SCHWEINI KUBAKI OLD TRAFFORD!

MANUNITED-SCHWEINIKEPTENI wa zamani wa Mabingwa wa Dunia Germany, Bastian Schweinsteiger, atabakia Manchester United na kucheza kwenye UEFA EUROPA LIGI.
Uamuzi huo umetobolewa na Meneja wa Man United Jose Mourinho Jana mara baada ya kuwafunga Wigan 4-0 na kutinga Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP kwenye Mechi ambayo Schweinsteiger alifunga Bao la kusisimua mno.
Mwanzoni mwa Msimu, Schweinsteiger, mwenye Miaka 32, hakujumuishwa kwenye Kikosi cha Man United kilichosajiliwa UEFA EUROPA LIGI na kuondolewa toka kwenye Kikosi cha Kwanza.
Akiongea hapo Jana, Mourinho alieleza: "Hatuna Wachezaji wengi wa Kiungo na hivyo yeye anaweza kutumika. Ataingizwa Listi ya EUROPA LIGI kwa sababu zipo nafasi baada kuondoka Memphis Depay na Morgan Schneiderlin."
Schneiderlin aliuzwa kwa Everton Januari 12 na Siku 8 baadae Depay akahamia Lyon ya France.
Mechi na Wigan ni ya 3 kwa Schweinsteiger kucheza chini ya Mourinho baada kurudishwa Kikosi cha Kwanza Mwezi Oktoba.
Man United watacheza Old Trafford na Saint-Etienne ya France kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI hapo Februari 16 na kurudiana Ugenini Wiki moja baadae.

BEKI SUNDERLAND APIMWA PALACE

VANAANHOLTBEKI wa Sunderland Patrick van Aanholt anafanyiwa upimwaji Afya yake huko Crystal Palace baada Klabu hizo mbili kuafikiana Dili inayotegemewa kufikia Pauni Milioni 14.

Beki huyo wa Kimataifa wa Netherlands mwenye Miaka 26 ataungana tena na Bosi wa Palace Sam Allardyce ambae walikuwa nae wote Sunderland.

Van Aanholt alianza kuchezea Chelsea lakini akapelekwa kucheza nje kwa Mkopo kewenye Klabu 5 na hatimae kusaini Mkataba wa kudumu na Sunderland Mwaka 2014 na kuichezea Mechi 95.

Big Sam, kama anavyojulikana Meneja wa Palace, amedokeza kuwa wapo kwenye mipango ya kusaini Wachezaji wengine wapya kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa Januari 31 huku akidokeza hawajapokea Ofa yeyote ya Mchezaji yao yeyote kutakiwa na Klabu nyingine.

Ameeleza: “Zipo dili kadhaa lakini hazijakamilika.”

Van Aanholt amekuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Allardyce tangu atue Palace Mwezi uliopita kuchukua nafasi ya Alan Pardew.

Mwingine aliesainiwa na Big Sam ni Jeffrey Schlupp kutoka kwa Mabingwa wa England Leicester City kwa Dau la Pauni Milioni 13.

LEJENDARI SIR ALEX ANENA: “HAKUNA ATAEVUNJA REKODI YA ROONEY!”

ROONEY-REKODI-250LEJENDARI wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametamka kuwa Rekodi ya Wayne Rooney ya kuifungia Klabu hiyo Mabao 250 haitavunjwa.

Rooney, mwenye Miaka 31, alifunga Bao lake la 250 kwa Klabu yake Manchester United Jumamosi iliyopita katika Dakika ya 94 walipotoka 1-1 na Stoke City huko Britannia Stadium kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

Bao hilo lilivunja Rekodi ya Mfungaji Bora katika Historia ya Man United, Sir Bobby Charlton, aliyoishikilia kwa Miaka 44.

Mwaka Jana, Rooney pia aliivunja Rekodi ya Sir Bobby Charlton na kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya Timu ya Taifa ya England.

Sir Alex Ferguson, ambae alikuwa Meneja wa Man United tangu 1986 hadi 2013 na ambae pia ndie aliemchukua Roooney Mwaka 2004 kutoka Everton, ameeleza: “Rekodi ilidumu Miaka 44 na wakati Rooney anajiunga sikutegemea kama atavunja Rekodi ya Sir Bobby! Kufanya hilo ni kitu kikubwa. Ni ajabu! Yeye amecheza kama Gemu 200 chini ya zile za Sir Bobby. Na hilo ni ajabu zaidi!”

