MMAREKANI BOB BRADLEY AFUKUZWA UMENEJA SWANSEA!

SWANSEA-BRADLEYSwansea City imemfukuza Bob Bradley baada ya Siku 85 kama Meneja wao wa Klabu hiyo ya EPL, Ligi Kuu England.

Jumatatu, Boksing Dei Desemba 26, Swansea ilitwangwa 4-1 na West Ham kwenye Mechi ya EPL na kuachwa wakiwa Pointi 4 tu juu ya zile Timu 3 za Mkiani ambazo mwishoni mwa Msimu huporomoka Daraja.

Kipigo hicho pia kilikuwa cha 7 kwa Swansea katika Mechi 11 ambazo Bradley, Raia wa Marekani wa kwanza kuongoza EPL, kuchukuwa wadhifa Oktoba 3 toka Meneja mwingine alietimuliwa Francesco Guidolin.

Huko nyuma, Bradley aliwahi kuwa Meneja wa USA, Egypt, Klabu ya Stabaek ya Norway na Le Havre ya France kabla kuja kumrithi Francesco Guidolin alieteuliwa Mwezi Januari.

Swansea imethibiti kutimuliwa kwa Bradley na kutangaza kuwa Makocha Wasaidizi Alan Curtis na Paul Williams watashika wadhifa kuanzia Mechi yao ya Jumamosi Desemba 31 na Bournemouth.

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumatano Desemba 28

2245 Southampton v Tottenham Hotspur                  

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton             

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea