UCL: LEO ARSENAL 'KUCHOMOKA' MIKONONI MWA BAYERN HUKO ALLIANZ ARENA?

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

Ratiba/Matokeo:

Mechi za Kwanza

Jumanne 14 Februari 2017

Benfica 1 Borussia Dortmund 0      

Paris Saint Germain 4 Barcelona 0          

Jumatano 15 Februari 2017

Bayern Munich v Arsenal                

Real Madrid v Napoli              

+++++++++++++++++++++++++

UCL-16-17-SITLEO Arsenal wako Ugenini huko Allianz Arena Jijini Munich Nchini Germany kucheza na Vigogo wa huko Bayern Munich ikiwa ni Mechi ya Kwanza kati yao ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Arsenal wanatarajiwa kumtumia Kipa wao kutoka Colombia David Ospina, mwenye Miaka 28, badala ya Petr Cech kama walivyofanya Hatua ya Makundi ambayo Kipa huyo aliruhusu Bao 6 katika Mechi zote 6 za Kundi lao.

Kwenye Mechi hii, Arsenal watamkosa Fowadi wao Lucas Perez alieumia Musuli za Pajani na pia zipo ripoti Kiungo wao kutoka Germany, Mesut Ozil, huenda akapigwa Benchi kutokana na kutokuwa kiwango katika Mechi za hivi karibuni.

Ozil hajaifungia Arsenal Bao tangu Desemba 10.

Kwa upande wa Bayern, Mchezaji pekee ambae kuna wasiwasi kucheza ni Kiungo wao kutoka Spain Xabi Alonso ambae ana maumivu ya Goti.

Tangu 2005, hii itakuwa ni mara ya 4 kwa Bayern na Arsenal kukutana katika hatua hii ya Mashindano haya na mara zote 3 za nyuma Bayern kusonga na kuitupa nje Arsenal.

=====

Uso kwa Uso:

UCL: Mara 10

Bayern Munich ushindi: 5Arsenal ushindi: 3

Magoli: Bayern 17 Arsenal 11

=====

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

Arsenal: Ospina; Bellerin, Koscielny, Mustafi, Monreal; Coquelin, Xhaka; Oxlade-Chamberlain, Ozil, Walcott; Sanchez.

Bayern Munich: Neuer; Alaba, Hummels, Javi Martinez, Lahm; Vidal, Alonso, Kimmich; Thiago, Muller; Lewandowski.

REFA: Milorad Mazic (Serbia)

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo

Mechi za Kwanza

Jumanne 21 Februari 2017

Bayer 04 Leverkusen v Atlético Madrid              

Manchester City v Monaco              

Jumatano 22 Februari 2017

FC Porto v Juventus              

Sevilla v Leicester City          

Mechi za Pili

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

Jumanne 7 Machi 2017

Arsenal v Bayern Munich                

Napoli v Real Madrid              

Jumatano 8 Machi 2017

Barcelona v Paris Saint Germain (0-4)          

Borussia Dortmund v Benfica (0-1)      

Jumanne 14 Machi 2017

Juventus v FC Porto              

Leicester City v Sevilla          

Jumatano 15 Machi 2017

Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen              

Monaco v Manchester City