UEFA CHAMPIONZ LIGI: LEO MECHI ZA MWISHO MAKUNDI, ARSENAL AU PSG NANI MBABE KUNDI A?

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Ratiba Mechi za 6 na za mwisho za Makundi

***Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku

Jumanne 6 Desemba 2016

KUNDI A

FC Basel v Arsenal

Paris Saint Germain v Ludogorets Razgrad                 

KUNDI B

Benfica v Napoli               

Dynamo Kiev v Besiktas             

KUNDI C

Barcelona v Borussia Monchengladbach           

Manchester City v Celtic

KUNDI D

Bayern Munich v Atlético Madrid           

PSV Eindhoven v FC Rostov        

+++++++++++++++++++++++++++++++++

UCL-2016-17-1-1UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Hatua ya Makundi, inafikia tamati Leo Jumanne kwa Makundi A hadi D na baadhi ya Makundi yake Timu zilizofuzu tayari zimepatikana na kilichobaki ni kuamua nani Mshindi wa Kundi.

Tayari Timu 12 zimeshafuzu Hatua ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na kubakisha Timu 7 kugombea Nafasi 4 zilizobaki.

Kundi A, Arsenal na Paris Saint-Germain, zimeshasonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na kilichobaki kuamua ni nani Mshindi wa Kundi na pia Timu ipi inamaliza Nafasi ya 3 ili iende kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Raundi ya Mtoano ya Timu 32.

Kwa Kundi B, vita ya kufuzu ipo kwa Timu 3, Napoli, Benfica na Besiktas, wakati Dynamo Kiev imeshatupwa nje kabis.

Kwa Kundi C, kazi imekwisha baada ya Barcelona kutwaa ushindi wa Kundi, Man City kuchukua Nafasi ya Pili na Borussia Monchengladbach kutupwa Nafasi ya 3 na hivyo kupelekwa EUROPA LIGI.

Kwenye Kundi D, Atletico Madrid wametwaa ushindi wa Kundi na Bayern Munich Nafasi ya Pili.

Rostov na PSV Eindhoven watagombea nani kucheza EUROPA LIGI.

TIMU ZILIZOFUZU RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16:

Atlético Madrid*

Barcelona*

Leicester City*

Monaco*

Arsenal

Bayer Leverkusen

Bayern München

Borussia Dortmund

Juventus

Manchester City

Paris Saint-Germain

Real Madrid

TIMU 7 AMBAZO ZINAWEZA KUFUZU [NAFASI 4 ZIMEBAKI]:

Sevilla

Lyon

Porto

København

Benfica

Napoli

Beşiktaş

TIMU AMBAZO ZIMETUPWA NJE UCL:

Celtic**

Club Brugge**

Dinamo Zagreb**

Dynamo Kyiv**

Basel

Borussia Mönchengladbach

CSKA Moskva

Legia Warszawa

Ludogorets Razgrad

PSV Eindhoven

Rostov

Sporting CP

Tottenham Hotspur

TIMU AMBAYO INA UHAKIKA KUCHEZA EUROPA LIGI:

Borussia Mönchengladbach

*=Timu ambayo imetwaa uongozi wa Ligi

**=Haziwezi kumaliza Nafasi za 3

PATA MAHESABU YA KUNDI KWA KUNDI:

-Timu 2 toka kila Kundi, toka Makundi 8, ndizo zitasonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16, na Timu zinazomaliza Nafasi ya 3, zitatupwa Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.

KUNDI A
MECHI ZA MWISHO: Basel v Arsenal, PSG v Ludogorets

Arsenal na Paris Saint-Germain washafuzu na wako Pointi sawa lakini PSG wana nafasi kubwa ya kumaliza wakiwa Nambari Wani wa Kundi hili kutokana na Matokeo Bora ya Uso kwa Uso kati yao.

Ikiwa PSG, ambao wako Nyumbani, wataifunga Ludogorets iliyopigwa Bao 6 na Arsenal, basi watatwaa uongozi wa Kundi A.

Hali iko hivyo hivyo kwa kusaka Ushindi wa 3 kwa Kundi ili kucheza UEFA EUROPA LIGI ambapo Razgrad wanawazidi FC Basel kwa Matokeo ya Uso kwa Uso.

KUNDI B
MECHI ZA MWISHO: Benfica v Napoli, Dynamo Kiev v Besiktas

Napoli wanahitaji Pointi 1 tu wakiwa Ugenini kwa Benfica lakini wanahitaji ushindi ili kutwaa Nafasi ya Kwanza ya Kundi.

Benfica wanahitaji ushindi ili wasonge lakini pia watafuzu wakipata Droo au hata kufungwa ikiwa Besiktas hawatapata matokeo bora kupita yao.

Besiktas watahakikisha kufuzu wakiwafunga Dynamo Kiev Ugenini lakini pia watasonga ikiwa Napoli hawashindi.

Dynamo Kiev wapo nje kabisa.

KUNDI C
MECHI ZA MWISHO: Barcelona v Borussia Monchengladbach, Manchester City v Celtic

Kwa Kundi hili, kazi imekwisha baada ya Barcelona kutwaa ushindi wa Kundi, Man City kuchukua Nafasi ya Pili na Borussia Monchengladbach kutupwa Nafasi ya 3 na hivyo kupelekwa EUROPA LIGI.

KUNDI D
MECHI ZA MWISHO: Bayern Munich v Atletico Madrid, PSV Eindhoven v FC Rostov

Atletico Madrid wametwaa ushindi wa Kundi na Bayern Munich Nafasi ya Pili.

Rostov na PSV Eindhoven watagombea nani kucheza EUROPA LIGI.

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Ratiba Mechi za 6 na za mwisho za Makundi

***Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku

Jumatano 7 Desemba 2016

KUNDI E

Bayer 04 Leverkusen v Monaco             

Tottenham Hotspur v CSKA Moscow                

KUNDI F

Legia Warsaw v Sporting Lisbon           

Real Madrid v Borussia Dortmund         

KUNDI G

Club Brugge v FC Copenhagen              

FC Porto v Leicester City

KUNDI H

Juventus v Dinamo Zagreb         

Lyon v Sevilla         

++++++++++++++++++++++++++++

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MAKUNDI:

Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba

Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba

Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba

Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba

Mechi ya Tano: 22 na 23 Novemba

Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba

MECHI ZA MTOANO:

11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza

18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

Habari MotoMotoZ