UEFA EUROPA LIGI:MAN UNITED WAITANDIKA FEYENOORD, KEPTENI ROONEY AWEKA REKODI!

MANUNITED-FEYEMANCHESTER UNITED wakiwa Uwanjani kwao Old Trafford wakicheza Mechi yao ya 5 ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI wameweka matumaini makubwa ya kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 32 baada ya kuiwasha Feyenoord Bao 4-0 na pia Kepteni wao Wayne Rooney kuvunja Rekodi ya Klabu hiyo.

Rooney ndie aliifungia Man United Bao la Kwanza akifika Bao 39 za Mechi za Mashindano ya UEFA Ulaya na kuvunja Rekodi ya Ruud Van Nistelrooy ya Bao 38 kwa Man United.

Pia Bao hilo limemfanya Rooney abakishe Bao 1 tu kuikamata Rekodi ya Mfungaji Bora katika Historia ya Man United Sir Bobby Charlton mwenye Bao 249.

Rooney ndie Mwaka Jana alievunja Rekodi ya Sir Bobby Charlton ya Goli nyingi kwa Timu ya Taifa ya England na yeye kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya Taifa hilo.

Rooney alifunga Bao hilo Dakika ya 35 na nyingine kupachikwa na Juan Mata, Kipa Bradley Jones kujifunga mwenyewe alipopigwa tobo na Zlatan Ibrahimovic na la mwisho la Jesse Lingard.

Mapema kabla Mechi hii katika Mechi nyingine ya Kundi A, Fenerbahce, wakiwa kwao Uturuki, waliifunga Zorya Luhansk ya Ukraine 2-0 na kuongoza Kundi A wakiwa na Pointi 10 na Man United wapo wa Pili wakiwa na Pointi 9 wakifuatia Feyenoord wenye Pointi 7.

Mechi za mwisho zitachezwa Desemba 8 kwa Feyenoord kuivaa Fenerbahce na Man United kuwa wageni wa Zorya Luhansk.

VIKOSI:

Man United: Romero; Valencia, Jones, Blind, Shaw; Carrick, Pogba; Mata, Rooney, Mkhitaryan; Ibrahimovic

Akiba: De Gea, Rojo, Fellaini, Herrera, Lingard, Memphis, Rashford

Feyenoord: Jones; Karsdorp, Dammers, Van der Heijden, Nelom; Tapia, Kuyt, Vilhena, Toornstra, Jørgensen, Elia

Akiba: Hansson, Woudenberg, Nieuwkoop, Vejinovic, Berghuis, Basaçikoglu, Kramer

REFA: Manuel Gräfe (Germany)

UEFA EUROPA LEAGUE

Ratiba:

Alhamisi Novemba 24

***Saa za Bongo

KUNDI A

Fenerbahçe 2 Zorya Luhansk 0    

Manchester United 4 Feyenoord 0         

KUNDI B

FC Astana 2 Apoel Nicosia 1        

Olympiakos 1 BSC Young Boys 1           

KUNDI C

FK Qabala 1 RSC Anderlecht 3              

Saint-Étienne 0 Mainz 0              

KUNDI D

Zenit St Petersburg 2 Maccabi Tel-Aviv 0          

Dundalk 0 AZ Alkmaar 1   

KUNDI E

Austria Vienna 1 Astra Giurgiu 2           

Roma 4 Viktoria Plzen 1             

KUNDI F

Athletic Bilbao 3 Sassuolo 2                  

KRC Genk 1 Rapid Vienna 0                  

KUNDI G

Ajax 2 Panathinaikos 0               

Celta Vigo 1 Standard Liege 1               

KUNDI H

KAA Gent 2 Sporting Braga 2                

Shaktar Donetsk 4 Konyaspor 0            

KUNDI I

FC Schalke 2 Nice 0          

FK Krasnodar 1 FC Red Bull Salzburg 1            

KUNDI J

Fiorentina 2 PAOK Salonika 3                

Slovan Liberec 3 FK Qarabag 0             

KUNDI K

Hapoel Be'er Sheva 3 Inter Milan 2                 

Sparta Prague 1 Southampton 0           

KUNDI L

FC Zürich 1 Villarreal 1     

Steaua Bucharest 2 Osmanlispor 1                  

TAREHE MUHIMU

Droo

26/08/16: Makundi

12/12/16: Raundi ya Mtoano ya Timu 32

24/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16

17/03/17: Robo Fainali

Makundi

15/09/16: Mechidei 1

29/09/16: Mechidei 2

20/10/16: Mechidei 3

03/11/16: Mechidei 4

24/11/16: Mechidei 5

08/12/16: Mechidei 6

16/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Mechi za Kwanza

23/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Marudiano

09/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi za Kwanza

16/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Marudiano

13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza

 

Habari MotoMotoZ