JUVENTUS STADIUM KUBATIZWA ALLIANZ STADIUM!

JUVE-STADIUM-ALLIANZMABINGWA wa Italy Juventus wamesaini Mkataba wa kubadili jina la Uwanja wao ambao sasa utaitwa Allianz Stadium kuanzia Julai Mosi.

Juve wamesaini Mkataba huo wa kubadili Jina la Uwanja kutoka Juventus Stadium ulioko Jijini Turin, Italy na Jina kuwa Allianz Stadium litadumu hadi 2023.

Mkataba huo umesainiwa na Kampuni ya Bima ya Kimataifa ya Allianz pamoja na Lagardere Sports wanaomiliki Majina ya Viwanja.

Kampuni ya Allianz pia inadhamini Viwanja vingine vikubwa sehemu nyingi Duniani ikiwa pamoja na cha Mabingwa wa Germany Bayern Munich kilichopo Jijini Munich, Germany kinachoitwa Allianz Arena na kile cha Klabu ya France, Nice, kiitwacho Allianz Riviera.

Uwanja huu wa Juventus ulifunguliwa rasmi Septemba 8 Mwaka 2011 na unapakia Watazamaji 41,507.

Juve ndio Mabingwa wa Italy kwa Misimu 6 mfululizo na pia Msimu huu wametwaa Coppa Italia na Jumamosi hii wanasaka Trebo kwani watacheza Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Mabingwa Watetezi Real Madrid huko Cardiff, Wales.

UEFA CHAMPIONZ LIGI - FAINALI - REAL v JUVE: BALE APOTEZA MATUMAINI, ISCO KUANZA?

UEFA CHAMPIONZ LIGI - FAINALI
Jumamosi Juni 3 Saa 3 Dak 45 Usiku
Millenium Stadium, Cardiff, Wales
Real Madrid v Juventus
××××××××××××××××××××××
REAL-BALEJUMAMOSI hii huko Millenium Stadium, Cardiff, Wales ndiko Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, itachezwa kati ya Mabingwa Watetezi Real Madrid na Juventus.
Timu hizi zote zimemaliza Ligi zao kwa kutwaa Ubingwa wa Nchi zao lakini Real wanatinga Fainali hii wakitaka kutetea Taji lao la UCL na kuweka Rekodi ya kuwa Timu ya Kwanza kutenda hilo.
Kila Timu hivi sasa ipo kwenye maandalizi makali na huko Spain umezuka mjadala mkali kuhusu nani aanze Mechi hii kubwa kati ya Gareth Bale na Isco wa Real Madrid.
Kikawaida Bale ndie chaguo la kwanza la Kocha Zinedine Zidane na Bale akicheza Mechi hii italeta shamrashamra kubwa humo Millenium Stadium kwani humo ni Mtoto wa Nyumbani Cardiff ukiwa ndio Mji aliozaliwa.
Lakini tatizo kubwa ni kuwa Bale alikuwa Majeruhi ingawa sasa yupo Mazoezini kama kawaida na wenzake.
Mwenyewe Bale amekiri kwamba ingawa yuko fiti itakuwa ngumu kwake kuanza Fainali hii na matumaini ni kuwa ataingizwa toka Benchi.
Bale aliumia Enka yake Mwezi Novemba kwenye Mechi ya UCL dhidi ya Sporting Lisbon na kuwa nje kwa Siku 88 na kurejea Uwanjani Siku Real inacheza na Espanyol.
Pia alianza Mechi na Barcelona hapo Aprili 23 na kutoka nje Kipindi cha Kwanza akiwa na maumivu ya Enka na tangu wakati huo hajacheza tena.
Kukosekana kwa Bale ndiko kulimpa nafasi Isco kung'ara Uwanjani.
Hata hivyo, Bale amesema ni juu ya Zidane kuamua nani amwanzishe na ikiwa ni yeye yuko tayari kutimiza ndoto yake kucheza Fainali kubwa ya Ulaya Nyumbani kwao
 

DFB-POKAL: AUBAMEYANG AIPA KOMBE BVB!

AUBAMEYANG-DHAHABUPENATI ya Dakika ya 67 ya Pierre-Emerick Aubameyang imewapa DFB-POKAL, Kombe la Germany, Borussia Dortmund BvB walipoifunga Eintracht Frankfurt 2-1 kwenye Fainali iliyochezwavJana huko Olympiastadion Jijini Berlin.
Dortmund walifunga Bao la Kwanza Dakika ya 8 Mfungaji wao akiwa Ousmane Dembele.
Eintracht Frankfurt walisawazisha Dakika ya 29 kupitia Ante Rabic na nusura Haris Seferovic awape Bao la Pili baada kupiga Posti.
Hadi Haftaimu Bao zilibaki 1-1.
Kipindi cha Pili Dakika ya 67 BvB walipewa Penati baada ya Christian Pulisic kuangushwa na Aubameyang akafunga Penati hiyo likiwa Bao lake la 40 Msimu huu na kuwapa Dortmund ushindi wa 2-1 na kuwapa Kombe.
Kutwaa DFB-POKAL kumewapa furaha kubwa Dortmund ambao wamekuwa wakipigwa katika Fainali 3 mfululizo zilizopita.
 

