KOMBE LA DUNIA 2018 – MBIO ZA RUSSIA: ITALY, SPAIN ZASHINDA, ZAFUKUZANA KUNDI G!

KOMBE LA DUNIA 2018 – MAKUNDI ULAYA

Matokeo:

Jumapili Juni 11

WC-RUSSIA2018-LOGO-1Moldova 2 Georgia 2 [Kundi D]

Finland 1 Ukraine 2 [Kundi I]

Ireland 1 Austria 1 [Kundi D]

Israel 0 Albania 3 [Kundi G]

Iceland 1 Croatia 0 [Kundi I]

Macedonia 1 Spain 2 [Kundi G]

Italy 5 Liechtenstein 0 [Kundi G]

Serbia 1 Wales 1 Kundi D]

Kosovo 1 Turkey 4 [Kundi I]

++++++++

Vita ya nani ataongoza Kundi G la Nchi za Ulaya kusaka kutinga Fainali za Kombe la Dunia la 2018 zitakazochezwa huko Russia imeendelea hapo Jana baada ya Spain na Italy kushinda Mechi zao za Jana.

Spain, ambao wamefungana kwa Pointi na Italy, Jana walishinda Ugenini 2-1 dhidi ya Macedonia kwa Bao za Dakika za 15 na 27 za David Silva na Diego Costa wakati lile la Macedonia kufungwa Dakika ya 66 na Stefan Ristovski.

Italy, wakiwa Nyumbani, waliichakaza Liechtenstein 5-0 kwa Mabao ya  Dakika za 35, 52, 74, 83 na 90 ya  Lorenzo Insigne, Andrea Belotti, Eder Citadin Martins, Federico Bernardeschi na Manolo Gabbiadini.

++++++++

JE WAJUA?

-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia

-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia

-Washindi wa Pili 8 Bora toka Makundi hayo 9 watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia

++++++++

Mechi nyingine za Makundi ya Nchi za Ulaya zitachezwa Agosti 31.

MSIMAMO:

WC-EURO-TEBO-JUN12

Habari MotoMotoZ