KUMBEEE: CONTE ACHUKIZWA BAADA CHELSEA KUMWAMBIA ‘UZA WACHEZAJI UNUNUE WAPYA’!

>NDIO MAANA COSTA AKAWASHWA SMS ‘SIKUTAKI’!

MGONGANA wa Meneja Antonio Contena Klabu yake Chelsea kumbe ulianza baada ya kuambiwa hawezi kupata Wachezaji Wapya bila kuuza baadhi ya waliokuwepo.

CHELSEA-CONTE-BORAHivi karibuni iliripotiwa kuwa Conte anataka kuondoka Chelsea kabla Msimu Mpya haujaanza kitu ambacho Chelsea ilikikanusha.

Sasa Magazeti huko England yamebaini kuwa yale aliyotoboa Straika wa Chelsea Diego Costa kuwa alitumiwa Ujumbe wa Simu na Conte na kuambiwa hayupo kwenye mipango yake kwa Msimu ujao, na hivyo hahitajika, yametokana na kuamriwa Conte na Klabu kuwa ‘Uza, Ununue’!

Duru za England zimebaini kuwa Conte amewaambia baadhi ya Marafiki zake huko kwao Italy kuwa amekasirishwa na amri hiyo ya kujitafutia Fedha mwenyewe za kununua Wachezaji Wapya kwa kuuza hao waliomsaidia kutwaa Ubingwa katika Msimu wake wa kwanza tu.

Hali hii imedaiwa kumfanya Conte atafakari kubwaga manyanga kwani tayari alishatoa Listi kwa Uongozi wa Chelsea nani anawataka kuimarisha Kikosi chake.

Inasemekana Conte alikabidhi Listi yenye Majina ya Straika wa Everton Romelu Lukaku, Kiungo wa AS Monaco Tiemoue Bakayoko, Sentahafu wa Bayern Munich Jerome Boateng na Fulbeki wa Kushoto wa Juventus Alex Sandro na wote kwa ujumla wangegharimu Pauni Milioni 200.

Inadaiwa Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich, hayupo tayari kumwaga Donge lote hilo na hiyo ndio imesababisha Chelsea kutonunua Mchezaji Mpya hadi sasa.

Hilo limemchukiza mno Conte na hasa akicheki Wapinzani Wakuu wake, kama vile Man City na Man United, wakiwa tayari wamejikita Sokoni kwa kishindo.

Pep Guardiola na Man City tayari washawachukuwa Kiungo wa AS Monaco Bernardo Silva kwa Pauni Milioni 43 na Pauni Milioni 35 kumnunua Kipa wa Benfica kutoka Brazil, Ederson.

Jose Mourinho na Man United tayari washamzoa Beki wa Kimataifa wa Sweden Victor Lindelof kutoka Benfica na wanakaribia kuwanasa Straika wa Real Madrid Alvaro Morata na Fowadi wa Inter Milan Ivan Perisic.

 

Habari MotoMotoZ