LA LIGA: RONALDO AIPAISHA REAL 4 MBELE YA BARCA. SEVILLA….NA 1 MKONONI!

RONALDO-WAYAVINARA wa La Liga Real Madrid wamepaa kileleni wakiwa Pointi 4 mbele na Mechi 1 mkononi baada ya Jana kuitwanga Real Sociedad 3-0 wakati Wapinzani wao Barca wakidroo na Sevilla kufungwa.

Real sasa wamecheza Mechi 19 na wana Pointi 46 wakati Barca na Sevilla, zilizocheza Mechi 20 kila moja, zina Pointi 42 kila moja.

Bao za Real hapo Jana Uwanjani kwao Santiago Bernabeu zilipigwa na Mateo Kovacic akipokea msaada wa Cristiano Ronaldo katika Dakika ya 38 na kisha Dakika ya 51 Kovacic kumtengenezea Ronaldo aliepiga la Pili, likiwa Bao lake la 13 katika Mechi 13 zilizopita, na la 3 kuingizwa Dakika ya 82 kupitia Alvaro Morata alieunganisha Krosi ya Lucas Vazquez.

Real Sociedad walicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 74 baada ya Inigo Martinez kuzoa Kadi za Njano 2 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

La Liga

Ratiba/Matokeo:

Jumamosi Januari 28

Villarreal 2 Granada 0

Alaves 0 Atletico Madrid 0

Eibar 3 Deportivo la Coruna 1

Leganes 0 Celta Vigo 2

Jumapili Januari 29

Real Betis 1 Barcelona 1

Espanyol 3 Sevilla 1

Athletic Bilbao 2 Sporting Gijon 1

Real Madrid 3 Real Sociedad 0

Jumatatu Januari 30

2245 Las Palmas v Valencia

LA LIGA: SUAREZ AINUSURU BARCA DAKIKA YA MWISHO!

>>USIKU VINARA REAL v REAL SOCIEDAD!

BETIS-BARCALuis Suarez aliinusuru Barcelona Ugenini na Real Betis kwa kusawazisha Dakika ya 90 na kuambua Sare ya 1-1 huku pia wakinyimwa Goli la wazi baada ya Mpira kuvuka Mstari wa Goli.

Betis walitawala na kupiga mwamba kupitia Dani Ceballos na Ruben Castro na hatimae Alex Alegria kufunga katika Dakika ya 75.

Barca walichukizwa pale Refa alipogomea Bao lao kwa Mpira uliovuka Mstari wa Golini na kuokolewa na Beki Aissa Mandi ukiacha Wachambuzi kusikitika kwa nini La Liga bado haijaanza kutumia Teknoloji ya Mstari wa Golini kubaini Goli au si Goli.

Matokeo haya yanawaacha Barca wakiwa nyuma ya Vinara Real Madrid kwa Pointi 1 na pia wakiwa wamecheza Mechi 2 zaidi ya Real.

Usiku huu Real wako kwao Santiago Bernabeu kucheza na Real Sociedad.

VIKOSI:

REAL BETIS (Mfumo 5-3-2): Adan; Piccini, Mandi, Pezzella, Tosca, Durmisi; Pardo, Petros, Ceballos; Castro, Alegria.

Akiba: Martinez, Nahuel, Zozulya, Donk, Navarro, Gonzalez, Gimenez.

BARCELONA (Mfumo 4-3-3): Ter Stegen; Vidal, Mathieu, Pique, Digne; Suarez, Rakitic, Turan; Messi, Suarez, Neymar.

Akiba: Roberto, Alcacer, Umtiti, Andre Gomes, Mascherano, Alba, Cillessen.

REFA: Alejandro José Hernández Hernández

La Liga

Ratiba

Jumamosi Januari 28

Villarreal 2 Granada 0

Alaves 0 Atletico Madrid 0

Eibar 3 Deportivo la Coruna 1

Leganes 0 Celta Vigo 2

Jumapili Januari 29

Real Betis 1 Barcelona 1

1815 Espanyol v Sevilla

2030 Athletic Bilbao v Sporting Gijon

2245 Real Madrid v Real Sociedad

Jumatatu Januari 30

2245 Las Palmas v Valencia

LA LIGA: JUMAPILI REAL KUIVAA REAL SOCIEDAD, KUUFUTA ‘MDORORO’?

LALIGA-2016-17-2-3VINARA wa La Liga huko Spain Real Madrid Jumapili watakuwa Wenyeji wa Timu ngumu Real Sociedad na sasa wapo kwenye kibarua kigumu cha kugeuza fomu yao iliyoporomoka ambayo imewafanya washindwe kushinda katika Mechi zao 3 kati ya 4 zilizopita.

Kati-Wiki, Real walibwagwa nje ya Copa del Rey walipotoka 2-2 na Celta Vigo baada ya kufungwa Mechi ya Kwanza 2-1.

Hata hivyo, kwenye La Liga, Real, chini ya Kocha Zinedine Zidane, wapo Pointi 1 mbele ya Sevilla na 2 mbele ya Barcelona huku wao wakiwa wamecheza Mechi 1 pungufu.

