BUNDESLIGA: BAYERN YAFUNGA MWAKA KWA KUIBONDA TIMU MPYA LEIPZIG NA KUKWEA KILELE

BUNDESLIGA-LOGO-16-17!MABINGWA WATETEZI Bayern Munich wanaenda Vakesheni ya Krismasi na Mwaka Mpya wakiwa kileleni mwa Bundesliga baada ya Jana kuibonda Timu iliyopanda Daraja Msimu huu RB Leipzig Bao 3-0.
Sasa Bayern wako mbele ya Timu ya Pili Leipzig kwa Pointi 3.
Bao za Bayern hapo Jana zilufungwa na Thiago na Xabi Alonso na kisha Leipzig wakapata pigo Dakika ya 30 pale Emil Fosberg alipopewa Kadi Nyekundu kwa kumchezea Rafu mbaya Philipp Lahm.      
Robert Lewandowski akapiga Bao la 3 kwa Penati iliyotolewa baada ya Kipa wa Leipzig Peter Gulasci kumchezea Faulo Douglas Costa.
Licha ya kufungwa, kikiwa ni kipigo chao cha pili Msimu huu wao wa kwanza kwenye Bundesliga, Leipzig wako Nafasi ya Pili.
Chini ya Kocha Ralph Hasenhuttl, Leipzig wameshinda Mechi zao 11 za kwanza za Bundesliga kati ta 15 ikiwa pamoja na kuifunga Timu ngumu Borussia Dortmund.
BUNDESLIGA
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumanne Desemba 20
BV Borussia Dortmund 1 FC Augsburg 1
Borussia Monchengladbach 1 VfL Wolfsburg 2
Hamburger SV 2 Schalke 1
Eintracht Frankfurt 3 FSV Mainz 0
Jumatano Desemba 21
Bayern Munich 3 RB Leipzig 0
Hertha Berlin 2 SV Darmstadt 0
FC Koln 1 Bayer 04 Leverkusen 1
TSG 1899 Hoffenheim 1 SV Werder Bremen 1
FC Ingolstadt 1 SC Freiburg 2
Ijumaa Januari 20
2230 SC Freiburg v Bayern Munich8