CONTE: 'SIPENDI MZAHA WA MOURINHO!"

5766136721Antonio Conte amesema hapendi 'mzaha'wa Jose Mourinho baada ya Meneja huyo wa Manchester United kudai Chelsea ambao ni Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, hawawezi kukamatika kileleni kwa sababu ni Timu 'inayojihami mno!'.
Hivi sasa Chelsea wapo Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Tottenham baada Jana kutoka 1-1 na Burnley huko Turf Moor.
Mourinho, ambae anasifika kwa kuchota akili za Mameneja wapinzani na kuwavuruga, Juzi alidai Chelsea haiwezi kuteleza kutoka kileleni kwa vile 'wanajihami mno' na kushinda kwa kutumia 'kaunta ataki'.
Jana Meneja wa Chelsea Antonio Conte alijibu mapigo kwa kusema: "Hiyo ni hadaa yake. Nina uzoefu kuelewa hilo!"
Mara nyingi Mourinho amekuwa akikwaruzana na Mameneja wenzake kutokana na vijembe vyake vya kuwapandisha munkari ili kushinda vita ya kisaikolojia na muhanga mkuu wa mashambulizi hayo huko nyuma akiwa Arsene Wenger wa Arsenal.
Hata hivyo Conte amegoma kuburutwa kwenye vita hiyo na kujibu: "Sipendi kujibu kuhusu Makocha wengine!"
EPL – Ligi Kuu England
Ratiba
Jumatatu Februari 13
2300 Bournemouth v Manchester City   
Jumamosi Februari 25
1800 Chelsea v Swansea City               
1800 Crystal Palace v Middlesbrough              
1800 Everton v Sunderland         
1800 Hull City v Burnley             
Southampton v Arsenal [IMEAHIRISHWA]
1800 West Bromwich Albion v Bournemouth              
2030 Watford v West Ham United         
Jumapili Februari 26
1630 Tottenham Hotspur v Stoke City             
Manchester City v Manchester United[IMEAHIRISHWA]
Jumatatu Februari 27
2300 Leicester City v Liverpool             
Jumamosi Machi 4
1530 Manchester United v Bournemouth         
1800 Leicester City v Hull City              
1800 Stoke City v Middlesbrough          
1800 Swansea City v Burnley                
1800 Watford v Southampton               
1800 West Bromwich Albion v Crystal Palace             
2030 Liverpool v Arsenal            
Jumapili Machi 5
1630 Tottenham Hotspur v Everton       
1900 Sunderland v Manchester City      
Jumatatu Machi 6
2300 West Ham United v Chelsea