UEFA CHAMPIONZ LIGI: ARSENAL KUIVAA NANI RAUNDI YA MTOANO?

UCL-2016-17-1-2-1BAADA kuitandika Basel 4-1 na kutwaa ushindi wa Kundi A sasa macho ya Arsenal ni Jumatatu ambapo watajua nani mpinzani wao kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Hii ni mara ya kwanza tangu 2011 kwa Arsenal kumaliza Kundi la UCL wakiwa ndio Washindi wa Kwanza na huenda safari hii wakafuta mkosi wa Misimu 6 mfululizo hadi sasa wa kutolewa Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Pia hii ni mara ya kwanza kwa Arsenal katika Miaka 11 kwa kumaliza Mechi za Kundi lake bila kufungwa.
Pengine hiyo ni dalili nzuri kwa Arsenal kwani mara ya mwisho kwa hilo kutokea kwao walifika Fainali ya UCL na kufungwa na Barcelona.
Miongoni mwa Timu ambazo Arsenal wanaweza kupangiwa kucheza nazo kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ni pamoja na Mabingwa Watetezi Real Madrid, Bayern Munich, Benfica au Bayer Leverkusen.
                    MSHINDI              MSHINDI WA PILI
KUNDI A Arsenal                     PSG
KUNDI B Napoli                       Benfica
KUNDI C Barcelona                 Manchester City
KUNDI D Atletico Madrid       Bayern Munich
KUNDI E Monaco                    Bayer Leverkusen
KUNDI F Borussia Dortmund Real Madrid
KUNDI G Leicester City           Porto
KUNDI H Juventus                   Sevilla
Droo:
Mshindi wa kila Kundi atapewa Mpinzani wa toka Kundi la Washindi wa Pili isipokuwa hatapangiwa Timu aliyokuwa nayo Kundi au Timu nyingine toka Nchi yake.
Mshindi wa Kundi atacheza Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 Ugenini na ile ya pili Nyumbani kwake.
TIMU ZIPI ZINAWEZA KUPANGWA KUWAVWAPINZANI:
Arsenal -Wapinzani wanaweza kuwa: Bayer Leverkusen, Bayern Munich, Benfica, Real Madrid, Porto, Sevilla.
Manchester City's  -Wapinzani wanaweza kuwa: Atletico Madrid, Borussia Dortmund, Juventus, Monaco, Napoli.
Leicester City  -Wapinzani wanaweza kuwa: Bayer Leverkusen, Bayern Munich, Benfica, Paris St-Germain, Real Madrid, Sevilla.
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MAKUNDI:
MECHI ZA MTOANO:
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)
 
 

Habari MotoMotoZ