DIRISHA LA UHAMISHO JANUARI: NANI KWENDA WAPI, MASTAA WANAOTAJWA KUHAMA!

EPL-TRANSFER17MASHABIKI wa Soka wanakodolea Macho Habari za Wachezaji Wakubwa kuhama Klabu na kwenda kwingine mara tu Dirisha la Uhamisho likifunguliwa hapo Januari Mosi.

Dirisha hilo litafungwa Januari 31.

Tayari uvumi umeshazagaa kila sehemu na baadhi yake upo ukweli lakini, kama ilivyo kawaida, nyingi hazina hata chembe ya ukweli hata kidogo.

Hivi sasa baadhi ya Majina yanayohusishwa na Uhamisho wa Januari ni yafuatayo:

Morgan Schneiderlin, Kiungo, Miaka 27, Man United

-Hana Namba Kikosi cha Jose Mourinho

-Anahusishwa na Everton, WBA

-Ada: Pauni Milioni 24

Virgil van Dijk, Sentahafu, 25, Southampton

-Ni Beki Mrefu anaecheza vizuri na kuwindwa na Klabu nyingi.

-Anahusishwa na Chelsea, Man United, Man City

Ada: Pauni Milioni 35

Mamadou Sakho, Sentahafu, 26, Liverpool

-Hajacheza hata Mechi 1 Msimu huu

-Anawindwa na PSG, Lille, WBA

-Ada: Pauni Milioni 12.5

Ross Barkley, Kiungo, 23, Everton

-Hana Namba ya kudumu kwa kukosa fomu nzuri Msimu huu.

-Anahusishwa na Tottenham

-Ada: Pauni Milioni 35

Dimitri Payet, Kiungo, 29, West Ham

-Ni Nyota anaetaka Klabu kubwa ili atwae Mataji

-Anahusishwa na Arsenal, Man United

-Ada: Pauni Milioni 35

Memphis Depay, Winga, 22, Man United

-Hana namba chini ya Jose Mourinho

-Anahusishwa na Everton, Lazio, Sevilla

Ada: Pauni Milioni 13

Asmir Begovic, Kipa, 29, Chelsea

-Msimu huu amecheza Mechi za EFL CUP tu

-Anahusishwa na Stoke, West Ham

-Ada: Mkopo

Jordan Rhodes, Straika, 26, Middlesbrough

-Hajang’ara tangu atinge Boro.

Anahusishwa na Aston Villa, Sheffield Wednesday

Ada: Pauni Milioni 9

Moussa Dembele, Kiungo Mshambuliaji, 20, Celtic

-Alifunga Bao lake la 18 Msimu huu hivi Juzi.

-Anahusishwa na Liverpool, Man City

-Ada: Pauni Milioni 20

Ademola Lookman, Winga, 19, Charlton

-Ni Tineja anaesifika sana ambae Msimu huu amefunga Bao 6

-Anahusishwa na Everton

-Ada: Pauni Milioni 11

Yacine Brahimi, Kiungo, 26, Porto

-Staa wa Algeria aliekosa Namba Msimu huu

-Anahusishwa na Everton, Arsenal, Man United

-Ada: Pauni Milioni 30

Marco Verratti, Kiungo, 24, PSG

-Wakala wake amedai hawezi kuganda Timu isiyoshinda Mataji

-Anahusishwa na Chelsea

-Ada: Pauni Milioni 40

James Rodriguez, Kiungo, 25, Real Madrid

-Hana Namba huko Real

-Anahusishwa na PSG, Inter Milan, Chelsea

Habari MotoMotoZ