BUNDESLIGA: AUBAMEYANG AIPENYEZA DORTMUND UEFA CHAMPIONZ LIGI NA YEYE KUZOA BUTI YA DHAHABU!

>>LAHM, ALONSO WAAGWA BAYERN!

AUBAMEYANG-DHAHABUSTAA KUTOKA AFRIKA Nchi ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, Jana alifunga Bao 2 wakati Borussia Dortmund inaichapa Werder Bremen 4-3 na kumaliza Bundesliga wakiwa Nafasi ya 3 na hivyo kufuzu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.

Bao la ushindi la Dortmund lilifungwa Dakika ya 89 kwa Penati aliyofunga Aubameyang.

Bao hilo limemfanya Aubameyang awe amefunga Jumla ya Bao 31 kwenye Mechi 32 za Bundesliga huku Bao nyingine 7 akizifunga kwenye Mechi za UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Kwa Msimu wa Bundesliga wa 2016/17, Aubameyang ameshinda Buti ya Dhahabu akiwa ndie Mfungaji Bora akimpiku Robert Lewandowski wa Bayern Munich mwenye Bao 30.

Nao Mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich, walimaliza Msimu kwa kuwachapa 4-1 SC Freiburg na hivyo kuzoa Pointi 82 kwa Mechi 34 wakifuatia RB Leipzig wenye 67 na Dortmund wenye 64.

Timu zote hizo 3 zitaiwakilisha Germany kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Katika Mechi hiyo ya Jana ya mwisho wa Msimu wa Bayern Munich, Klabu hiyo pia ikiwaaga Nahodha wao Philipp Lahm na Mchezaji kutoka Xabi Alonso ambao wameamua kustaafu.

Lahm, mwenye Miaka 33, Jana ilikuwa Gemu yake ya 517 kwa Bayern na alipewa zawadi mwisho wa Gemu hiyo.

 

Wengine waliostaafu Jana na kupewa zawadi ni Xabi Alonso, 35, na Kipa Tom Starke, 36.

BAYERN-ALONSO-LAHM

COPPA ITALIA: JUVE YABEBA KOMBE!

COPPA-ITALIA-2017JANA Mabingwa wa Italy Juventus wamebeba Coppa Italia kwa mara ya 12 ikiwa ni Rekodi kwa kuichapa Lazio 2-0 kwenye Fainali iliyochezwa Stadio Olimpico Jijini Rome huko Nchini Italy.
Kwa kubeba Kombe hili Juve sasa wamekamilisha awamu ya kwanza ya Trebo Msimu huu kwani Wikiendi hii inayokuja wanaweza kutetea vyema Ubingwa wao wa Serie A kwa mara ya 6 mfululizo na hapo Juni 3 wanaweza kutwaa Ubingwavwa UEFA CHAMPIONZ LIGI wakiwafunga Mabingwa Watetezi Real Madrid huko Cardiff, Wales.
Jana Bao za ushindi za Juve zilifungwa na Mabeki wao Dani Alves Dakika ya 12 na Leonardo Bonucci katika Dakika ya 24.
Juve, chini ya Kocha Massimiliano Allegri, wamekuwa Timu ya kwanza kubeba Coppa Italia mara 3 mfululizo.
Kwa Lazio hii ilikuwa ni Fainali yao ya 3 katika Miaka Mitano.
VIKOSI:

Juventus: Neto; Barzagli, Bonucci, Chiellini, Alex Sandro; Marchisio, Rincon; Dani Alves, Dybala (Lemina 78), Mandzukic; Higuain

Lazio: Strakosha; Bastos (Felipe Anderson 52), De Vrij (Luis Alberto 69), Wallace; Basta, Biglia, Parolo (Radu 20), Milinkovic-Savic, Lulic; Immobile, Keita

REFA: Tagliavento

JUVE YADUNDWA, YAKOSA NAFASI KUTWAA UBINGWA MAPEMA!

