CHELSEA ‘MWENDOKASI’ KUWANASA ALEX SANDRO, TIEMOUÉ BAKAYOKO KUMPOZA ‘MBOGO’ CONTE!

CHELSEA CONTE BORAMABINGWA WA ENGLAND Chelsea wanatarajiwa Wiki hii kuongeza kasi ya kuwanasa Alex Sandro wa Juventus na Tiemoué Bakayoko wa AS Monaco ili kumtuliza Meneja Antonio Conte ambae amepandwa na hasira kwa kutonunuliwa Mchezaji yeyote Mpya katika Walengwa wa Listi yake.

Conte, ambae yuko Vakesheni huko kwao Italy, alichukizwa na kutokuwepo na jitihada zozote na kukazuka habari ataondoka Chelsea kitu ambacho Klabu hiyo imekikana.

Inadaiwa Chelsea ilimtaka Conte auze baadhi ya Wachezaji waliokuwepo ilia pate Wapya na hilo likamsukuma kumtumia SMS Diego Costa kuwa hayumo kwenye mipango ya Chelsea na kumfanya Fowadi huyo alipue taarifa hiyo hadharani na kuibua msuguano mwingine kati ya Conte na Uongozi wa Chelsea.

Pengine hilo la kuondoka kwa Costa ndilo limewafanya Everton, wakijua wazi Chelsea wanamtaka Straika wao Romelu Lukaku, kudai Dau la Rekodi ya Dunia kumnunua Fowadi huyo wa Belgium alieazimwa toka Chelsea na kisha kuuzwa moja kwa moja kwa Bei chee.

+++++++++++++

Chelsea – Uhamisho wa Wachezaji Kipindi hiki:

Ndani

Hamna

Nje

Juan Cuadrado (Juventus) Ada Haikutajwa

Christian Atsu (Newcastle United) Ada Haikutajwa

Asmir Begovic (AFC Bournemouth) Ada Haikutajwa

Dominic Solanke (Liverpool) Uhamisho wa Bure

Alex Kiwomya (Doncaster Rovers) Ada Haikutajwa

+++++++++++++

Kuhusu Alex Sandro, Meneja Mkuu wa Juventus, Beppe Marotta, ametoboa Ofa ya kwanza ya Chelsea imekataliwa na sasa Chelsea wanategemewa kurudi na Dau la Pauni Milioni 55.

Sandro, alieichezea Brazil Mechi 7, alianzia huko Ureno akiwa na FC Porto na Antonio Conte anamthamini kuwa ni bora kupita Winga-Beki wao wa Kushoto Marcos Alonso.

Pia, Chelsea wameongeza juhudi za kumnasa Kiungo Tiemoué Bakayoko wa AS Monaco anaechezea Timu ya Taifa ya France ambae Dau lake linakadiriwa kuwa zaidi ya Pauni Milioni 40.

Wadau wanahisi ujio wa Bakayoko huenda ukafungua kuuzwa kwa Nemanja Matic.

Vile vile, Chelsea wanatarajiwa kumsaini kama Mchezaji Huru Kipa Willy Caballero aliemaliza Mkataba na Manchester City ili awe Msaidizi wa Kipa Nambari Wani Thibaut Courtois baada ya Kipa Rizevu Asmir Begovi kuuzwa kwa Bournemouth.

 

Habari MotoMotoZ