UEFA CHAMPIONZ LIGI: BAYERN YAIFUMUA 5 ARSENAL!

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

Mechi za Kwanza

Jumanne 14 Februari 2017

Benfica 1 Borussia Dortmund 0                 

Paris Saint Germain 4 Barcelona 0                

Jumatano 15 Februari 2017

Bayern Munich 5 Arsenal 1                 

Real Madrid 3 Napoli 1              

+++++++++++++++++++++++++

BAYERN5ARSENAL1BAYERN MUNICH wameishushia Arsenal kisago cha Bao 5-1 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, iliyochezwa huko Allianz Arena Jijini Munich Nchini Germany.

Hadi Mapumziko Timu hizi zilikuwa Sare 1-1 baada ya Arjen Robben kutangulia kuifungia Bayern na Arsenal kusawazisha baada ya Alexis Sanchez kupiga Penati iliyookolewa na Kipa Neuer na kumrudia tena na kufunga.

Lakini Kipindi cha Pili, ndani ya Dakika 20, Bayern walifunga Bao 3 za chapchap kupitia Robert Lewandowski na Thiago Alcantara, na kuongoza 4-1.

Dakika ya 88, Thomas Muller akaipa Bayern bao lao la 5 na kupata ushindi mnono wa 5-1 kwa kuisambaratisha Timu ya Arsene Wenger.

++++++++++++++

MAGOLI:

Bayern Munich 5

Arjen Robben 11

Robert Lewandowski 53

Alcantara Thiago 56

Alcantara Thiago 64

Thomas Muller 88

Arsenal 1

Alexis Sanchez 30

++++++++++++++

Timu hizi zirarudiana huko Emirates Jijini London hapo Machi 7.

VIKOSI:

Bayern Munich:Neuer, Lahm, Javi Martinez, Hummels, Alaba, Alonso, Thiago, Vidal, Robben, Douglas Costa, Lewandowski.

Akiba:Ulreich, Rafinha, Bernat, Muller, Coman, Kimmich, Renato Sanches.

Arsenal:Ospina, Bellerin, Mustafi, Koscielny, Gibbs, Coquelin, Xhaka, Iwobi, Ozil, Oxlade-Chamberlain, Sanchez.

Akiba:Cech, Gabriel, Giroud, Walcott, Monreal, Welbeck, Elneny.

REFA: Milorad Mazic (Serbia)

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo

Mechi za Kwanza

Jumanne 21 Februari 2017

Bayer 04 Leverkusen v Atlético Madrid              

Manchester City v Monaco               

Jumatano 22 Februari 2017

FC Porto v Juventus               

Sevilla v Leicester City           

Mechi za Pili

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza

Jumanne 7 Machi 2017

Arsenal v Bayern Munich [1-5]         

Napoli v Real Madrid [1-3]               

Jumatano 8 Machi 2017

Barcelona v Paris Saint Germain [0-4]                

Borussia Dortmund v Benfica [0-1]           

Jumanne 14 Machi 2017

Juventus v FC Porto               

Leicester City v Sevilla           

Jumatano 15 Machi 2017

Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen              

Monaco v Manchester City              

++++++++++++++++++++++++++++

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MTOANO:

14/15 na 21/22 Feb 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza

7/8 na 14/15 Machi 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Pili

11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza

18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)