ROBERT LEWANDOWSKI – BAYERN YAZIONYA CHELSEA NA MAN UNITED KUMSAHAU AU KULIKWAA RUNGU LA FIFA!

Bayern Munich imeziambia Chelsea na Manchester United kusahau kabisa kumsaini Robert Lewandowski kipindi hiki cha Uhamisho.

BAYERN LEWANDOWSKI MAGOLIBayern Munich imesisitiza hamna nafasi hata chembe kwa Lewandowski kuihama Klabu hiyo ya Germany hivi sasa.

Hivi karibuni Wakala wa Lewandowskit, Maik Barthel, alitoboa kuwa Staa huyo wa Poland hakuwa na furaha na Bosi wa Bayern Carlo Anceloti na Wachezaji wenzake kwa kushindwa kumsaidia kutwaa Buti ya Dhahabu ya Bundesliga anayopewa Mfungaji Bora wa Ligi hiyo.

Buti hiyo ilitwaliwa na Straika wa Borussia Dortmund anaetoka Gabon Pierre-Emerick Aubameyang aliepachika Bao 31 huku Lewandowski akifunga Bao 30.

Maik Barthel aliliambia Gazeti la Germany Kicker: "Robert aliniambia hakupata sapoti ya na Kocha hakuamrisha asaidiwe ili afunge Bao zaidi awe Mfungaji Bora. Hilo lilimvunja moyo sana!”

Matamshi hayo yakaibua hisia kuwa Lewandowski atahama na Klabu za England Chelsea na Man United kumkodolea macho na kuhusishwa sana na kumchukua Straika huyo mwenye Miaka 28.

Lewandowski, ambae amewafungia Mabingwa hao wa Germany Mabao 110 katika Misimu Mitatu, alisaini Mkataba Mpya na Bayern Mwezi Desemba 2016 ambao utamweka kwa Miaka Mitatu zaidi.

Kufuatia hali hii ya utata Klabu ya Bayern imetoa tamko kali: “Bayern Munich haipotezi muda kuhusu Uhamisho wa Lewandowski. Hamna mazungumzo na Klabu yeyote na hayatakuwepo. Ikiwa Klabu nyingine zinataka kuzungumza na Wachezaji, wenye Mikataba ya muda mrefu, wapo hatarini kuadhibiwa na FIFA. Hata Wakala wake ametuhakikishia hakuna mazungumzo ya Uhamisho yanayofanyika.”

UEFA EUROPA LIGI: PATA MECHI ZA RAUNDI YA 1, NA YA PILI ZA MTOANO, KALENDA YA TAREHEMU MUHIMU!

EUROPA LIGIJANA ilifanyika Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya Kwanza ya Mtoano na ya Pili za UEFA EUROPA LIGI kwa Msimu Mpya wa 2017/18.

Kwa Wadau wa England, Arsenal, ambao walimaliza Nafasi ya 5 na sasa wamo Mashindano haya, wao wapo moja kwa moja Makundi.

Southampton wao wataanzia Raundi ya Mchujo ambayo ni Hatua moja kabla Makundi.

RAUNDI YA KWANZA YA MTOANO

**Mechi kuchezwa Juni 29 na Julai 6

Dacia Chisinau (MDA) v Shkëndija (MKD)

Levski Sofia (BUL) v Sutjeska (MNE)

Irtysh Pavlodar (KAZ) v Dunav Ruse (BUL)

Jagiellonia Białystok (POL) v Dinamo Batumi (GEO)

Željezničar (BIH) v Zeta (MNE)

AEK Larnaca (CYP) v Lincoln (GIB)

Midtjylland (DEN) v Derry City (IRL)

Dinamo Minsk (BLR) v NSÍ Runavík (FRO)

Ferencváros (HUN) v Jelgava (LVA)

Lyngby (DEN) v Bangor City (WAL)

Trenčín (SVK) v Torpedo Kutaisi (GEO)

Lech Poznań (POL) v Pelister (MKD)

Mladost Podgorica (MNE) v Gandzasar-Kapan (ARM)

Videoton (HUN) v Balzan (MLT)

AEL Limassol (CYP) v St Joseph's (GIB)

Skënderbeu (ALB) v Sant Julià (AND)

Haugesund (NOR) v Coleraine (NIR)

Stjarnan (ISL) v Shamrock Rovers (IRL)

IFK Norrköping (SWE) v Prishtina (KOS)

AIK (SWE) v KÍ Klaksvík (FRO)

RAUNDI YA PILI MTOANO

**Mechi kuchezwa Julai 13 na Julai 20

Partizani (ALB) AU Botev Plovdiv (BUL) v Beitar Jerusalem (ISR) AU Vasas (HUN)