JUVE-UshindiJuventus imekosa nafasi ya kutwaa Ubingwa wao wa Serie A wa 6 mfululizo mapema kabla Ligi hiyo kuu ya Italy kwisha baada Jana kudundwa Bao 3-1 Ugenini na Timu ya Pili AS Roma.
Hata hivyo, Juve wanabaki kileleni mwa Serie A wakiwa Pointi 4 mbele ya Roma huku Mechi zikibaki 2 na Jumapili ijayo, wakiwa kwao Juventus Stadium Jijini Turin, wana nafasi nyingine ya kuwa Mabingwa ikiwa wataifunga Crotone.
Kabla ya hapo, Jumatano Usiku, wanapambana na SS Lazio kwenye Fainali ya Coppa Italia.
Jana Juve walitangulia kuifunga Roma kupitia Mario Lemina lakini Bao za Daniele de Rossi, Stephan El Shaarawy na Radja Nainggolan ziliipa Roma ushindi wa 3-1 na kuweka hai matumaini yao finyu ya kuwa Mabingwa.
Juve, chini ya Kocha Massimiliano Allegri, wanahitaji Pointi 1 tu ili kutwaa Ubingwa wa Serie A na kuweka Rekodi ya kuwa Timu pekee kutwaa Ubingwa mara 6 mfululizo katika Historia ya Italy.
Lakini pia Juve wanaweza kutwaa Ubingwa Jumamosi hii bila wao kucheza ikiwa tu Roma itafungwa Ugenini na Chievo na Napoli, wakiwa Nyumbani, kushindwa kuifunga Fiorentina.
Kwa wakati huo, Juve, ikiwa Jumatano watatwaa Coppa Italia, watajijua kama wako mbioni kutwaa Trebo Msimu huu kwani pia wanacheza Fainali ya UEFA CHAMPIONZ na Real Madrid hapo Juni 3 huko Cardiff, Wales.

EPL: SANCHEZ, GIROUD WAIWEKA ARSENAL NAFASI YA 5!

SANCHEZ-5BAO 2 za Kipindi cha Pili za Alexis Sanchez na Olivier Giroud zimeipa ushindi Arsenal wa 2-0 walipocheza na Southampton huko Saint Mary Jana Usiku katika Mechi ya EPL, LIGI KUU ENNGLAND.

Ushindi huo umeifanya Arsenal iwe na Pointi 66 wako mbele ya Timu ya 6 Manchester United kwa Pointi 1 huku wao wakiwEPL-MEI11a Pointi 3 nyuma ya Timu ya 4 Man City.

Bao la kwanza la Arsenal lilifungwa Dakika ya 60 baada ya Sanchez kuwahadaa Mabeki Wawili na la pili kupigwa Dakika ya 83 kwa Kichwa cha Giroud alieingizwa muda mfupi tu kabla akitokea Benchi.

EPL itaendelea Ijumaa kwa Mechi 2 ambazo Everton itacheza na Watford na Vinara Chelsea kuwa Ugenini huko The Hawthorns wakihitaji kuifunga tu West Bromwich Albion ili kutwaa Ubingwa wakiwa na Mechi 1 mkononi.

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba/Matokeo:

Jumatano Mei 10

Southampton 0 Arsenal 2           

Ijumaa Mei 12

2145 Everton v Watford              

2200 West Bromwich Albion v Chelsea             

Jumamosi Mei 13

1430 Manchester City v Leicester City             

1700 Bournemouth v Burnley                

1700 Middlesbrough v Southampton     

1700 Sunderland v Swansea City 

1930 Stoke City v Arsenal 

Jumapili Mei 14

1400 Crystal Palace v Hull City    

1615 West Ham United v Liverpool       

1830 Tottenham Hotspur v Manchester United

MOURINHO ASEMA 4 BORA IKO NJE, AIKEBEHI ARSENAL NA WENGER!

