EMIRATES FA CUP – RAUNDI YA 3: LEO MABINGWA MAN UNITED WAANZA UTETEZI OLD TRAFFORD, KUIVAA READING YA JAAP STAM!

FA-CUP-16-17-ROONEY-KOMBEMABINGWA Watetezi wa Kombe Kongwe kabisa Duniani, FA CUP, Leo wanaanza utetezi wao kwa kucheza Mechi ya Raundi ya 3 ya Kombe hilo Uwanjani kwao Old Trafford dhidi ya Timu ya Daraja la chini Reading.

Hii Raundi ya 3 ndio inayoingiza kwa mara ya kwanza Timu za EPL na zile za Daraja la chini yake, Championship, kushiriki Mashindano haya yaliyotanguliwa na Raundi za Awali zilizohusishwa Timu za Madaraja ya chini.

Hivi sasa Reading wapo chini ya Meneja Jaap Stam ambae ni Mchezaji wa zamani wa Man United aliechezea Klabu hiyo kwa Miaka Mitatu kuanzia 1998 na hii ni mara yake ya kwanza kurejea Old Trafford.

Hii Leo Meneja wa Man United, Jose Mourinho, anatarajiwa kubadili Kikosi chake huku akitupia jicho Mechi zao zijazo ya kwanza ikiwa ni Nusu Fainali ya EFL CUP Jumanne ijayo dhidi ya Hul City na inayofuata ni ya EPL, Ligi Kuu England, dhidi ya Liverpool Uwanjani Old Trafford.

Man United haitakuwa nae Beki Eric Bailly ambae amejiunga na Kikosi cha Timu ya Taifa ya Ivory Coast kitakachocheza AFCON 2017 huko Gabon kuanzia Januari 14.

Wengine ambao hawamo Kikosini ni Memphis Depay na Morgan Scneiderlin wanaohusishwa na kuhama Dirisha la Uhamisho la hii Januari.

Baadhi ya Wachezaji wanaotarajiwa kuanza Mechi hii na Reading ni Nahodha Wayne Rooney, aliekosa Mechi 3 zilizopita akiwa Majeruhi, pamoja na Kipa Sergio Romero na pengine Kiungo Bastian Schweinsteiger.

Kwa upande wa Reading, wao watawakosa Majeruhi Stephen Quinn na Deniss Rakels.

Reading hivi sasa wapo Nafasi ya 3 kwenye Ligi ya Championship na wapo kwenye wimbi la ushindi wa Mechi 3 mfululizo za Ligi hiyo.

Kikosi cha Reading kina Wachezaji Wawili ambao waliwahi kuwa Man United na hao ni Mabeki Paul McShane na Tyler Blackett.

Uso kwa Uso

Man United wameshinda Mechi 11 na Sare 7 kati ya Mechi 19 walizocheza mwisho na ya mwisho kukutana ni Msimu wa 2012/13 wakati Wayne Rooney alipofunga Bao pekee na la Ushindi.

++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.

-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.

-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.

-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.

-Bingwa Mtetezi ni Manchester United.

+++++++++++++++++++

Mbali ya Mechi hii ya Old Trafford, zipo Mechi nyingine 24.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

MANCHESTER UNITED: Romero, Fosu-Mensah, Smalling, Blind, Shaw, Fellaini, Herrera, Martial, Mata, Rashford, Ibrahimovic.

READING: Al Habsi, Blackett, Moore, Gunter, McShane, Beerens, Swift, Van den Berg, McCleary, Williams, Kermorgant.

REFA: Andre Marriner

EMIRATES FA CUP:

Ratiba/Matokeo:

**Mechi zote kuanza Saa 12 Jioni isipokuwa inapotajwa

Ijumaa Januari 6

West Ham United 0 Manchester City 5             

Jumamosi Januari 7

1530 Manchester United v Reading                 

Accrington Stanley v Luton Town          

Barrow v Rochdale           

Birmingham City v Newcastle United               

Blackpool v Barnsley                  

Bolton Wanderers v Crystal Palace                  

Brentford v Eastleigh                 

Brighton & Hove Albion v Milton Keynes Dons            

Bristol City v Fleetwood Town               

Everton v Leicester City              

Huddersfield Town v Port Vale              

Hull City v Swansea City             

Ipswich Town v Lincoln City                 

Millwall v Bournemouth              

Norwich City v Southampton                

Queens Park Rangers v Blackburn Rovers                 

Rotherham United v Oxford United                 

Stoke City v Wolverhampton Wanderers           

Sunderland v Burnley                 

Sutton United v AFC Wimbledon           

Watford v Burton Albion             

West Bromwich Albion v Derby County            

Wigan Athletic v Nottingham Forest                

Wycombe Wanderers v Stourbridge                

2030 Preston North End v Arsenal          

Jumapili Januari 8

1430 Cardiff City v Fulham

1630 Liverpool v Plymouth Argyle

Chelsea v Peterborough United             

Middlesbrough v Sheffield Wednesday             

1900 Tottenham Hotspur v Aston Villa             

Jumatatu Januari 9

2245 Cambridge United v Leeds United 

TAREHE MUHIMU:

HATUA

RAUNDI

DROO

MECHI

Raundi za Awali

Raundi ya Awali kabisa

8 Julai 2016

6 Agosti 2016

Raundi ya Awali

20 Agosti 2016

Raundi ya 1 Mchujo

15 Agosti 2016

3 Septemba 2016

Raundi ya 2 Mchujo

5 Septemba 2016

17 Septemba 2016

Raundi ya 3 Mchujo

19 Septemba 2016

1 Oktoba 2016

Raundi ya 4 Mchujo

3 Oktoba 2016

15 Oktoba 2016

Mashindano rasmi

Raundi ya 1

17 Oktoba 2016

5 Novemba 2016

Raundi ya 2

7 Novemba 2016

3 Desemba 2016

Raundi ya 3

5 Desemba 2016

7 Januari 2017

Raundi ya 4

Kujulishwa

28 Januari 2017

Raundi ya 5

Kujulishwa

18 Februari 2017

Raundi ya 6 [Robo Fainali]

Kujulishwa

11 Machi 2017

Nusu Fainali

Kujulishwa

22 na 23 Aprili 2017

FAINALI

27 Mei 2017