Željezničar (BIH) AU Zeta (MNE) v AIK (SWE) AU KÍ Klaksvík (FRO)

Haugesund (NOR) AU Coleraine (NIR) v Lech Poznań (POL) AU Pelister (MKD)

Apollon Limassol (CYP) v Zaria Balti (MDA) AU FK Sarajevo (BIH)

AEK Larnaca (CYP) AU Lincoln (GIB) v Levadia Tallinn (EST) AU Cork City (IRL)

Brøndby (DEN) v VPS Vaasa (FIN) AU Olimpija Ljubljana (SVN)

Rabotnicki (MKD) AU Tre Penne (SMR) v Dinamo Minsk (BLR) AU NSÍ Runavík (FRO)

Kairat Almaty (KAZ) AU Atlantas (LTU) v Skënderbeu (ALB) AU Sant Julià (AND)

IFK Norrköping (SWE) AU Prishtina (KOS) v St Johnstone (SCO) AU Trakai (LTU)

Slovan Bratislava (SVK) AU Pyunik (ARM) v Lyngby (DEN) AU Bangor City (WAL)

Panionios (GRE) v Shirak (ARM) AU Gorica (SVN)

Hajduk Split (CRO) v Levski Sofia (BUL) AU Sutjeska (MNE)

Stjarnan (ISL) AU Shamrock Rovers (IRL) v Mladá Boleslav (CZE)

Zirä (AZE) AU Differdange (LUX) v Astra Giurgiu (ROU)

Nõmme Kalju (EST) AU B36 Tórshavn (FRO) v Videoton (HUN) AU Balzan (MLT)

Maccabi Tel-Aviv (ISR) AU Tirana (ALB) v SJK Seinäjoki (FIN) AU KR Reykjavík (ISL)

Chikhura Sachkhere (GEO) AU Altach (AUT) v Dinamo Brest (BLR)

Aberdeen (SCO) v Ordabasy (KAZ) AU Široki Brijeg (BIH)

Valletta (MLT) AU Folgore (SMR) v Utrecht (NED)

Östersund (SWE) v Galatasaray (TUR)

Ferencváros (HUN) AU Jelgava (LVA) v Midtjylland (DEN) AU Derry City (IRL)

Vojvodina (SRB) AU Ružomberok (SVK) v Brann (NOR)

Mladost Lučani (SRB) AU İnter Bakı (AZE) v Fola Esch (LUX) AU Milsami Orhei (MDA)

Sturm Graz (AUT) v Mladost Podgorica (MNE) AU Gandzasar-Kapan (ARM)

Crusaders (NIR) AU Liepāja (LVA) v Shakhtyor Soligorsk (BLR) AU Sūduva (LTU)

Bala Town (WAL) AU Vaduz (LIE) v Odd (NOR) AU Ballymena United (NIR)

Dacia Chisinau (MDA) AU Shkëndija (MKD) v Connah's Quay Nomads (WAL) AU HJK Helsinki (FIN)

Gabala (AZE) v Jagiellonia Białystok (POL) AU Dinamo Batumi (GEO)

Ventspils (LVA) AU Valur Reykjavík (ISL) v Domžale (SVN) AU Flora Tallinn (EST)

Trenčín (SVK) AU Torpedo Kutaisi (GEO) v Bnei Yehuda Tel-Aviv (ISR)

Rangers (SCO) AU Progrès Niederkorn (LUX) v AEL Limassol (CYP) AU St Joseph's (GIB)

Irtysh Pavlodar (KAZ) AU Dunav Ruse (BUL) v Crvena zvezda (SRB) AU Floriana (MLT)

UE Santa Coloma (AND) AU Osijek (CRO) v Luzern (SUI)

