FIFA YAITUPIA ZIGO LIVERPOOL KUAMUA MATIP KUCHEZA AU LA BAADA YA KUIKATAA CAMEROON!

LIVER-MATIP-SITLIVERPOOL wameambiwa kinagaubaga na FIFA waamue wenyewe kama Mchezaji wao Joel Matip anaweza kuichezea Timu hiyo baada ya kukataa kujiunga na Cameroon kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2017, yanayoendelea huko Gabon hivi sasa.

Liverpool waliamua wenyewe kumtoa Matip Kikosini Jumapili walipocheza huko Old Trafford na Manchester United kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, wakidai wanangoja ufafanuzi wa FIFA.

Hii Leo FIFA imetoa ufafanuzi na kuitaka Liverpool kufuata Kanuni zinazohusu Wachezaji na moja ikiwa ile inayotaka Mchezaji anaeitwa na Nchi yake kuichezea Timu ya Taifa kutoichezea Klabu yake katika kipindi hicho.

Liverpool imekuwa ikidai Matip hakuwemo kwenye Kikosi cha mwisho cha AFCON 2017 na kabla alishatangaza kuachana na kuichezea Cameroon.

Hata hivyo, Liverpool wameshindwa kumtumia Matip kwenye Mechi zao na kumwacha Meneja wao Jurgen Klopp akilalamika baada ya Shirikisho la Soka la Cameroon, FECAFOOT, kukaa kimya na kutojibu maombi ya Liverpool ya kutaka ufafanuzi na uthibitisho.

FIFA pia hii Leo imefafanua kuwa Chama cha Soka cha Nchi kikitaka kumwita Mchezaji kwa ajili ya Mashindano ya Fainali za Kimataifa inapaswa kumjulisha Mchezaji anaehusika kwa Maandishi si chini ya Siku 15 kabla Siku anayopaswa kujiunga rasmi na Nchi yake na Taarifa hiyo pia inapaswa kupelekwa kwa Klabu ya Mchezaji huyo katika muda huo huo.

FIFA pia imesisitiza kukiukwa kwa Kanuni hizo kutafanya Wahusika kuburuzwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA.

Hadi sasa haijulikani kama FECAFOOT ilitoa rasmi Notisi hiyo ya Siku 15 kwa Matip na Liverpool.

EPL - TUZO: MCHEZAJI BORA IBRAHIMOVIC, GOLI BORA MKHITARYAN!

MANUNITED-TUZO-DECZlatan Ibrahimovic ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa EPL, Ligi Kuu England, kwa Mwezi Desemba na mwenzake wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan kuzoa ile ya Goli Bora.

Ibrahimovic, Mchezaji kutoka Sweden mwenye Miaka 35, alifunga Bao 5 Mwezi Desemba na sasa ana Jumla ya Mabao 18 tangu ajiunge na Man United mwanzoni mwa Msimu.

Desemba alifungua akaunti yake kwa Bao dhidi ya Everton huko Goodison Park na kisha kupiga Bao la ushindi kule Selhurst Park walipoicharanga Crystal Palace 2-1.

The Hawthorns ilishuhudia Ibrahimovic akipiga 2 wakati Man United inaipiga West Bromwich Albion 2-0 na kuifunga Sunderland 1 Siku ya Boksing Dei.

Pia, Ibrahimovic alifunga wakati Man United inaibwaga Zorya Luhansk 2-0 kwenye UEFA EUROPA LIGI huko Ukraine.

Tuzo hii kwa Ibrahimovic inafuatia zile za Raheem Sterling wa Manchester City, Son Heung-min wa Tottenham Hotspur na Wawili wa Chelsea Eden Hazard na Diego Costa kwa Msimu huu.

Tuzo nyingine ya Goli Bora la Mwezi imekwenda kwa Mchezaji mwingine wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan, kwa Bao lake la ushindi dhidi ya Sunderland ambalo limebatizwa ‘Kiki ya Nge’, Scorpion Kick.

MORGAN SCHNEIDERLIN KUHAMA MAN UNITED KWENDA EVERTON, ADA YAKUBALIWA!

