RONALDO ASHITAKIWA SPAIN UKWEPAJI KODI!

>AJIBU: "QUIEN NO DEBE NO TEME!"

REAL-RONALDO-BAOWAENDESHA MASHITAKA huko Spain wamefungua Kesi wakimtuhumu Cristiano Ronaldo na Ukwepaji Kodi.

Ronaldo, Mchezaji wa Klabu ya Real Madrid humo Nchini Spain na pia ni Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Portugal, anadaiwa kukwepa kulipa Kodi ya Euro Milioni 14.7 kati ya Miaka 2011 na 2014.

Tangu tuhuma hizi ziibuke Ronaldo, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani na pia ndie Mchezaji mwenye kulipwa Pesa nyingi Duniani, amesema hana wasiwasi na uchunguzi dhidi yake kwa vile hana cha kuficha.

Imedaiwa kuwa Ronaldo alijua ‘Mfumo wa Kibiashara’ ulioanzishwa kwa makusudi ili kuficha Mapato yake yatokanayo na Haki zake za Picha na Matangazo yake.

Tuhuma zilichomoza Mwezi Desemba ilipodaiwa Ronaldo alianzisha Makampuni nje ya Spain ili kukwepa Kodi.

Alipohojiwa kuhusu uchunguzi dhidi yake na Redio ya Nchini kwao Ureno kuhusu tuhuma za Ukwepaji Kodi, Ronaldo alijibu: "Quien no debe no teme", ambayo tafsiri yake inamaanisha "Yule ambae hana cha kuficha, haogopi kitu!"

Kwa mujibu wa Magwiji wa Habari za Fedha, Forbes, Ronaldo ndie Mwanamichezo alievuna Pesa nyingi Duniani kwa Miaka Miwili mfululizo akizoa Dola Milioni 93 kutokana na Mshahara, Bonasi na Matangazo kwa Mwaka Jana.

 

LIONEL MESSI AMSIFIA CRISTIANO RONALDO - AMTAJA ANA 'KIPAJI CHA AJABU'!

NI NADRA sana kwa Wachezaji wa Barcelona na Real Madrid kusifiana lakini Lionel Messi ameibuka na kumpongeza Cristiano Ronaldo.

CR7-MESSIMessi amemsifia Ronaldo kwamba ana kipaji cha pekee kwa kuisaidia Real Madrid kubeba UEFA CHAMPIONZ LIGI walipoibamiza Juventus 4-1 Wiki iliyopita huku Ronaldo akipiga Bao 2.
Mara nyingi Messi na Ronaldo hupambana kuzoa Mataji na hata safari hii wanachuana tena kugombea Ballon d'Or huku Ronaldo akionekana na uhakika kuitwaa Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora Duniani kwa mara ya 5 na kumfikia Messi kwa idadi.
Lakini Messi amesisitiza upinzani kati yake na Ronaldo ni kitu kinachokuzwa na kushabikiwa na Vyombo vya Habari.
Huku akimtaja Ronaldo kama mmoja wa Wachezaji Bora Duniani, Messi ametamka: "Huo upinzani kati yetu umebuniwa na Wanahabari na si sisi!"
Aliongeza: "Sisi tunachotaka ni kufanya vyema kila Mwaka kwa Timu zetu na kinachosemwa nje sikipi umuhimu!"
Kuhusu Ronaldo, Messi amesisitiza: "Yeye. Ni Mchezaji wa Kipaji cha ajabu mno ana uwezo wa aina yaje na Mwaka hadi Mwaka anakuwa Bora zaidi na ndio maana yeye ni mmoja wa wale Bora Duniani!"

CRISTIANO RONALDO - GOLI 600, UBINGWA ULAYA MARA 3 NDANI YA MIAKA 4!

== PATA NINI KABEBA TANGU 2009!
SASA MCHEZAJI BORA DUNIANI Cristiano Ronaldo amepachika Jumla ya Bao 600 kwa Klabu na Nchi yake Portugal na Juzi kutwaa UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, kwa mara ya 3 katika Miaka Minne.
Ronaldo alijiunga na Real Madrid kutoka Manchester United Mwaka 2009 kwa Dau la Dunia wakati huo la Pauni Milioni 80.
CR7-UCLAkiwa na Man United, kati ya 2003 na 2009, aliweza kutwaa Ballon d'Or mara moja huku akibeba Ubingwa wa England mara 3, FA CUP 1, LIGI CUP 2, Ngao ya Jamii 1, UCL 1 na FIFA Kombe la Dunia kwa Klabu 1.
Akiwa na Real kwenye Msimu wa kwanza alitoka kapa.
LAKINI MSIMU ULIOFUATA NI HISTORIA, TIZAMA NINI ALIBEBA:
2011
Buti ya Dhahabu Ulaya (Goli 40)
Copa del Rey
2012
La Liga
2013
Ballon d'Or
2014
UEFA CHAMPIONZ LIGI   (Mara ya 2) 
Copa del Rey
Buti ya Dhahabu Ulaya (Bao 31 akifungana na Luis Suarez)
Ballon d'Or
2015
Buti ya Dhahabu Ulaya (Bao 48)
2016
Euro 2016
UEFA CHAMPIONZ LIGI  (Mara ya 3)
2017
La Liga
UEFA CHAMPIONZ LIGI  (Mara ya 4) 
***Kwenye Tuzo hizi akiwa na Real, Mataji kama vile UEFA SUPER CUP na FIFA Kombe la Dunia kwa Klabu hayamo kwa vile wanayahesa yana 'ulakini!'.
 

