SERIE A: WIKIENDI YAANZA, MABINGWA JUVE UGENINI GENOA

JUVE-CHIELLINI-EVRAWIKIENDI ya Ligi Kuu huko Italy Serie A inaanza Leo kwa Mechi mbiliambapo Vigogo AC Milan wako Ugenini kwa Empoli na Torino wapo kwao kucheza AC Chievo Verona wakati Jumapili Mabingwa Watetezi na ambao pia Vinara Juventus wako Ugenini kucheza na Genoa.

Hiyo Jumapili, Mechi ya kwanza kabisa ni ile ya Palermo na Lazio huku Palermo wakiwania kukwepa kipigo chao cha 7 mfululizo.

Mechi nyingine za Jumapili ni zile za Atalanta na Bologna, Cagliari kuwa Wenyeji wa Udinese na Sampdoria kuitembelea Crotone.

Siku hiyo Usiku, AS Roma, ambao Wikiendi iliyopitwa walichapwa 2-1 na Atalanta, wapo kwao kuivaa Pescara.

Msimu uliopita, Mechi ya Genoa na Juve iliisha kwa Mabingwa hao wa Italy kushinda 2-0 na ukiondoa kipigo cha 1-0 cha Oktoba 2014, Juve wameichapa Genoa Mechi 6 zilizopita.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

Genoa: Perin; Izzo, Burdisso, Gentiletti; Edenilson, Rincon, Ntcham; Rigoni; Simeone, Ocampos

Kifungoni: Orban, Veloso

Juventus: Buffon; Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra; Khedira, Hernanes, Pjanic, Cuadrado, Mandzukic, Alex Sandro

Suspended: Hamna

Ratiba

Jumamosi Novemba 26

2000 Torino FC v AC Chievo Verona

2245 Empoli v AC Milan

Jumapili Novemba 27

1430 U.S. Citta di Palermo v SS Lazio

1700 Bologna FC v Atalanta

1700 Cagliari Calcio v Udinese Calcio

1700 Genoa CFC v Juventus FC

1700 Crotone v UC Sampdoria

2245 AS Roma v Pescara

Jumatatu Novemba 28

2100 SSC Napoli v US Sassuolo Calcio

2300 Inter Milan v ACF Fiorentina

Habari MotoMotoZ