BUNDESLIGA KUFUNGA MWAKA: TIMU MPYA LEIPZIG KUWAFUNGA BAYERN, KUWANG’OA KILELENI NA KUKAA WAO??

BUNDESLIGA-LOGO-16-17RB Leipzig, ambayo imepanda Daraja Msimu huu, na kuishangaza Germany yote kwa kuwahi kutwaa uongozi wa Bundesliga, wanatarajia kufunga Mwaka kwa kutua huko Allianz Arena Jumatano kuwavaa Bayern Munich na ushindi kwao utawaweka kileleni mwa Ligi hiyo ambayo inaenda Mapumzikoni hadi Januari.

Leipzig, ambao walifufuliwa rasmi baada ya Kampuni ya Kutengeneza Red Bull kuanza kuwadhamini Mwaka 2009 na kuanza kupanda Madaraja haraka, wanafungana Pointi na Bayern, wote wakiwa na Pointi 36 baada ya Mechi 15, lakini Bayern wapo kileleni kwa Ubora wao wa Magoli.

Chini ya Mkurugenzi wa Michezo, Ralf Rangnick, Leipzig wameshinda Mechi 11 na kufungwa 1 tu katika Mechi 15 za Bundesliga.BUNDESLIGA-DES19

Rangnick amesema: “Tunakwenda Munich na ikiwezekana tuchukue Pointi 3!”

Msimu huu, chini ya Kocha Carlo Ancelotti, Bayern imefifia kidogo na Jumapili walihenya kuilaza Darmstadt 98 Bao 1-0 lakini kwenye Mechi hii na Leipzig wanatarajiwa kuongezwa nguvu kwa kurudi dimbani Majeruhi Arjen Robben na Franck Ribery.

Tishio kubwa toka kwa Leipzig kwa Bayern ni Mchezaji wa Kimataifa wa Germany Timo Werner, ambae tayari ana Bao 9, na mwenzake Emil Forsberg mwenye 15 Msimu huu katika Mashindano yote.

BUNDESLIGA

Ratiba

**Saa za Bongo

Jumanne Desemba 20

2200 BV Borussia Dortmund v FC Augsburg

2200 Borussia Monchengladbach v VfL Wolfsburg

2200 Hamburger SV v Schalke 04

2200 Eintracht Frankfurt v FSV Mainz 05

Jumatano Desemba 21

2200 Bayern Munich v RB Leipzig

2200 Hertha Berlin v SV Darmstadt 98

2200 FC Koln v Bayer 04 Leverkusen

2200 TSG 1899 Hoffenheim v SV Werder Bremen

FC Ingolstadt 04 v SC Freiburg

Ijumaa Januari 20

2230 SC Freiburg v Bayern Munich