MOURINHO, ‘THE MANCHESTER ONE’, BORA KUCHEZA UEFA CHAMPIONZ LIGI NJIA HII KULIKO KUMALIZA NAFASI YA 4, 3 AU 2!

>’SASA TUMETWAA KILA KOMBE DUNIANI!’

MANUNITED-MABINGWA-EUROPALIGIMENEJA wa MABINGWA WA ULAYA wa EUROPA LIGI, Jose Mourinho, amesema Ubingwa huo unastahili kwao hasa baada ya kubatizwa ‘Timu mbovu Duniani’ mara kadhaa kwenye Msimu huu.

Jana, Bao za Paul Pogba na Henrikh Mkhitaryan ziliwapa Man United ushindi wa 2-0 dhidi ya Ajax Amsterdam kwenye Fainali ya UEFA EUROPA LIGI na kubeba Kombe ambalo Man United walikuwa hawajawahi kulitwaa Ulaya licha kubeba mengine yote.

Kwenye Msimu wa Kwanza akiwa na Man United, Timu hii ya Mourinho ilimaliza EPL, LIGI KUU ENGLAND, ikiwa Nafasi ya 6 lakini kwa kuzoa Kombe la UEFA EUROPA LIGI Man United sasa watacheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao wakianzia Makundi.

Kwa mujibu wa Mourinho, ambae pia Msimu huu walibeba Ngao ya Jamii na EFL CUP, Msimu huu ulikuwa ni mafanikio.MANUNITED-MOU-SON

×××××××

JE WAJUA?

-Jose Mourinho ameshinda Fainali zote 4 za Ulaya alizotinga kama Meneja akitwaa UEFA CUP 2003 na UEFA CHAMPIONZ LIGI 2004 akiwa na FC Porto, na UEFA CHAMPIONZ LIGI 2010 akiwa na Inter Milan.

-Mourinho amedumisha Rekodi yake ya 100% ya ushindi dhidi ya Ajax katika Mechi zote 7 alizocheza nao.

×××××××

Ameeleza: “Ni mwisho wa Msimu mgumu. Lakini ni Msimu mzuri mno!”

Aliongeza: “Tulipendelea kufuzu UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa njia hii kupita ile ya kumaliza Nafasi ya 4, 3 au 2! Tumetimiza lengo kwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Ulaya, Taji muhimu. Sasa Klabu ina kila Taji Duniani!”

Mourinho alieleza: “Sasa tuna heshima ya kucheza UEFA SUPER CUP na Bingwa Mpya wa UEFA CHAMPIONZ LIGI, kwa hiyo Msimu huu ulikuwa mzuri mno!”

×××××××

JE WAJUA?

-MAN UNITED wamejumuika na Ajax, Bayern Munich, Chelsea na Juventus kuwa Klabu pekee zilizonyakua Makombe yote ya UEFA huko Ulaya.

-Vikombe hivyo ni UEFA CHAMPIONZ LIGI, UEFA Cup Winners' Cup, UEFA Cup/UEFA EUROPA LIGI

×××××××

Nae Mchezaji wa zamani wa Man United na Kepteni wa England, David Beckham, amesema Usiku wa Jana ulikuwa muhimu kuliko Michezo na ulikuwa Usiku mkubwa kwa Man United lakini mkubwa sana kwa Jiji la Manchester na Nchi yao.

Maneno ya Beckham yalilenga kuomboleza Msiba mkubwa uliolikumba Jiji la Manchester baada ya Mlipuko wa Bomu ulioua Watu 22 kwenye Ukumbi wa Muziki Siku 2 kabla Fainali hii ya UEFA EUROPA LIGI.

Ander Herrera, aliezoa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Fainali hiyo, amesema ushindi wao wa Man United ni kwa ajili ya Wahanga wa Shambulizi la Bomu.

Alinena: “Hii ni Soka tu lakini kilichotokea Siku 2 zilizopita ni kibaya mno! Tunataka Amani Duniani, Dunia ya kawaida ya heshima!”

UEFA EUROPA LIGI FAINALI - JUMATANO: AJAX v MAN UNITED, PATA DONDOO MUHIMU!

