UEFA YABUNI TUZO 5 MPYA ZA WACHEZAJI BORA WA MWAKA, WASHINDI AGOSTI 24!

>TOTTI ATUNUKIWA TUZO YA RAIS WA UEFA!

UEFA imetangaza kuanza kutolewa kwa Tuzo za Wachezaji Bora wa Mwaka 5 Mpya kuanzia Agosti hii ambazo Washindi wake watapatikana toka Kura za Makocha na Wanahabari.

UEFA-GRIMALDI-FORUMTuzo hizo zitakabidhiwa huko Monaco hapo Agosti 24 wakati wa Droo ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Tuzo hizo 5 Mpya ni kwa Wachezaji waliofanya vyema kwenye Mashindano ya Klabu ya UEFA kwa Msimu uliopita, yaani ule wa 2016/17, na zitatoka sambamba na zile za sasa za Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Wanaume na Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Kinamama.

Tuzo hizo 5 Mpya ni:

-UEFA CHAMPIONZ LIGI:

-Kipa Bora

-Beki Bora

-Kiungo Bora

-Fowadi Bora

**Hizi zitatolewa Agosti 24

-UEFA EUROPA LIGI:

-Mchezaji Bora wa UEFA Europa Ligi kwa Msimu wa 2016/17.

Kura Kupata Washindi zitakavyopigwa:

Wapiga Kura za Washindi wa Tuzo ni Makocha wa zile Klabu zilizocheza Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na UEFA EUROPA LIGI kwa Msimu wa 2016/17 wakijumuika na Wanahabari 55 kutoka European Sports Media (ESM) kila Mmoja akiwakilisha Nchi Moja Wanachama wa UEFA.

Makocha hawaruhusiwi kumpigia Mchezaji kutoka Timu yake.

Wagombea watakaofika Fainali:

Wagombea wa Tuzo 5 Mpya ambao watatinga Fainali watatangazwa Agosti 4.

Wagombea wa Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Wanaume na Kinamama, Watatu Watatu kila Kundi, watatangazwa Agosti 15.

Tuzo ya Rais wa UEFA:

Tuzo ya Rais wa UEFA kwa Mwaka 2017 imeenda kwa Mchezaji wa Italy Francesco Totti kwa Uchezaji wake uliotukuka katika Maisha yake ya Soka ambapo ameamua kustaafu hivi karibuni.

Totti atakabidhiwa Tuzo yake Agosti 24.

 

Habari MotoMotoZ