KALENDA - UEFA EUROPA LIGI 2017/18

19/06/17: Droo Raundi ya 1 na 2 za Mtoano

29/06/17: Mechi za Kwanza Raundi ya Mtoano ya

06/07/17 1Mechi za Pili Raundi ya Mtoano ya 1

13/07/17: Mechi za Kwanza Raundi ya Mtoano ya 2

14/07/17: Droo ya Raundi ya 3 Mtoano

20/07/17: Second qualifying round, second leg

27/07/17: Mechi za Kwanza Raundi ya Mtoano ya 3

03/08/17: 1Mechi za Pili Raundi ya Mtoano ya 3

04/08/17: Droo Raundi ya Mchujo

17/08/17: Mechi za Kwanza Raundi ya Mchujo

24/08/17: Mechi za Pili Raundi ya Mchujo

25/08/17 Droo ya Makundi

14/09/17: Mechi ya 1

28/09/17: Mechi ya 2

19/10/17: Mechi ya 3

02/11/17: Mechi ya 4

23/11/17: Mechi ya 5

07/12/17: Mechi ya 6

11/12/17: Droo Raundi ya Mtoano ya Timu 32

15/02/18: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Mechi ya Kwanza

22/02/18: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Mechi ya Pili

23/02/18: Droo Raundi ya Mtoano ya Timu 16

08/03/18: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza

15/03/18: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechibya Pili

16/03/18: Droo Robo Fainali

05/04/18: Robo Fainali Mechi ya Kwanza

12/04/18: Robo Fainali Mechi ya Pili

13/04/18: Droo Nusu Fainali na Fainali

26/04/18: Nusu Fainali Mechi ya Kwanza

03/05/18: Nusu Fainali Mechi ya Pili

16/05/18: Fainali (Stade de Lyon, Lyon)

CHELSEA ‘MWENDOKASI’ KUWANASA ALEX SANDRO, TIEMOUÉ BAKAYOKO KUMPOZA ‘MBOGO’ CONTE!

CHELSEA CONTE BORAMABINGWA WA ENGLAND Chelsea wanatarajiwa Wiki hii kuongeza kasi ya kuwanasa Alex Sandro wa Juventus na Tiemoué Bakayoko wa AS Monaco ili kumtuliza Meneja Antonio Conte ambae amepandwa na hasira kwa kutonunuliwa Mchezaji yeyote Mpya katika Walengwa wa Listi yake.

Conte, ambae yuko Vakesheni huko kwao Italy, alichukizwa na kutokuwepo na jitihada zozote na kukazuka habari ataondoka Chelsea kitu ambacho Klabu hiyo imekikana.

Inadaiwa Chelsea ilimtaka Conte auze baadhi ya Wachezaji waliokuwepo ilia pate Wapya na hilo likamsukuma kumtumia SMS Diego Costa kuwa hayumo kwenye mipango ya Chelsea na kumfanya Fowadi huyo alipue taarifa hiyo hadharani na kuibua msuguano mwingine kati ya Conte na Uongozi wa Chelsea.

Pengine hilo la kuondoka kwa Costa ndilo limewafanya Everton, wakijua wazi Chelsea wanamtaka Straika wao Romelu Lukaku, kudai Dau la Rekodi ya Dunia kumnunua Fowadi huyo wa Belgium alieazimwa toka Chelsea na kisha kuuzwa moja kwa moja kwa Bei chee.

+++++++++++++

Chelsea – Uhamisho wa Wachezaji Kipindi hiki:

Ndani

Hamna

Nje

Juan Cuadrado (Juventus) Ada Haikutajwa

Christian Atsu (Newcastle United) Ada Haikutajwa

Asmir Begovic (AFC Bournemouth) Ada Haikutajwa

Dominic Solanke (Liverpool) Uhamisho wa Bure

Alex Kiwomya (Doncaster Rovers) Ada Haikutajwa

+++++++++++++

Kuhusu Alex Sandro, Meneja Mkuu wa Juventus, Beppe Marotta, ametoboa Ofa ya kwanza ya Chelsea imekataliwa na sasa Chelsea wanategemewa kurudi na Dau la Pauni Milioni 55.

Sandro, alieichezea Brazil Mechi 7, alianzia huko Ureno akiwa na FC Porto na Antonio Conte anamthamini kuwa ni bora kupita Winga-Beki wao wa Kushoto Marcos Alonso.

Pia, Chelsea wameongeza juhudi za kumnasa Kiungo Tiemoué Bakayoko wa AS Monaco anaechezea Timu ya Taifa ya France ambae Dau lake linakadiriwa kuwa zaidi ya Pauni Milioni 40.

Wadau wanahisi ujio wa Bakayoko huenda ukafungua kuuzwa kwa Nemanja Matic.

Vile vile, Chelsea wanatarajiwa kumsaini kama Mchezaji Huru Kipa Willy Caballero aliemaliza Mkataba na Manchester City ili awe Msaidizi wa Kipa Nambari Wani Thibaut Courtois baada ya Kipa Rizevu Asmir Begovi kuuzwa kwa Bournemouth.

 

KUMBEEE: CONTE ACHUKIZWA BAADA CHELSEA KUMWAMBIA ‘UZA WACHEZAJI UNUNUE WAPYA’!

>NDIO MAANA COSTA AKAWASHWA SMS ‘SIKUTAKI’!

MGONGANA wa Meneja Antonio Contena Klabu yake Chelsea kumbe ulianza baada ya kuambiwa hawezi kupata Wachezaji Wapya bila kuuza baadhi ya waliokuwepo.

CHELSEA-CONTE-BORAHivi karibuni iliripotiwa kuwa Conte anataka kuondoka Chelsea kabla Msimu Mpya haujaanza kitu ambacho Chelsea ilikikanusha.