MANUNITED-FUATILIA-SITBOSI wa Manchester United Jose Mourinho amekiri kuwa Timu yake kumaliza 4 Bora kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, ni kuwa kitu hakiwezekani baada ya Jana kufungwa 2-0 na Arsenal huku pia akimkejeli Arsene Wenger.Kipugo hicho cha Jana ni cha kwanza kwa Timu inayoongozwa na Wenger kuifunga Timu ya Mourinho katika Mechi 16 zilizodumu Miaka 13.Mourinho ameeleza: "Mashabiki wa Arsenal wamefurahi na mimi nimefurahi kwa ajili yao. Hii ni mara ya kwanza naondoka na wako na furaha. Nlikuwa nkiondoka Highbury wanalia! Nkiondoka Emirates, wanalia!"Aliongeza: "Wanalia wakitembea Mitaani vichwa chini. Ni Klabu kubwa. Unafkiri naskia raha Klabu kubwa kama Arsenal kutoshinda Vikombe? Sisikii raha. Arsene Wenger ni Meneja mkubwa. Kuwa na rekodi ya kutofungwa Mechi nyingi si kawaida!"Kabla ya Mechi hiyo na Arsenal, Mourinho alishakiri nafasi ya Man United kumaliza 4 Bora kwenye EPL ni finyu hivyo njia pekee ni kutilia mkazo kutwaa UEFA EUROPA LIGI ambayo Alhamisi iliyopita waliifunga Celta Vigo 1-0 huko Spain katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali.Alhamisi hii inayokuja Man United itarudiana na Celta Vigo huko Old Trafford.Katika kuonyesha Mechi hii na Arsenal ni kero kwao kwa vile imejichimbia katikati ya Mechi na Celta Vigo, Jana Mourinho alibadili Wachezaji 8 toka Kikosi chake kilichocheza na Vigo na pia kumuanzisha Kinda Tuanzebe na pia Kipindi cha Pili kumuingiza Kinda mwingine, McTominay, Wachezaji ambao hawajawahi kukichezea Kikosi cha Kwanza cha Man United.Licha ya kushusha Kikosi hicho, Mourinho amekiri hawakustahili kufungwa na Arsenal kwani waliidhibiti Mechi hiyo.Kuhusu kumaliza 4 Bora Mourinho ameeleza: "Haiwezekani. Sidhani hao wanaocheza Mechi 1 kwa Wiki watafungwa. Kwa sababu Alhamisi tutacheza kufa na kupona kwenye EUROPA hatuwezi Jumapili kwenda Tottenham tukiwa imara kila kitu. Hivyo 4 Bora hatuna nafasi. Tuikimbize nafasi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kujaribu kutwaa EUROPA LIGI!"Kwa Arsenal, ushindi wao umewaongezea matumaini kwani wana Mechi mkononi.
Hadi sasa Chelsea inaongoza Ligi ikiwa na Pointi 81 kwa Mechi 34 wakifuata Tottenham wenye Pointi 77 kwa Mechi 35, Liverpool ni wa 3 na wana Pointi 70 kwa Mechi 36, kisha Man City waliocheza Mechi 35 na wana Pointi 65.
Man United wamecheza Mechi 35 na wana Pointi 65 wakishika Nafasi ya 5 wakifuata Arsenal waliocheza Mechi 34 na wana Pointi 63.
EPL, LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
Jumatatu Mei 8
2200 Chelsea v Middlesbrough
Jumatano Mei 10
2145 Southampton v Arsenal               
Ijumaa Mei 12
2145 Everton v Watford              
2200 West Bromwich Albion v Chelsea    
Jumamosi Mei 13
1430 Manchester City v Leicester City             
1700 Bournemouth v Burnley                
1700 Middlesbrough v Southampton     
1700 Sunderland v Swansea City 
1930 Stoke City v Arsenal 
Jumapili Mei 14
1400 Crystal Palace v Hull City    
1615 West Ham United v Liverpool       
1830 Tottenham Hotspur v Manchester United