SERIE A: MWANA WA DIEGO SIMEONE AIFYEKA JUVE!

GIOVANNI-SIMEONEBAO 2 za Giovanni Simeone, Mtoto wa Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone, Jana ziliipa Genoa ushindi wa 3-1 dhidi ya Mabingwa na Vinara wa Serie A Juventus na kufumua mbio za Ubingwa wa Italy kuwa wazi.
Kipigo hiki cha 3 kwa Juve wanaowania kutwaa 'Scudetto', Ubingwa wa Serie A, kwa mara ya 6 mfululizo kimewaacha bado wako kileleni sasa wakiwa Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili AS Roma ambao Jana waliwafunga Pescara 3-2 na pia AC Milan ambao waliwachapa Empoli 4-1.
Juventus walisafiri kwenda huko Luigi Ferraris Stadium bila Mastaa kadhaa ambao walikuwa ni Majeruhi na hao ni Paulo Dybala, Marko Pjaca na Andrea Barzagli huku Beki Mzoefu Giorgio Chiellini akiwa fiti kuanzia Benchi tu na kulazimika kumtumia Beki Wingi Stephan Lichtsteiner kama Sentahafu.
Kocha wa Juve Massimiliano Allegri amekiri kipigo hicho ni pigo kwao kwenye Mechi ambayo pia Leonardo Bonucci na Dani Alves waliongezeka kwenye Listi yao ndefu ya Majeruhi.
Bao za Genoa zilufungwa na Simeone Dakika za 3 na 13 na la 3 Dakika ya 29 baada Alex Sandro kujifunga mwenyewe wakati Juve wakifunga Bao lao pekee Dakika ya 82 kwa Frikiki ya Mirelem Pjanic.

Habari MotoMotoZ