KLABU ULAYA: PILIKAPILIKA ZA UEFA CHAMPIONZ LIGI, EUROPA LIGI WIKI IJAYO!

>PSG, BARCA, REAL, ARSENAL DIMBANI, MAN UNITED, SPURS KILINGENI!

ULAYAMechi za Mtoano za Mashindano makubwa Barani Ulaya, UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI na UEFA EUROPA LIGI, zitakuwa kilingeni kuanzia Jumanne hadi Alhamisi Wiki ijayo.

Jumanne Usiku zipo Mechi 2 za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL kati ya Benfica na Borussia Dortmund na nyingine ni Paris Saint Germain kucheza na Barcelona.

Jumatano Usiku pia zipo Mechi nyingine 2 za za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL kati ya Bayern Munich na Arsenal na pia Mabingwa Watetezi Real Madrid kucheza na Napoli.

Alhamisi Usiku ndio Usiku wa UEFA EUROPA LIGI ambapo zipo Mechi 16 za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 na miongoni mwake ni Manchester United kucheza kwao Old Trafford na Klabu ya France Saint-Etienne wakati wenzao wa England, Tottenham Hotspur, wakiwa Ugenini Nchini Belgium kucheza na KAA Gent.

Pia kwenye Mashindano hayo, Klabu ya Straika wa Tanzania Mbwana Samatta Genk ya Belgium ipo Ugenini huko Romania kucheza na Astra Giurgiu.

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

Mechi za Kwanza

**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo

Jumanne 14 Februari 2017

Benfica v Borussia Dortmund          

Paris Saint Germain v Barcelona              

Jumatano 15 Februari 2017

Bayern Munich v Arsenal                 

Real Madrid v Napoli              

Jumanne 21 Februari 2017

Bayer 04 Leverkusen v Atlético Madrid              

Manchester City v Monaco               

Jumatano 22 Februari 2017

FC Porto v Juventus               

Sevilla v Leicester City           

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++

UEFA EUROPA LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 32

Mechi za Kwanza

**Saa za Bongo

1900 Krasnodar v Fenerbahce

2100 AZ Alkmaar v Lyon

2100 Celta Vigo v Shakhtar Donetsk

2100 Borussia Monchengladbach v Fiorentina

2100 Olympiakos v Osmanlispor

2100 KAA Gent v Tottenham Hotspur

2100 FK Rostov v Sparta Prague

2100 Astra Giurgiu v Genk

2100 Ludogorets v FC Copenhagen

2305 Athletic Bilbao v Apoel Nicosia

2305 Legia Warsaw v Ajax

2305 Anderlecht v Zenit St Petersburg

2305 Manchester United v Saint-Etienne

2305 Villarreal v Roma

2305 Hapoel Beer Sheva v Besiktas

2305 PAOK v Schalke

         

 

UEFA CHAMPIONZ LIGI: PEP ASALIMU KWA YAYA, AREJESHWA KUNDINI ULAYA!

CITY-PEP-YAYAKIUNGO Yaya Toure amerejeshwa Kikosini mwa Manchester City kwa ajili ya Mechi zao za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL.

Toure, mwenye Miaka 33, hakusajiliwa kwa ajili ya Mechi za Makundi za UCL na pia kutupwa nje ya Kikosi cha Kwanza cha Man City baada ya Meneja wa Timu hiyo Pep Guardiola kuingia kwenye Bifu na Wakala wa Gwiji huyo kutoka Ivory Coast.

Wakala Dimitri Seluk alimijia juu Guardiola na Meneja huyo kuapa Toure hatakuwemo Kikosini mwake hadi aombwe radhi.

Wakala huyo hakuomba radhi na ikabidi Yaya Toure mwenyewe achukue jukumu hilo na kuanzia Novemba, Kiungo huyo akarejeshwa Kikosi cha Kwanza.

Kwenye UCL, Toure anachukuwa Nafasi ya Ilkay Gundogan ambae ni Majeruhi.

Man City wataivaa AS Monaco hapo Februari 21 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL.

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo

Jumanne 14 Februari 2017

Benfica v Borussia Dortmund                

Paris Saint Germain v Barcelona            

Jumatano 15 Februari 2017

Bayern Munich v Arsenal             

Real Madrid v Napoli                  

Jumanne 21 Februari 2017

Bayer 04 Leverkusen v Atlético Madrid             

Manchester City v Monaco          

Jumatano 22 Februari 2017

FC Porto v Juventus          

Sevilla v Leicester City                

Jumanne 7 Machi 2017

Arsenal v Bayern Munich             

Napoli v Real Madrid                  

Jumatano 8 Machi 2017

Barcelona v Paris Saint Germain            

Borussia Dortmund v Benfica                

Jumanne 14 Machi 2017

Juventus v FC Porto          

Leicester City v Sevilla                

Jumatano 15 Machi 2017

Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen             

Monaco v Manchester City          

++++++++++++++++++++++++++++

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MTOANO:

14/15 na 21/22 Feb 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza

7/8 na 14/15 Machi 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Pili

11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza

18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

SCHWEINI KUBAKI OLD TRAFFORD!