RONALDO AMPIKU MESSI UFUNGAJI BORA UEFA CHAMPIONZ LIGI MSIMU HUU!

== APEWA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA FAINALI NA SIR ALEX!
KABLA ya Fainali ya Jana ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, ambayo Mabingwa Real Madrid walitetea vyema Taji lao kwa kuifunga Juventus 4-1, Rekodi ya Cristiano Ronaldo ya Ufungaji Bora kwa Misimu Minne iliyopita ilikuwa hatarini.
CR7-SIRALEXlLionel Messi wa Barcelona ndie aliekuwa Juu akiongoza kwa Bao 1 huku Ronaldo akiwa na Bao 10.
Kabla Robo Fainali ya UCL Msimu huu Ronaldo alikuwa nyuma mno ya Messi akiwa na Bao 9 pungufu.
Lakini Bao 5 katika Mechi 2 za Robo Fainali dhidi ya Bayern Munich zilimbeba na kwenye Nusu Fainali dhidi ya Atletico Madrid Ronaldo alipiga Hetitriki na kumfanya awe na Bao 10 dhidi ya 11 za Messi na yeye kutinga Fainali ya Jana huko Cardiff, Wales dhidi ya Juve akiwa na matumaini makubwa ya kumgalagaza Messi kwa Misimu Mitano ya Ulaya.
Jana, kwenye Fainali, Ronaldo alipiga Vao 2 Real ikiichapa Juve 4-1.
Pia mara baada ya Fainali hiyo, Ronaldo alikabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Fainali hiyo kutoka kwa Sir Alex Ferguson ambae alikuwa na Ronaldo kwa Miaka 6 huko Man United.
×××××××××××××××××××××
UCL - WAFUNGAJI BORA:
12 Cristiano Ronaldo Real Madrid
11 Lionel Messi Barcelona
8 Edinson Cavani Paris
8 Robert Lewandowski Bayern
7 Pierre-Emerick Aubameyang Dortmund
×××××××××××××××××××××
Ronaldo pia ameikamata Rekodi ya Messi ya kupiga Hetitriki 7 kwenye UCL.
UCL - WAFUNGAJI BORA KWA MISIMU MFULULIZO:
5 Cristiano Ronaldo Real Madrid 2012/13, 2013/14, 2014/15, 2015/16, 2016/17
4 Lionel Messi Barcelona 2008/09, 2009/10, 2010/11, 2011/12
3 Gerd Müller Bayern 1972/73, 1973/74, 1974/75
3 Jean Pierre Papin Marseille, Milan 1989/90, 1990/91, 1991/92

CAS YAIPIGA MSUMARI ATLETICO, KIFUNGO CHA FIFA KUSAJILI CHABAKI!

ATLETICO-BARCACAS(Court of Arbitration for Sport), Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, imeitupa Rufaa ya Klabu ya Spain Atletico Madrid iliyopinga kufungiwa na FIFA kusajili Wachezaji Wapya.
Atletico, na wenzao wa Spain Real Madrid, waliadhibiwa na FIFA kutosajili Wachezaji Wapya kwa kukiuka Kanuni za Kusajili Wachezaji Chipukizi.
Hatua hii ya CAS inamaanisha Atletico hairuhusiwi kusajili Mchezaji Mpya hadi Dirisha la Uhamisho la Januari 2018.
FIFA iliwaadhibu Atletico na Real Mwaka Jana kutosajili kwa Madirisha ya Uhamisho Mawili na pia kutwangwa Faini za Pauni 622,000.
CAS iliipunguzia Real Adhabu yao kwa Mwaka Mmoja lakini kwa Atletico hawakupata afueni.
Hivyo Atletico hawawezi kusajili Mchezaji Mpya hadi Januari 2018 lakini wako huru kumuuza yeyote.
Hatua hii inamaanisha Atletico haiwezi hivi sasa kumchukua Alexandre Lacazette kutoka Lyon ya France licha ya kuwepo makubaliano kwa Klabu hizo mbili.

Habari MotoMotoZ