MORGAN-SCHNEIDERLINRIPOTI toka England zimebaini kuwa Klabu za Manchester United na Everton zimeafikiana Ada ya Uhamisho ya Pauni Milioni 22 kwa Kiungo Morgan Schneiderlin.
Schneiderlin, mwenye Miaka 27, alisaini Manchester United kutoka Southampton kwa Dau la Pauni Milioni 25 Julai 2015 kwenye wakati wa himaya ya Meneja Louis van Gaal.
Kiungo huyo wa Kimataifa wa France ameichezea Man United Mechi 47 lakini tangu ujio wa Jose Mourinho Msimu huu amecheza Mechi 8 tu na 3 zikiwa za EPL, Ligi Kuu England.
Mara Jana baada ya Man United kuifunga Hull City 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya EFL CUP, Mourinho aligusia Uhamisho wa Schneiderlin na kueleza kuwa Makamu Mwenyekiti Mtendaji Ed Woodward alimweleza kuwa Mchezaji huyo anakaribia kuhama.
Mourinho alisema: "Nasikitika na nina furaha, nasikitika kwa sababu nampenda na angeweza kutusaidia kinamna lakini nina furaha kwa sababu hili ndio alilitaka, anataka kucheza kila Mechi na kuwa muhimu kwenye Timu!"
Ikiwa Uhamisho huu wa Schneiderlin utakamilika, Mchezaji huyo ataungana tena na Meneja Ronald Koeman huko Goodison Park baada ya kuwa wote kwa Miaka Miwili huko Southampton.
Mbali ya Schneiderlin, Koeman pia anamtaka Mchezaji mwingine wa Man United, Memphis Depay, atue Everton.
Lakini kwa Depay, Everton huenda wakaingia mvutano na Klabu nyingine za Ulaya zinazomtaka.
Depay, mwenye Miaka 22, alijiunga Man United Mei 2015 kwa Dau la Pauni Milioni 25 kutoka PSV Eindhoven ya Uholanzi.

REFA MIKE DEAN KUCHEZESHA SPURS-VILLA LICHA KUWA KIKAANGONI KADI NYEKUNDU YA FEGHOULI!

REFA-MIKE-DEANREFA Mike Dean antakuwa dimbani Jumapili kuchezesha Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP kati ya Tottenham Hotspur na Aston Villa licha kulalamikiwa kuhusu uamuzi wake wa kumpa Kiungo wa West Ham United kutoka Algeria Sofiane Feghouli Kadi Nyekundi kwa rafu yake dhidi ya Beki wa Manchester United Phil Jones.

West Ham imethibitisha kukataa Rufaa kupinga hiyo Kadi Nyekundu ya Feghouli na FA, Chama cha Soka England, kitatoa uamuzi wa Rufaa hiyo baadae Leo.

Feghouli, mwenye Miaka 27, amekuwa Mchezaji wa 5 kuonyeshwa Kadi Nyekundu na Refa Mike Dean Msimu huu.

Baada ya Mechi hiyo, Wachambuzi na Mashabiki wengi walikuja juu kuhusu uamuzi huo wa Refa Dean lakini Listi ya Marefa kwa ajili ya Mechi za FA CUP za Wikiendi hii ilikuwa tayari imeshatoka kabla ya Mechi ya Man United na West Ham.

Hadi sasa, PGMOL, Taasisi inayosimamia Marefa wa Kulipwa huko England, inaaminika haina nia kumwadhibu Dean ingawa habari za ndani zimedai wamekiri kosa la Dean.

Lakini pia inaaminika PGMOL inaelewa ni kwanini Dean alitoa Kadi Nyekundu wakiamini Dean aliona Mguu wa Feghouli uko juu na kugongana na Jones aliepiga kelele kwa maumivu matukio yote yakitokea kwa muda mfupi mno na spidi kali.

Refa Mike Dean ameshaichezesha Tottenham mara 3 Msimu huu, Mechi zote zikiwa za Ligi, na kila Mechi amempa Kadi Nyekundu Mchezaji wa Timu pinzani ya Tottenham wakiwa ni Adnan Januzaj wa Sunderland, Winston Reid wa West Ham na Nathan Redmond wa Southampton.

BAO LA NGE: MJADALA WAZUKA – LIPI BORA OLIVIER GIROUD V HENRIKH MKHITARYAN?

KUMEZUKA MJADALA mkubwa huko England na Duniani kote Mashabiki wakizozana Mitandaoni baada ya kufungwa Mabao Mawili ya ajabu kwa Kisigino na kubatizwa ‘Scorpion Kick’, kwa Kiswahili Kiki ya Nge.

Bao hizo mbili zilifungwa wakati Manchester United wakicheza na Sunderland Siku ya Boksing Dei na jingine Jana wakati Arsenal ikicheza na Crystal Palace.

Kwenye Mechi na Sunderland, Henrikh Mkhitaryan alifunga Bao kwa Kisigino kwa kuruka juu na Olivier Giroud alifunga Bao kama hilo wakati Arsenal ikiichapa Palace.

Wakati wote wakikiri Mabao hayo yanastahili kuwa Mabao Bora ya Msimu, sasa umezuka Mjadala mkali kwamba lipi kati ya Bao hizo ni Bora kupita jingine.

JE WEWE UNAONAJE?

LIPI BORA LA MKHITARYAN au GIROUD?

MKHI-GIROUD

Habari MotoMotoZ