KIPONDO 5 CHA BAYERN: WENGER AUNGAMA 'WALISAMBARATIKA KIAKILI', MASHABIKI WATAKA ATOKOMEE!

WENGER-ATAFAKARIBaada ya Jana kubondwa 5-1 huko Allianz Arena, Munich, Germany toka kwa Bayern Munich katika Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekiri Timu yake 'ilisambaratika kiakili'.
Hadi Mapumziko Bayern na Arsenal zilikuwa 1-1 lakini Kipindi cha Pili, baada ya Sentahafu wao Laurent Koscielny kuumia na kutoka, Bayern ikabamiza Bao 4 na kushinda 5-1 ikijiweka nafasi nzuri kutinga Robo Fainali labda Arsenal ishinde 4-0 katika Marudiano huko Emirates hapo Machi 7.
Ikiwa Arsenal watatupwa nje, hii itakuwa ni ni mara ya 7 mfululizo kushindwa kuvuka Hatua hii ya Mtoano ya UCL.
Mara baada ya kipigo hicho, Wenger akiongea na TV alisema: "Ni ngumu kueleza. Kabla ya Mapumziko tulikosa nafasi 2 nzuri za kufunga. Tukarudi na kucheza vizuri lakini tukampoteza Koscielny gemu ikiwa 1-1 na kisha tukasambaratika! Lakini Bayern ni Timu nzuri kupita sisi!"
Mara baada ya Mechi hiyo Wachambuzi wa Soka huko England na Mashabiki wa Arsenal kila kona ya Dunia wakakiri sasa ni muda muafaka kwa Wenger kuondoka huko Emirates.