COPPA ITALIA: HIGUAIN AIPELEKA JUVE FAINALI KUIVAA LAZIO!

HIGUAIN-JUVEMabingwa wa Italy Juventus Jana wametinga Fainali ya Kombe la Italy, COPPA ITALIA, licha kufungwa 3-2 na Napoli waliokuwa kwao Uwanjani San Paolo kwa vile walishinda 3-1 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali iliyochezwa huko Turin.
Kupenya kwa Juve kutinga Fainali ambako watacheza na Lazio ni kwa sababu ya Bao 2 za Gonzalo Higuain alizofunga Jana dhidi ya Klabu yake ya zamani.
Higuain alifunga Bao la Kwanza Dakika ya 32 na Marek Hamsik kuisawazishia Napoli Dakika ya 53 lakini Higuain akaipa Juve Bao la Pili Dakika ya 59.
Napoli wakajibu kwa Bao za Dakika za 61 na 67 kupitia Dries Mertens na Lorenzo Insigne lakini ushindi huo wa 3-2 haukutosha kwani wametupwa nje kwa Jumla ya Bao 5-4 kwa Mechi 2.
Hii ni mara ya 3 mfululizo kwa Juve kutinga Fainali ya COPPA ITALIA huku pia wakielekea kutwaa Ubingwa wa Serie A na pia wapo Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambako Wiki ijayo watacheza na Barcelona.
Juzi Lazio walifungwa 3-2 na AS Roma lakini wapo Fainali baada ya kushinda Mechi ya Kwanza 2-0 na hivyo kufuzu kwa Jumla ya Mabao 4-3.
Hii itakuwa mara ya 3 katika Miaka 5 kwa Lazio kutinga Fainali baada 2013 kuibwaga AS Roma na kubeba Kombe na 2015 kufungwa na Juve.

SERIE A: MABINGWA, VINARA JUVE WABANWA NA NAPOLI, JUVE 6 MBELE!

Khedira-1704-Nap-celeb-epa 0Jana Usiku Mabingwa wa Italy na ambao ndio Vinara wa Serie A Juventus walitoka Sare 1-1 Ugenini na Timu ya 3 Napoli.
Kwenye Mechi iliyochezwa Stadio San Paolo Juve walitangulia kufunga kwa Bao la Sami Khedira aliepachika Dakika ya 7 tu na Wenyeji Napoli kurudisha Dakika ya 60 Mfungaji akiwa Marek Hamsik.
Matokeo haya pamoja na AS Roma kumfunga Empoli yamefanya uongozi wa Juve kwenye Serie A uwe Pointi 6 mbele ya Roma
VIKOSI:
Napoli: Rafael; Hysaj, Albiol, Koulibaly, Strinic (Ghoulam 79); Allan (Zielinski 68), Jorginho, Hamsik (Rog 76); Callejon, Mertens, Insigne
Juventus: Buffon; Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Asamoah; Khedira, Marchisio (Dybala 79); Lemina (Cuadrado 61), Pjanic (Rincon 86), Mandzukic; Higuain
REFA: Orsato
 
 

UEFA YATOA LISTI YA NCHI BORA INAYOAMUA UWAKILISHI ULAYA KWA KLABU!

UCL-16-17-SITSpain, Germany, England na Italy zimethibitishwa kuwa ndio Nchi Wanachama wa Juu kabisa katika Listi ya Ubora ya UEFA huku France na Russia zikishika Nafasi za 5 na 6.

Uthibitisho huo ndio utaamua Nchi zipi zinaingiza Timu ngapi kwenye UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, kuanzia Msimu wa 2018/19 wakati ule wa 2017/18 ukibaki vile vile kama sasa kwa vile uliamuliwa kwa Takwimu za kuanzia Misimu ya 2012/13 hadi 2016/17.

Uthibitisho huu wa sasa unazihakikishia Spain, Germany, England na Italy kuwa na Timu 4 kila moja kwenye UCL kwenye Makundi kuanzia Mwaka 2018 wakati zile za Nafasi za 5 na 6, ambazo ni France na Russia, zitakuwa na Klabu 2 kwenye Makundi na ya 3 ikianzia Raundi ya Mchujo.

Nchi za kuanzia Nafasi za 7 hadi 10 zitapata Nafasi 1 ya Makundi na moja itaanzia Raundi ya Mchujo.

Nchi ambazo zipo Nafasi hizo ni Portugal, Ukraine, Belgium na Turkey.

