hii itatimia kwa kuhama hivi sasa.
Kuwepo kwa Stretford huko China kuzungumzia dili ya Uhamisho wa Rooney kumetafsiriwa na Wachambuzi huko England kuwa Meneja wa Man United Jose Mourinho ataruhusu Rooney, mwenye Miaka 31, kuondoka Klabuni hapo.
Hivi sasa Rooney hana namba kwenye Kikosi cha Kwanza cha Man United na hajacheza tangu Februari 1 akidaiwa kuwa na maumivu ya Musuli.
Wiki hii Rooney alirejea Mazoezini lakini hakujumuika kwenye Kikosi kilichoenda France ambacho Jana kiliifunga Saint-Etienne 1-0 na kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI.
Jumapili Man United wapo huko Wembley Jijini London kucheza Fainali ya Kombe la Ligi, EFL CUP,  dhidi ya Southampton na hadi sasa hamna uhakika kama Rooney atakuwemo miongoni ma Wachezaji kwa ajili ya Mechi hiyo.
Inaaminika kuwa chaguo la Rooney ni kubakia Man United hadi 2019 ambapo Mkataba wake utamalizika ili apate fursa kuichezea Timu ya Taifa ya England Mechi 7 zaidi ili aweke Rekodi ya kuwa ndie Mchezaji alieichezea Nchi hiyo Mechi nyingi zaidi katika Historia yake.

Akiwa na Man United, Rooney ametwaa Ubingwa wa England mara 5 na UEFA CHAMPIONZ LIGI mara 1 tangu ajiunge nao Mwaka 2004 akiwa na Miaka 18 kutoka Everton kwa Dau la Pauni Milioni 27.

EMIRATES FA CUP: MABINGWA MAN UNITED NA CHELSEA MACHI 11, STAMFORD BRIDGE!

EMIRATES-FACUP-2017-SITMECHI za Raundi ya 6 ya EMIRATES FA CUP, ambayo ndiyo Robo Fainali, zitachezwa Machi 11 na moja ya mvuto mkubwa ni Mabingwa Watetezi Manchester United kutua Stamford Bridge kupambana na Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea.

Hiyo ndio Bigi Mechi pekee kwenye Raundi hiyo wakati Mechi nyingine zikipambanisha ‘Timu kubwa’ na upinzani hafifu.

Lakini, ikiwa Man City wataitoa Huddersfield katika Mechi yao ya Marudiano ya Raundi ya 5 kufuatia Sare ya 0-0 basi watakuwa Wageni wa Middlesbrough na hii itakuwa ni Mechi ya Pili kukutanisha Timu za EPL, Ligi Kuu England, baada ya ile kati ya Chelsea na Man United.

+++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.

-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.

-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.

-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.

-Bingwa Mtetezi ni Manchester United.

+++++++++++++++++++

Arsenal wao watakuwa Nyumbani Emirates kucheza na Lincoln City, Timu ambayo haipo Mfumo rasmi wa Ligi huko England, ambayo ilijizolea sifa kubwa kwa kuibwaga Burnley wanaocheza EPL na waliokuwa Nyumbani kwao.

FA CUP

Ratiba

Jumatano Machi 1

Raundi ya 5 - Marudiano

2245 Manchester City v Huddersfield Town [Mechi ya Kwanza 0-0] 

Jumamosi Machi 11

Raundi ya 6 [Robo Fainali]

**Mechi zote kuanza Saa 12 Jioni

Arsenal v Lincoln City       

Chelsea v Manchester United                

Middlesbrough v Huddersfield/Man City           

Tottenham Hotspur v Millwall

**Ratiba inaweza kubadilika kwa matakwa ya Warushaji Matangazo mubashara wa TV.                            

TAREHE MUHIMU:

HATUA

RAUNDI

DROO

MECHI

Raundi za Awali

Raundi ya Awali kabisa

8 Julai 2016

6 Agosti 2016

Raundi ya Awali

20 Agosti 2016

Raundi ya 1 Mchujo

15 Agosti 2016

3 Septemba 2016

Raundi ya 2 Mchujo

5 Septemba 2016

17 Septemba 2016

Raundi ya 3 Mchujo

19 Septemba 2016

1 Oktoba 2016

Raundi ya 4 Mchujo

3 Oktoba 2016

15 Oktoba 2016

Mashindano rasmi

Raundi ya 1

17 Oktoba 2016

5 Novemba 2016

Raundi ya 2

7 Novemba 2016

3 Desemba 2016

Raundi ya 3

5 Desemba 2016

7 Januari 2017

Raundi ya 4

Kujulishwa

28 Januari 2017

Raundi ya 5

Kujulishwa

18 Februari 2017

Raundi ya 6 [Robo Fainali]

Kujulishwa

11 Machi 2017

Nusu Fainali

Kujulishwa

22 na 23 Aprili 2017

FAINALI

27 Mei 2017