Sasa Magazeti huko England yamebaini kuwa yale aliyotoboa Straika wa Chelsea Diego Costa kuwa alitumiwa Ujumbe wa Simu na Conte na kuambiwa hayupo kwenye mipango yake kwa Msimu ujao, na hivyo hahitajika, yametokana na kuamriwa Conte na Klabu kuwa ‘Uza, Ununue’!

Duru za England zimebaini kuwa Conte amewaambia baadhi ya Marafiki zake huko kwao Italy kuwa amekasirishwa na amri hiyo ya kujitafutia Fedha mwenyewe za kununua Wachezaji Wapya kwa kuuza hao waliomsaidia kutwaa Ubingwa katika Msimu wake wa kwanza tu.

Hali hii imedaiwa kumfanya Conte atafakari kubwaga manyanga kwani tayari alishatoa Listi kwa Uongozi wa Chelsea nani anawataka kuimarisha Kikosi chake.

Inasemekana Conte alikabidhi Listi yenye Majina ya Straika wa Everton Romelu Lukaku, Kiungo wa AS Monaco Tiemoue Bakayoko, Sentahafu wa Bayern Munich Jerome Boateng na Fulbeki wa Kushoto wa Juventus Alex Sandro na wote kwa ujumla wangegharimu Pauni Milioni 200.

Inadaiwa Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich, hayupo tayari kumwaga Donge lote hilo na hiyo ndio imesababisha Chelsea kutonunua Mchezaji Mpya hadi sasa.

Hilo limemchukiza mno Conte na hasa akicheki Wapinzani Wakuu wake, kama vile Man City na Man United, wakiwa tayari wamejikita Sokoni kwa kishindo.

Pep Guardiola na Man City tayari washawachukuwa Kiungo wa AS Monaco Bernardo Silva kwa Pauni Milioni 43 na Pauni Milioni 35 kumnunua Kipa wa Benfica kutoka Brazil, Ederson.

Jose Mourinho na Man United tayari washamzoa Beki wa Kimataifa wa Sweden Victor Lindelof kutoka Benfica na wanakaribia kuwanasa Straika wa Real Madrid Alvaro Morata na Fowadi wa Inter Milan Ivan Perisic.

 

UEFA YABUNI TUZO 5 MPYA ZA WACHEZAJI BORA WA MWAKA, WASHINDI AGOSTI 24!

>TOTTI ATUNUKIWA TUZO YA RAIS WA UEFA!

UEFA imetangaza kuanza kutolewa kwa Tuzo za Wachezaji Bora wa Mwaka 5 Mpya kuanzia Agosti hii ambazo Washindi wake watapatikana toka Kura za Makocha na Wanahabari.

UEFA-GRIMALDI-FORUMTuzo hizo zitakabidhiwa huko Monaco hapo Agosti 24 wakati wa Droo ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Tuzo hizo 5 Mpya ni kwa Wachezaji waliofanya vyema kwenye Mashindano ya Klabu ya UEFA kwa Msimu uliopita, yaani ule wa 2016/17, na zitatoka sambamba na zile za sasa za Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Wanaume na Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Kinamama.

Tuzo hizo 5 Mpya ni:

-UEFA CHAMPIONZ LIGI:

-Kipa Bora

-Beki Bora

-Kiungo Bora

-Fowadi Bora

**Hizi zitatolewa Agosti 24

-UEFA EUROPA LIGI:

-Mchezaji Bora wa UEFA Europa Ligi kwa Msimu wa 2016/17.

Kura Kupata Washindi zitakavyopigwa:

Wapiga Kura za Washindi wa Tuzo ni Makocha wa zile Klabu zilizocheza Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na UEFA EUROPA LIGI kwa Msimu wa 2016/17 wakijumuika na Wanahabari 55 kutoka European Sports Media (ESM) kila Mmoja akiwakilisha Nchi Moja Wanachama wa UEFA.

Makocha hawaruhusiwi kumpigia Mchezaji kutoka Timu yake.

Wagombea watakaofika Fainali:

Wagombea wa Tuzo 5 Mpya ambao watatinga Fainali watatangazwa Agosti 4.

Wagombea wa Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Wanaume na Kinamama, Watatu Watatu kila Kundi, watatangazwa Agosti 15.

Tuzo ya Rais wa UEFA:

Tuzo ya Rais wa UEFA kwa Mwaka 2017 imeenda kwa Mchezaji wa Italy Francesco Totti kwa Uchezaji wake uliotukuka katika Maisha yake ya Soka ambapo ameamua kustaafu hivi karibuni.

Totti atakabidhiwa Tuzo yake Agosti 24.

 

Habari MotoMotoZ