EPL: ARSENAL YANUSURIKA KICHAPO, LEO KUNG’OLEWA NAFASI YA 4?

>LEO WHITE HART LANE, LONDON NI DABI SPURS v CHELSEA!

EPL – Ligi Kuu England

Matokeo:

Jumanne Januari 3

Bournemouth 3 Arsenal 3           

Crystal Palace 1 Swansea City 2            

Stoke City 2 Watford 0      

+++++++++++++++++++++++++++++

JANA USIKU huko Fitness First Stadium, Wenyeji Bournemouth waliumwaga uongozi wa 3-0 katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England,na kuiruhusu Arsenal kusawazisha Bao zote na kuambua Sare ya 3-3 huku Bao la mwisho ambalo liliiokoa Arsenal likifungwa Dakika ya 92.

Bournemouth walitangulia 2-0 hadi Haftaimu kwa Bao za Charlie Daniels na Penati Callum Wilson.

Kipindi cha Pili Bournemouth wakafunga Bao la 3 kuongoza 2-0.

Arsenal walianza kuzinduka Dakika ya 70 kwa Bao la Alexis Sanchez na Dakika 5 baadae Perez akaifanya Gemu iwe 3-2.

Bournemouth wakapata pigo Dakika ya 82 kwa kubaki Mtu 10 pale Simon Francis alipotolewa kwa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya kwa Aaron Ramsey na Arsenal kutumia mwanya huo kusawazisha kwa Kichwa cha Olivier Giroud katika Dakika ya 92.

+++++++++++

MAGOLI:

Bournemouth 3

Daniels 16’

Wilson 20’, Penati

Fraser 58’    

Arsenal 3

Sánchez 70’

Pérez 75’

Giroud 92’

+++++++++++

Matoke ohayo yamewaweka Arsenal Nafasi ya 4 kwenye EPL wakiwa Pointi 1 nyuma ya Timu ya 3 Man City na Pointi 2 mbele ya Timu zinazofuata Tottenham na Man United lakini Tottenham Leo wana nafasi ya kuiteka Nafasi ya 4 ikiwa watawafunga Vinara Chelsea huko White Hart Lane Jijini London.

ARSENAL-GIROUD-DROOBournemouth:

Boruc; Francis, Cook, Ake, Daniels; Arter, Gosling; Fraser, Stanislas, King; WilsonEPL-JAN4

Akiba: Federici, Mings, Adam Smith, Brad Smith, Surman, Ibe, Mousset.

Arsenal:

Cech; Bellerin, Mustafi, Koscielny, Monreal; Coquelin, Xhaka; Ramsey, Iwobi, Sanchez; Giroud

Akiba: Ospina, Maitland-Niles, Gabriel, Holding, Oxlade-Chamberlain, Perez, Reine-Adelaide.

REFA: Michael Oliver

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea       

Saturday 14th January 2017

1530 Tottenham Hotspur v West Bromwich Albion     

1800 Burnley v Southampton               

1800 Hull City v Bournemouth              

1800 Sunderland v Stoke City               

1800 Swansea City v Arsenal                

1800 Watford v Middlesbrough             

1800 West Ham United v Crystal Palace           

2030 Leicester City v Chelsea                

Sunday 15th January 2017

1630 Everton v Manchester City

1900 Manchester United v Liverpool