EPL: LEO ARSENAL AU SPURS KUMSHUSA CITY NAFASI YA 3!

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace                

+++++++++++++++++++++++++++++

EPL-2016-17-LOGO2LEO zipo Mechi mbili za EPL, Ligi Kuu England, za kufungua Mwaka Mpya 2017 na Timu za Arsenal na Tottenham zina nafasi murua ya kutwaa Nafasi ya 3 kwenye Ligi hiyo.

Baada ya Jana kufungwa 1-0 na Liverpool, Manchester City wameshika Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya Pili Liverpool na Pointi 10 nyuma ya Vinara Chelsea.

City pia wapo Pointi 2 mbele ya Timu ya 4 Arsenal na Pointi 3 mbele ya Timu ya 5 Spurs.

Ikiwa Leo Arsenal wataifunga Crystal Palace kwenye Mechi yao itakayochezwa Emitrates Jijini London, basi Arsenal watashika Nafasi ya 3.EPL-DEC31C

Lakini Arsenal akiteleza na Spurs kushinda Ugenini na Watford basi Spurs wataifikia City kwa Pointi na kuishusha kwa Ubora wa Magoli na wao kukamata nafasi ya 3.

Endapo zote Arsenal na Spurs zitashinda basi Arsenal watakuwa wa 3 na Spurs wa 4 huku City akiporomoka hadi Nafasi ya 5.

EPL itaendelea tena Kesho Jumatatu kwa Mechi 6.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea                 

 

 

Habari MotoMotoZ