UEFA CHAMPIONZ LIGI: ARSENAL YATWAA USHINDI KUNDI A!

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Matokeo

Jumanne 6 Desemba 2016

KUNDI A

FC Basel 1 Arsenal 4

Paris Saint Germain 2 Ludogorets Razgrad 2              

KUNDI B

Benfica 1 Napoli 2            

Dynamo Kiev 6 Besiktas 0          

KUNDI C

Barcelona 4 Borussia Monchengladbach 0                 

Manchester City 1 Celtic 1

KUNDI D

Bayern Munich 1 Atlético Madrid 0                  

PSV Eindhoven 0 FC Rostov 0     

+++++++++++++++++++++++++++++++++

UCL-2016-17-1-1Arsenal wamemaliza Mechi za Kundi A la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, wakiwa kileleni baada ya kuibamiza FC Basel 4-1 huko Uswisi wakati wenzao Paris Saint Germain wakitoka Sare 2-2 huko Paris.

PSG sasa wanashika Nafasi ya Pili na hivyo wao na Arsenal wanatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL wakati Ludogorets Razgrad, waliomaliza Nafasi ya 3, wanatumbukizwa Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.

Kwenye Kundi B, Napoli iliifunga Benfica 2-1 huko Ureno na Dynamo Kiev kuichapa Besiktas 6-0 na matokeo haya yanazifanya Napoli na Benfica zifuzu Raundi ya Mtoano wakati Besiktas ikitupwa EUROPA LIGI.

Dynamo Kiev walishatupwa nje kabla ya Mechi za Jana.

Katika Kundi C, ambalo likuwa likikamilisha Ratiba tu kwa vile Barcelona walishatwaa ushindi wa Kundi, Man City kuchukua Nafasi ya Pili na Borussia Monchengladbach kutupwa Nafasi ya 3 na hivyo kupelekwa EUROPA LIGI.

Jana Barca iliichapa Borussia Monchengladbach 4-0 na City kutoka Sare na Celtic.UCL-FINAL-A-D

Kwenye Kundi D, Atletico Madrid, ambao walishatwaa ushindi wa Kundi na Bayern Munich Nafasi ya Pili, Jana Bayern iliichapa Atletico 1-0 na PSV kutoka Sare 0-0 na Rostov matokeo ambayo yameipeleka Rostov EUROPA LIGI.

TIMU ZILIZOFUZU RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16:

Atlético Madrid*

Barcelona*

Leicester City*

Monaco*

Arsenal*

Bayer Leverkusen

Bayern München

Borussia Dortmund

Juventus

Manchester City

Paris Saint-Germain

Real Madrid

TIMU 7 AMBAZO ZINAWEZA KUFUZU [NAFASI 4 ZIMEBAKI]:

Sevilla

Lyon

Porto

København

Benfica

Napoli*

Beşiktaş

TIMU AMBAZO ZIMETUPWA EUROPA LIGI:

Borussia Mönchengladbach

Ludogorets Razgrad

Besiktas

Rostov

*=Timu ambayo imetwaa uongozi wa Kundi

PATA MAHESABU YA KUNDI KWA KUNDI:

-Timu 2 toka kila Kundi, toka Makundi 8, ndizo zitasonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16, na Timu zinazomaliza Nafasi ya 3, zitatupwa Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Ratiba Mechi za 6 na za mwisho za Makundi

***Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku

Jumatano 7 Desemba 2016

KUNDI E

Bayer 04 Leverkusen v Monaco             

Tottenham Hotspur v CSKA Moscow                

KUNDI F

Legia Warsaw v Sporting Lisbon           

Real Madrid v Borussia Dortmund         

KUNDI G

Club Brugge v FC Copenhagen              

FC Porto v Leicester City

KUNDI H

Juventus v Dinamo Zagreb         

Lyon v Sevilla         

++++++++++++++++++++++++++++

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MAKUNDI:

Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba

Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba

Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba

Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba

Mechi ya Tano: 22 na 23 Novemba

Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba

MECHI ZA MTOANO:

11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza

18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

 

 

 

 

 

Habari MotoMotoZ