FIFA KOMBE LA MABARA RUSSIA 2017: LEO NI MABINGWA WA DUNIA GERMANY v AUSTRALIA

FIFA CONFED2017 SITMARA ya mwisho kwa Germany na Australia kukutana ilikuwa kwenye Mashindano kama haya na Germany kushinda 4-3.

Kabla ya Mechi hiyo, Timu hizi zimekutana mara 5 na Germany kushinda 3 za mwanzo kufungwa iliyofuatia na ikaja Sare.

Lakini Australia ya sasa ni kigaga na imepoteza Mechi 1 tu katika 19 iliyocheza mwisho na hiyo ni ile ya Wiki iliyopita ilipopigwa 4-0 na Brazil huko Melbourne.

Kwa Germany, Kikosi kilicholetwa Russia kwa ajili ya Mashindano haya hakina Wazoefu wengi na kina Wachezaji Watatu tu waliyoipa Ubingwa wa Dunia huko Brazil Mwaka 2014.

Watatu hao ni Shkodran Mustafi, Matthias Ginter na Julian Draxler huku wengine wote ama ni Wastaafu, Majeruhi au wamepumzishwa.

Lakini Rekodi ya Germany ni ya kutisha kwani wameshinda Mechi 8 na sare 2 katika Mechi zao 10 zilizopita wakifunga Bao 31 na kufungwa 2 tu.

Hii ni mara ya 4 kwa Australia kucheza Kombe la Mabara baada kushiriki Mashindano yale ya Miaka ya 1997, 2001 na 2005.

Pia Kikosi chao kina Wachezaji wenye uzoefu wa Germany kwa vile wanacheza kwenye Bundesliga na hao ni Mitch Langerak na Mathew Leckie na Mchezaji aliesainiwa hivi karibuni na Klabu ya Darmstadt, Jamie MacLaren, wakati yupo pia aliewahi kuichezea Bayer Leverkusen kama Fowadi Robbie Kruse.

Wachambuzi wana usongo kuona Australia ngumu itafanyaje dhidi ya Germany Chipukizi.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

Australia: Mat Ryan; Bailey Wright, Milos Degenek, Trent Sainsbury; Mark Milligan, Aaron Mooy, Aziz Behich, Jackson Irvine, Tom Rogic, Mathew Leckie; Tomi Juric

Germany: Bernd Leno; Joshua Kimmich, Matthias Ginter, Antonio Rudiger, Jonas Hector; Emre Can, Julian Brandt, Leon Goretzka, Lars Stindl, Julian Draxler; Sandro Wagner

REFA: Mark Geiger (USA)

++++++++++++++++

FIFA KOMBE LA MABARA

Ratiba/Matokeo:

Hatua ya Kwanza

Jumamosi Juni 17

KUNDI A

Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg

Russia 2 New Zealand 0

Jumapili Juni 18

KUNDI A

Kazan Arena, Kazan

Portugal 2 Mexico 2

KUNDI B

Spartak Stadium, Moscow

Cameroon 0 Chile 2 

Jumatatu Juni 19

KUNDI B

Fisht Stadium, Sochi

1800 Australia v Germany

Jumatano Juni 21

KUNDI A

Spartak Stadium, Moscow

1800 Russia v Portugal

Fisht Stadium, Sochi

2100 Mexico v New Zealand

Alhamisi Juni 22

KUNDI B

Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg

1800 Cameroon v Australia

Kazan Arena, Kazan

2100 Germany v Chile

Jumamosi Juni 24

KUNDI A

Kazan Arena, Kazan

1800 Mexico v Russia

Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg

1800 New Zealand v Portugal

Jumapili Juni 25

KUNDI B

Fisht Stadium, Sochi

1800 Germany v Cameroon

Spartak Stadium, Moscow

1800 Chile v Australia

Hatua ya Pili

Nusu Fainali

Jumatano Juni 28

Kazan Arena, Kazan

2100 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [NF1]

Alhamisi Juni 29

Fisht Stadium, Sochi

2100 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [NF2]

Mshindi wa 3

Jumapili Julai 2

Spartak Stadium, Moscow

1500 Atakaefungwa NF1 v Atakaefungwa NF2

FAINALI

Jumapili Julai 2

Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg

2100 Mshindi NF1 v Mshindi NF2

Habari MotoMotoZ