WEST HAM KUSHINDWA KUCHEZA MECHI YA KWANZA MSIMU MPYA WA LIGI 2017/18 UWANJANI KWAO!

West Ham hawataweza kucheza Mechi yao ya kwanza ya Msimu Mpya wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, kwenye Uwanja wao wa Nyumbani London Stadium.

LONDON-STADIUMKlabu hiyo inaanza Msimu Mpya Agosti 12 kwa kucheza Ugenini huko Old Trafford na Manchester United na Mechi ya Pili ilitakiwa ichezwe Agosti 19 Nyumbani kwao London Stadium na Southampton lakini Uwanja huo hautakuwa tayari baada ya kutumika kwa Mashindano ya Riadha ya Dunia.

Mashindano hayo ya Riadha yanaisha Jumapili Agosti 13 na ili kuuweka tayari Uwanja West Ham wamethibitisha Mechi yao ya kwanza ya EPL humo London Stadium itakuwa Septemba 9 dhidi ya Huddersfield Town.

Tatizo kubwa ni kuwa Uwanjani humo Viti vyote vya Safu za mbele vitang’olewa ili kutoa nafasi kwa ile sehemu maalum ya kukimbilia Wanaradha na kuhifadhiwa sehemu nyingine kabisa nje ya Uwanja huo.

Kazi ya kuving’oa Viti vyote itachukua Siku 15 na inakadiriwa zinahitajika pia Siku 15 kuvirudisha vile vile kama mwanzo.

West Ham sasa wapo kwenye mchakato wa kuomba Mechi yao Agosti 19 na Southampton ichezwe Ugenini huko St Mary’s na ile waliyopangiwa kucheza huko St Mary’s hapo 31 Machi 2018 ichezwe London Stadium.

Ikiwa hilo litaafikiwa, basi West Ham watacheza Mechi zao 3 za kwanza za Msimu Mpya wa EPL zote Ugenini.

Msimu uliopita Liverpool walikutana na hali kama hiyo ya kucheza Mechi zao zote za mwanzo Ugenini kutokana na Ujenzi Uwanjani kwao Anfield.

West Ham United - Ratiba yao Mechi za Mwanzoni:

12 Agosti – Manchester United (U)

19 Agosti – Southampton (N)

26 Agosti – Newcastle United (U)

9 Septemba – Huddersfield Town (N)

16 Septemba – West Bromwich Albion (U)

23 Septemba – Tottenham Hotspur (N)

30 Septemba – Swansea City (N)

**U-Ugenini N=Nyumbani

Habari MotoMotoZ