Aliongeza: ‘Sidhani kama kuna Mtu atampita Rooney. Siwezi kusema hapana, hapana usiseme hapa, lakini ukitizama Soka la sasa, Man United ni moja ya Klabu chache kabisa kuweka Mchezaji kwa Miaka 10!”

FIFA YAITUPIA ZIGO LIVERPOOL KUAMUA MATIP KUCHEZA AU LA BAADA YA KUIKATAA CAMEROON!

LIVER-MATIP-SITLIVERPOOL wameambiwa kinagaubaga na FIFA waamue wenyewe kama Mchezaji wao Joel Matip anaweza kuichezea Timu hiyo baada ya kukataa kujiunga na Cameroon kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yanayoendelea huko Gabon hivi sasa.

Liverpool waliamua wenyewe kumtoa Matip Kikosini Jumapili walipocheza huko Old Trafford na Manchester United kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, wakidai wanangoja ufafanuzi wa FIFA.

Hii Leo FIFA imetoa ufafanuzi na kuitaka Liverpool kufuata Kanuni zinazohusu Wachezaji na moja ikiwa ile inayotaka Mchezaji anaeitwa na Nchi yake kuichezea Timu ya Taifa kutoichezea Klabu yake katika kipindi hicho.

Liverpool imekuwa ikidai Matip hakuwemo kwenye Kikosi cha mwisho cha AFCON 2017 na kabla alishatangaza kuachana na kuichezea Cameroon.

Hata hivyo, Liverpool wameshindwa kumtumia Matip kwenye Mechi zao na kumwacha Meneja wao Jurgen Klopp akilalamika baada ya Shirikisho la Soka la Cameroon, FECAFOOT, kukaa kimya na kutojibu maombi ya Liverpool ya kutaka ufafanuzi na uthibitisho.

FIFA pia hii Leo imefafanua kuwa Chama cha Soka cha Nchi kikitaka kumwita Mchezaji kwa ajili ya Mashindano ya Fainali za Kimataifa inapaswa kumjulisha Mchezaji anaehusika kwa Maandishi si chini ya Siku 15 kabla Siku anayopaswa kujiunga rasmi na Nchi yake na Taarifa hiyo pia inapaswa kupelekwa kwa Klabu ya Mchezaji huyo katika muda huo huo.

FIFA pia imesisitiza kukiukwa kwa Kanuni hizo kutafanya Wahusika kuburuzwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA.

Hadi sasa haijulikani kama FECAFOOT ilitoa rasmi Notisi hiyo ya Siku 15 kwa Matip na Liverpool.

EPL - TUZO: MCHEZAJI BORA IBRAHIMOVIC, GOLI BORA MKHITARYAN!

MANUNITED-TUZO-DECZlatan Ibrahimovic ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa EPL, Ligi Kuu England, kwa Mwezi Desemba na mwenzake wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan kuzoa ile ya Goli Bora.

Ibrahimovic, Mchezaji kutoka Sweden mwenye Miaka 35, alifunga Bao 5 Mwezi Desemba na sasa ana Jumla ya Mabao 18 tangu ajiunge na Man United mwanzoni mwa Msimu.

Desemba alifungua akaunti yake kwa Bao dhidi ya Everton huko Goodison Park na kisha kupiga Bao la ushindi kule Selhurst Park walipoicharanga Crystal Palace 2-1.

The Hawthorns ilishuhudia Ibrahimovic akipiga 2 wakati Man United inaipiga West Bromwich Albion 2-0 na kuifunga Sunderland 1 Siku ya Boksing Dei.

Pia, Ibrahimovic alifunga wakati Man United inaibwaga Zorya Luhansk 2-0 kwenye UEFA EUROPA LIGI huko Ukraine.

Tuzo hii kwa Ibrahimovic inafuatia zile za Raheem Sterling wa Manchester City, Son Heung-min wa Tottenham Hotspur na Wawili wa Chelsea Eden Hazard na Diego Costa kwa Msimu huu.

Tuzo nyingine ya Goli Bora la Mwezi imekwenda kwa Mchezaji mwingine wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan, kwa Bao lake la ushindi dhidi ya Sunderland ambalo limebatizwa ‘Kiki ya Nge’, Scorpion Kick.