MANUNITED-SCHWEINIKEPTENI wa zamani wa Mabingwa wa Dunia Germany, Bastian Schweinsteiger, atabakia Manchester United na kucheza kwenye UEFA EUROPA LIGI.
Uamuzi huo umetobolewa na Meneja wa Man United Jose Mourinho Jana mara baada ya kuwafunga Wigan 4-0 na kutinga Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP kwenye Mechi ambayo Schweinsteiger alifunga Bao la kusisimua mno.
Mwanzoni mwa Msimu, Schweinsteiger, mwenye Miaka 32, hakujumuishwa kwenye Kikosi cha Man United kilichosajiliwa UEFA EUROPA LIGI na kuondolewa toka kwenye Kikosi cha Kwanza.
Akiongea hapo Jana, Mourinho alieleza: "Hatuna Wachezaji wengi wa Kiungo na hivyo yeye anaweza kutumika. Ataingizwa Listi ya EUROPA LIGI kwa sababu zipo nafasi baada kuondoka Memphis Depay na Morgan Schneiderlin."
Schneiderlin aliuzwa kwa Everton Januari 12 na Siku 8 baadae Depay akahamia Lyon ya France.
Mechi na Wigan ni ya 3 kwa Schweinsteiger kucheza chini ya Mourinho baada kurudishwa Kikosi cha Kwanza Mwezi Oktoba.
Man United watacheza Old Trafford na Saint-Etienne ya France kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI hapo Februari 16 na kurudiana Ugenini Wiki moja baadae.

BEKI SUNDERLAND APIMWA PALACE

VANAANHOLTBEKI wa Sunderland Patrick van Aanholt anafanyiwa upimwaji Afya yake huko Crystal Palace baada Klabu hizo mbili kuafikiana Dili inayotegemewa kufikia Pauni Milioni 14.

Beki huyo wa Kimataifa wa Netherlands mwenye Miaka 26 ataungana tena na Bosi wa Palace Sam Allardyce ambae walikuwa nae wote Sunderland.

Van Aanholt alianza kuchezea Chelsea lakini akapelekwa kucheza nje kwa Mkopo kewenye Klabu 5 na hatimae kusaini Mkataba wa kudumu na Sunderland Mwaka 2014 na kuichezea Mechi 95.

Big Sam, kama anavyojulikana Meneja wa Palace, amedokeza kuwa wapo kwenye mipango ya kusaini Wachezaji wengine wapya kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa Januari 31 huku akidokeza hawajapokea Ofa yeyote ya Mchezaji yao yeyote kutakiwa na Klabu nyingine.

Ameeleza: “Zipo dili kadhaa lakini hazijakamilika.”

Van Aanholt amekuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Allardyce tangu atue Palace Mwezi uliopita kuchukua nafasi ya Alan Pardew.

Mwingine aliesainiwa na Big Sam ni Jeffrey Schlupp kutoka kwa Mabingwa wa England Leicester City kwa Dau la Pauni Milioni 13.

LEJENDARI SIR ALEX ANENA: “HAKUNA ATAEVUNJA REKODI YA ROONEY!”

ROONEY-REKODI-250LEJENDARI wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametamka kuwa Rekodi ya Wayne Rooney ya kuifungia Klabu hiyo Mabao 250 haitavunjwa.

Rooney, mwenye Miaka 31, alifunga Bao lake la 250 kwa Klabu yake Manchester United Jumamosi iliyopita katika Dakika ya 94 walipotoka 1-1 na Stoke City huko Britannia Stadium kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

Bao hilo lilivunja Rekodi ya Mfungaji Bora katika Historia ya Man United, Sir Bobby Charlton, aliyoishikilia kwa Miaka 44.

Mwaka Jana, Rooney pia aliivunja Rekodi ya Sir Bobby Charlton na kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya Timu ya Taifa ya England.

Sir Alex Ferguson, ambae alikuwa Meneja wa Man United tangu 1986 hadi 2013 na ambae pia ndie aliemchukua Roooney Mwaka 2004 kutoka Everton, ameeleza: “Rekodi ilidumu Miaka 44 na wakati Rooney anajiunga sikutegemea kama atavunja Rekodi ya Sir Bobby! Kufanya hilo ni kitu kikubwa. Ni ajabu! Yeye amecheza kama Gemu 200 chini ya zile za Sir Bobby. Na hilo ni ajabu zaidi!”

Aliongeza: ‘Sidhani kama kuna Mtu atampita Rooney. Siwezi kusema hapana, hapana usiseme hapa, lakini ukitizama Soka la sasa, Man United ni moja ya Klabu chache kabisa kuweka Mchezaji kwa Miaka 10!”

Habari MotoMotoZ