SUPA WAKALA JORGE MENDES KUTUA MANCHESTER LEO KUPIGA DILI LA £38M LA DIFENDA!

VICTOR-LINDELOFSUPA WAKALA Jorge Mendes na Rais wa Benfica ya Ureno Luis Filipe Vieira wameripotiwa wako niani kutua Jiji la Manchester kukamilisha Dili la Uhamisho wa Pauni Milioni 38 wa Beki Victor Lindelof.

Ripoti hizi zimevujishwa na Gazeti maarufu huko Ureno, O Jogo, ambalo limedai Manchester United watamnunua Beki huyo mwenye Umri wa Miaka 22.

Lindelof, ambae ni Sentahafu, atakuwa Mchezaji wa Kwanza kusainiwa na Jose Mourinho katika Dirisha lijalo linalofunguliwa Januari Mosi.

Kusainiwa haraka kwa Beki huyo ni kuzidi pengo la Majeruhi Eric Bailly na Chris Smalling na hasa kwa vile Bailly anatarajiwa kutokuwepo Januari yote akiwa huko kwenye Fainali za AFCON 2017 na Nchi yake Ivory Coast.

++++++++++++++++++++++++++++++++

Ni Nani Victor Lindelof?

Kuzaliwa:Julai 17, 1994 (Miaka 22)

Nafasi: Sentahafu

Wasifu: Lindelof alisainiwa na Benfica kutoka Klabu ya Sweden Vasteras SK akiwa na Miaka 17 na kuichezea Timu ya Kwanza Oktoba 2013.

Mwaka Jana ndio hasa aling’ara kwa kuisaidia Benfica kutwaa Ubingwa na pia kuwemo Kikosi cha Timu ya Taifa ya Sweden iliyocheza Fainali za EURO 2016 huko France.

Ni Mrefu wa Futi 6 Nci 2 na aliekakamaa Musuli na mwenye nguvu.

++++++++++++++++++++++++++++++++

Mendes, ambae pia Wakala wa Mourinho na Cristiano Ronaldo, ndie anatarajiwa kuilainisha Dili hii kati ya Menejimenti za Man United na Benfica ambazo zinavutana kuhusu Dau huku Benfica wakitaka zaidi ya Pauni Milioni 38.

Kukosekana kwa Bailly na Smalling kulimlazimisha Mourinho kuwatumia Phil Jones na Marcos Rojo kama Masentahafu na usajili huu unaifanya Man United iimarishe safu yake ya ulinzi.

Hivi sasa Man United wamejiimarisha Nafasi ya 6 ya EPL, Ligi Kuu England baada ya kushinda Mechi 3 mfululizo na kukata pengo lao na Timu ya 5 Tottenham kuwa Pointi 3 na Pointi 4 kwa Timu ya 4 Arsenal.

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumatatu Desemba 19

2300 Everton v Liverpool  

Jumatatu Desemba 26

1530 Watford v Crystal Palace              

1800 Arsenal v West Bromwich Albion            

1800 Burnley v Middlesbrough              

1800 Chelsea v Bournemouth               

1800 Leicester City v Everton               

1800 Manchester United v Sunderland            

1800 Swansea City v West Ham United           

2015 Hull City v Manchester City  

Habari MotoMotoZ