LEO ANFIELD: LIVERPOOL v TOTTENHAM, NANI MBABE?

>PATA RIPOTI/VIKOSI!

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

LIVER-SPURSJumamosi Februari 11

1530 Arsenal v Hull City             

1800 Manchester United v Watford                 

1800 Middlesbrough v Everton    

1800 Stoke City v Crystal Palace           

1800 Sunderland v Southampton

1800 West Ham United v West Bromwich Albion                 

2030 Liverpool v Tottenham Hotspur     

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

LEO huko Anfield Jijini Liverpool ipo Mechi kali mno ya EPL, Ligi Kuu England, EPL-FEB5-Bkati ya Liverpool na Tottenham.

Liverpool wapo Nafasi ya 5 na wana Pointi 46 wakati Spurs wapo Nafasi ya 2 na wana Pointi 50.

Mbali ya Timu hizi kugombea kupanda Chati, kitu muhimu ni athari ya kipigo kwani ikiwa Spurs watafungwa wanaweza kutupwa na kuwa Pointi 12 nyuma ya Vinara Chelsea huku kipigo kwa Liverpool kinaweza kuwafanya wawe Pointi 16 nyuma ya Chelsea.

Lakini pia, kwa Suprs, rekodi yao Uwanjani Anfield si nzuri hata kidogo na pia rekodi yao kwa ujumla dhidi ya Liverpool ni mbovu kwani mara ya mwisho kushinda ni Novemba 2012.

Hata hivyo, Spurs wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na moto kwani hawajafungwa katika Mechi 10 wakati Liverpool wameshinda Mechi 1 tu kati ya 10 walizocheza mwisho na Mechi yao ya mwisho kutwangwa 2-0 na Hull City.

++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-Spurs imefungwa Mechi 15 kati ya 24 walizocheza Anfield dhidi ya Liverpool kwenye Ligi Kuu England wakishinda 2 tu na Sare 9.

++++++++++++++++++

VIKOSI-LIVER-SPURSLiverpool wana hatihati ya kuwakosa Wachezaji wenye maumivu ambao ni Klavan, Lallana na Lovren na ambao ni Majeruhi na watakosekana jkabisa ni Grujic, Ejaria na Ings.

Kwa upande wa Spurs, Majeruhi ambao watakosekana ni Rose, Vertonghen, Lamela na Nkoudou.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

Jumapili Februari 12

1600 Burnley v Chelsea    

1900 Swansea City v Leicester City                 

Jumatatu Februari 13

2300 Bournemouth v Manchester City