FRIENDS ARENA Mjini Stockholm Nchini Sweden kesho ndio Dimba la Fainali ya UEFA EUROPA LIGI kati ya Klabu ya Netherlands Ajax Amsterdam na Manchester United ya England.
UEL-FINALMbali ya kuwania Kombe pia Mshindi wa Fainali hii atatinga moja kwa moja Hatua ya Makundi ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, na hilo ni muhimu mno kwa Man United kuliko Ajax kwani wao wamekosa nafasi hiyo baada ya kumaliza Nafasi ya 6 kwenye EPL, Ligi Kuu England, wakati Ajax wao wamepata Nafasi ya kucheza UCL kwa kumaliza Nafasi ya Pili kwenye Ligi ya kwao.
Hapo Kesho Ajax watakuwa wakiwania kutwaa Kombe la Ulaya kwa mara ya kwanza baada Miaka 22 wakati Man United wanalitaka Kombe pekee la Ulaya ambalo hawajawahi kulitwaa baada kutwaa mengine yote yaliyobakia.
Hii itakuwa ni mara ya 5 kwa Ajax na Man United kupambana kwenye Mashindano Barani Ulaya na kila Timu kushinda mara 2 ingawa mara zote hizo Man United kuibuka kidedea katika Mechi 2.
Mara ya kwanza Timu hizi zilikutana kwenye UEFA CUP Msimu wa 1976/77 na Ajax kushinda 1-0 Mechi ya kwanza huko kwao lakini Man United ikashinda 2-0 huko Old Trafford na kuibwaga Ajax.
Mara ya Pili ni Msimu wa 2012/13 kwenye UEFA EUROPA LIGI Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ambayo Man United walishinda 2-0 huko Amsterdam kwa Bao za Ashley Young na Javier Hernández 'Chicharito' na Mechi ya Pili huko Old Trafford Ajax walishinda 2-1 na kutupwa nje ya Mashindano kwa Jumla ya Mabao 3-2.
×××××××
JE WAJUA?

-MAN UNITED wanasaka kujumuika na Ajax, Bayern Munich, Chelsea na Juventus kwa kuwa Klabu pekee zilizonyakua Makombe yote ya UEFA huko Ulaya.
-Vikombe hivyo ni UEFA CHAMPIONZ LIGI, UEFA Cup Winners' Cup, UEFA Cup/UEFA EUROPA LIGI
×××××××
Ajax, chini ya Kocha Peter Bosz, wanasaka kutwaa Kombe lao la kwanza tangu Bosi huyo atue hapo Mwezi Mei Mwaka Jana. 
Nae Jose Mourinho, alianza kazi Man United mwanzoni mwa Msimu huu na tayari ashatia Kabatini Ngao ya Jamii na EFL CUP huko England na sasa analitaka Kombe hili ili Msimu ujao atinge UEFA CHAMPIONZ LIGI baada kumaliza Nafasi ya 6 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND.
Hali za Timu
Ajax ni Timu inayocheza kwa kushambulia kwa haraka kwa mfumo wa kaunta ataki na Msimu huu kwenye Mashindano haya wamefunga Bao 24 wakati Man United wamepachika 23 katika Mechi 14.
Ajax, kikawaida, hutumia Mfumo wa 4-3-3 na Mtu 3 zao za Fowadi ni Kasper Dolberg, Bertrand Traore, ambae ni wa Mkopo kutoka Chelsea, na Amin Younes huku Fowadi wa Miaka 17, Justin Kluivert, Mwana wa Lejendari Patrick Kluivert, mar kwa mara akiingizwa kuongeza nguvu kwenye Wingi.
Kwa Man United, kumkosa Mkongwe Zlatan Ibrahimovic ambae ameumia na aliepiga Bao 5 kwenye Mashindano haya ni pigo lakini yupo Kinda Marcus Rashford ambae ni moto.
Pia kumkosa Ibrahimovic kunaweza kumfanya Jose Mourinho akabadili Mfumo kutoka ule wa jawaida yao wa 4-2-3-1.
Nguvu kubwa ya Ajax ipo kwenye Kiungo chao na hasa Davy Klassen na Lasse Schone na endapo Ander Herrera na Paul Pogba wataibuka juu yao, Difensi ya Ajax, hasa Masentahafu Davinson Sanchez na Nick Viergever, si imara kiasi hicho kwani huwa mchecheto kwenye presha na wao na Kipa wao Onana hufanya makosa mengi kwenye hali hiyo.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
AJAX: Onana; Tete, De Ligt, Sanchez, Veltman; Klaassen, Schone, Ziyech; Traore, Dolberg, Younes
MAN UNITED: Romero; Valencia, Blind, Jones, Darmian; Herrera, Fellaini, Pogba; Lingard, Rashford, Mkhitaryan
REFA: Damir Skomina (Slovenia)
 
 
 
 

Habari MotoMotoZ