UEFA CHAMPIONZ LIGI: PEP ASALIMU KWA YAYA, AREJESHWA KUNDINI ULAYA!

CITY-PEP-YAYAKIUNGO Yaya Toure amerejeshwa Kikosini mwa Manchester City kwa ajili ya Mechi zao za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL.

Toure, mwenye Miaka 33, hakusajiliwa kwa ajili ya Mechi za Makundi za UCL na pia kutupwa nje ya Kikosi cha Kwanza cha Man City baada ya Meneja wa Timu hiyo Pep Guardiola kuingia kwenye Bifu na Wakala wa Gwiji huyo kutoka Ivory Coast.

Wakala Dimitri Seluk alimijia juu Guardiola na Meneja huyo kuapa Toure hatakuwemo Kikosini mwake hadi aombwe radhi.

Wakala huyo hakuomba radhi na ikabidi Yaya Toure mwenyewe achukue jukumu hilo na kuanzia Novemba, Kiungo huyo akarejeshwa Kikosi cha Kwanza.

Kwenye UCL, Toure anachukuwa Nafasi ya Ilkay Gundogan ambae ni Majeruhi.

Man City wataivaa AS Monaco hapo Februari 21 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL.

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo

Jumanne 14 Februari 2017

Benfica v Borussia Dortmund                

Paris Saint Germain v Barcelona            

Jumatano 15 Februari 2017

Bayern Munich v Arsenal             

Real Madrid v Napoli                  

Jumanne 21 Februari 2017

Bayer 04 Leverkusen v Atlético Madrid             

Manchester City v Monaco          

Jumatano 22 Februari 2017

FC Porto v Juventus          

Sevilla v Leicester City                

Jumanne 7 Machi 2017

Arsenal v Bayern Munich             

Napoli v Real Madrid                  

Jumatano 8 Machi 2017

Barcelona v Paris Saint Germain            

Borussia Dortmund v Benfica                

Jumanne 14 Machi 2017

Juventus v FC Porto          

Leicester City v Sevilla                

Jumatano 15 Machi 2017

Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen             

Monaco v Manchester City          

++++++++++++++++++++++++++++

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MTOANO:

14/15 na 21/22 Feb 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza

7/8 na 14/15 Machi 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Pili

11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza

18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)