KOMBE LA DUNIA 2018 – MBIO ZA RUSSIA: ENGLAND YACHOMOA MWISHONI KWA SCOTLAND!

KOMBE LA DUNIA 2018 – MAKUNDI ULAYA

Matokeo:

Jumamosi Juni 10         

Slovenia 2 Malta 0 [Kundi F]

Scotland 2 England 0 [Kundi F]

Azerbaijan 0 Northern Ireland 1 [Kundi C]

Kazakstan 1 Denmark 3 [Kundi E]

Norway 1 Czech Republic 1 [Kundi C]

Poland 3 Romania 1 [Kundi E]

Germany 7 San Marino 0 [Kundi C]

Lithuania 1 Slovakia 2 [Kundi F]

Montenegro 4 Armenia 1 [Kundi E]

++++++++

WC-RUSSIA2018-LOGO-FBEngland Jana ilinusurika kipigo kutoka kwa Mahasimu wao Scotland na kutoka Sare 2-2 katika Mechi ya Kundi F la Nchi za Ulaya kusaka kutinga Fainali za Kombe la Dunia la 2018 zitakazochezwa huko Russia.

Katika Mechi hiyo iliyochezwa huko hampden Park, Scotland, England walitangulia kufunga Dakika ya 70 kwa Bao la Alex Oxlade-Chamberlain na Scotland kusawazisha Dakika ya 87 na kwenda mbele 2-1 Dakika ya 90 kwa Frikiki za Leigh Griffiths.

Lakini Harry Kane, Nahodha wa England, aliinusuru Nchi yake kwa kufunga Bao la kusawazisha katika Dakika ya 93 na kuambua Sare ya 2-2.

Matoke ohayo bado yanaiweka England kwenye uongozi wa Kundi F wakiwa na Pointi 14 wakifuata Slovakia wenye 12, Slovenia 11, Scotland 8, Lithuania 6 na Malta hawana Pointi.

++++++++

JE WAJUA?

-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia

-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia

-Washindi wa Pili 8 Bora toka Makundi hayo 9 watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia

++++++++

KOMBE LA DUNIA 2018 – MAKUNDI ULAYA

MSIMAMO:

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumapili Juni 11

19:00 Moldova v Georgia [Kundi D]

19:00 Finland v Ukraine [Kundi I]

19:00 Ireland v Austria [Kundi D]

21:45 Israel v Albania [Kundi G]

21:45 Iceland v Croatia [Kundi I]

21:45 Macedonia v Spain [Kundi G]

21:45 Italy v Liechtenstein [Kundi G]

21:45 Serbia v Wales Kundi D]

21:45 Kosovo v Turkey [Kundi I]

Habari MotoMotoZ