Czech Republic na Switzerland, ambazo ziko Nafasi za 11 na 12, Mabingwa wao wataanza Raundi ya Mchujo kwenye UCL lakini zitapa Nafasi Moja kwa Timu zao kucheza kuanzia Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI kama vile Timu 10 za juu zinavyopata.

Kwa upande wa Ubora kwa Klabu, Mabingwa Watetezi wa Ulaya Real Madrid ndio Nambari Wani wakiiongoza Bayern Munich kwa Pointi 10 na zinafuatia Barcelona, Atlético Madrid na Juventus.

MARIO GOTZE: NYOTA HATARINI KUFIFIA, ASAKAMWA NA UGONJWA NADRA!

GOTZEMARIO GOTZE ndie aliwapa Ubingwa wa Dunia Germany huko Brazil alipofunga Bao 1 na pekee walipowabwaga Argentina 1-0 lakini sasa yupo nje ya Uwanja akiugua Ugonjwa ambao umeelezwa ni wa kipekee na nadra kumkumba Binadamu.

Wengi wanakumbuka, Gotze, mwenye Miaka 22, akiunganisha Krosi ya André Schürrle katika Dakika za Nyongeza 30 na kumchambua Kipa wa Argentina Sergio Romero akifunga Bao safi na kuipa Germany Taji kubwa Duniani ndani ya Rio De Janeiro Mwaka 2014.

Kwenye Mechi hiyo, Gotze alitokea Benchi na kuingizwa Uwanjani ngoma ikiwa 0-0 na inadaiwa Kocha wa Germany, Joachim Löw, alimpa morali kabla tu kukanyaga Uwanjani kwa kumwambia: “Onyesha wewe ni Bora kupita Messi!”

Tukio hilo la kuipa ushindi Germany lilimfanya Gotze awe Shujaa wa Germany na wengi kutegemea makubwa zaidi kutoka kwake hapo baadae.

+++++++++++++++++

JE WAJUA:

-Gotze ni Neno la Kijerumani lililobuniwa Karne ya 16 na Martin Luther akitafsiri Bibilia ya Kilatino.

-Lilimaanisha ‘Mungu Feki’.

+++++++++++++++++

Mwishoni mwa Mwezi uliopita, Klabu yake Borussia Dortmund ilitamka kuwa Gotze amegunduliwa na Ugonjwa nadra kumkumba Binadamu unaoathiri Musuli, kumletea uchovu na Mwili kuongezeka Uzito.

Wiki iliyopita, Dortmund ikathibitisha kuwa Nyota huyo hataonekana tena Uwanjani Msimu huu.

Gotze alichomoza kwenye Soka Mwaka 2009 akiwa na Miaka 17 akikichezea Kikosi cha Jurgen Klopp cha Borussia Dortmund na Msimu wa 2010/11 kuitwa kwa mara ya kwanza kuichezea Germany.

Mashaka ya Gotze kwa sasa yameleta wasiwasi mkubwa kwa Mashabiki wa Germany wakihofia huenda Jina ‘Gotze’ ndilo limeleta nuksi kwenye Maisha yake.

ENGLAND: 4 BORA MOJA KUIKOSA CHAMPIONZ LIGI IKIWA LEICESTER, MAN UNITED WATABEBA MAKOMBE ULAYA!

UCL-16-17-SITjavascript:;LEO huko England kumezuka mjadala mkubwa kuhusu 4 Bora ya EPL, Ligi Kuu England, na hatari iliyokuwepo kwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 4 kukosa kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Msimu ujao ikiwa tu Leicester City na Manchester United zitabeba Makombe Ulaya Msimu huu.

Kwa mujibu wa Sheria za UEFA, kila Mwanachama wake anaruhusiwa kuwa na Timu zisizodi 5 kwenye Mashindano ya UCL Msimu wa 2017/18.

Hii inamaanisha kwamba ikiwa Leicester watatwaa UCL Msimu huu na Man United kubeba EUROPA LIGI basi Timu hizo 2 zitacheza UCL pamoja na zile 3 za Juu za EPL wakati ile inayomaliza Nafasi ya 4 kutupwa EUROPA LIGI.

Uwezekano huo unaleta hatari kubwa kwa Tottenham, Man City, Liverpool na Arsenal ambazo zinaweza kukosa kucheza UCL zikimaliza Nafasi ya 4.

Hali kama hii ishawahi kutokea Msimu wa 2012/13 wakati Tottenham walipomaliza Nafasi ya 4 kwenye EPL na kutupwa EUROPA LIGI wakati Chelsea, iliyomaliza Nafasi ya 6 kuchukua Nafasi yao kwa vile tu walibeba Ubingwa wa UCL.

Habari MotoMotoZ