Kuporomoka kwa fomu ya Real kumeandamwa na kuwa na Majeruhi 7 kwenye Kikosi chao cha Kwanza ambao ni Raphael Varane, Gareth Bale, James Rodriguez, Luka Modric, Marcelo, Dani Carvajal na Pepe ingawa Varane huenda akacheza Mechi na Sociedad.

Nao Real Sociedad watatinga kwenye Mechi hii na Real huko Santiago Bernabeu wakitoka kwenye kichapo cha 5-2 toka kwa Barcelona kwenye Mechi ya Copa del Rey.

Jumapili Barcelona watacheza Mechi yao mapema Ugenini na Real Betis na ushindi kwao utawafanya waongoze La Liga kwa muda kwa vile Real na Sevilla watacheza Mechi zao baadae.

La Liga

Ratiba

Jumamosi Januari 28

1500 Villarreal v Granada

1815 Alaves v Atletico Madrid

2030 Eibar v Deportivo la Coruna

2245 Leganes v Celta Vigo

Jumapili Januari 29

1400 Real Betis v Barcelona

1815 Espanyol v Sevilla

2030 Athletic Bilbao v Sporting Gijon

2245 Real Madrid v Real Sociedad

Jumatatu Januari 30

2245 Las Palmas v Valencia

COPA DEL REY: BARCA YATINGA NUSU FAINALI KWA KISHINDO!

>LEO DROO YA NUSU FAINALI, BARCA KUMVAA YUPI, ATLETI, CELTA AU ALAVES?

COPADELREY-BARCAMABINGWA Watetezi wa Kombe la Mfalme wa huko Spain, Copa del Rey, FC Barcelona, Jana waliitandika Real Sociedad Bao 5-2 kwenye Mechi ya Pili ya Robo Fainali.

Kwenye Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Anoeta Stadium, Barca ilishinda 1-0 na hivyo sasa wametinga Nusu Fainali kwa Jumla ya Mabao 6-2.

Hapo Jana, Bao za Barca zilifungwa na Denis Suarez, Bao 2, Lionel Messi, Penati, Luis Suarez na Arda Turan.

Bao za Real Sociedad zilipachikwa na Juanmi na Da Silva.

Kwenye Nusu Fainali, Barcelona, ambao wametwaa Copa Del Rey mara 28, wataungana na Atletico Madrid, Celta Vigo na Alaves.

Droo ya Nusu Fainali itafanyika baadae Leo

COPA DEL REY

Robo Fainali – Mechi za Kwanza

Matokeo:

Jumatano Januari 18

Alcorcon 0 Deportivo Alaves 2

Real Madrid 1 Celta de Vigo 2

Alhamisi Januari 19

Atletico Madrid 3 SD Eibar 0

Real Sociedad 0 Barcelona 1

Robo Fainali – Mechi za Pili

**Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi Mbili

Jumanne Januari 24

Deportivo Alaves 0 Alcorcon 0 [2-0]      

Jumatano Januari 25

SD Eibar 2 Atletico de Madrid 2 [2-5]    

Celta de Vigo 2 Real Madrid CF 2 [4-3]  

Alhamisi Januari 26

FC Barcelona 5 Real Sociedad 2 [6-2]

LA LIGA: SEVILLA, BARCA ZASHINDA ZAIKIMBILIA REAL KILELENI!

LALIGA-2016-17-2-3JANA Timu ambazo zinawakimbiza Vinara Real Madrid, Sevilla na Barcelona, zote zimeshinda na kuleta presha kwa Real ambao wamecheza Mechi 1 pungufu.
Wakati Real wamecheza Mechi 18 nacwana Pointi 43, Sevilla wanafuatia wakiwa na Pointi 42 kwa Mechi 19 na Barca wamecheza Mechi 19 na wana Pointi 41.
Timu ya 4 ni Atletico Madrid wenye Pointi 35 kwa Mechi 19.
Hapo Jana, Barca wakicheza Ugenini waliitandika SD Eibar 4-0 kwa Bao za Denis Suárez (Dakika ya 31'), Messi (50'), Luis Suárez (68' ), na Neymar (90'+1).
Katika Mechi hiyo Barca walipata pigo mapema baada ya Kiungo wao wa kutegemewa Sergio Busquets kuumia na Denis Suarez kuingizwa na kuwapatia Bao la kwanza kwa Mkwaju wa Mita 20.
Nayo Timu ya Pili Sevilla ilipigana na hatimae kuishinda Ugenini 4-3 Osasuna.
Osasuna walifunga Bao zao Dakika za 15, 63 na 90.kupitia Sergio Leon, Fuente, aliejifunga mwenywe, na Kenan Kodro.
Bao za Sevilla zilipachikwa na Fuente Dakika za 43 na 65, na nyingine ni Dakika za 80 na 90 kupitia Franco Vazquez na Pablo Sirabia.
Atletico Madrid walitoka 2-2 Ugenini na Athletic Bilbao waliofunga Bao zao kupitia Inigo Lekne na Oscar De Macos Dakika za 42 na 56 wakati za Atletico zikipigwa na Koke na Antoine Griezmann kwenye Dakika za 3 na 80.
LA LIGA
Ratiba/Matokeo
**Saa za Bongo
Jumamosi Januari 21
Real Madrid 2 Malaga 1
Villareal 0 Valencia 2
Espanyol 3 Granada 1
Deportivo Alaves 2 CD Leganes 2
Jumapili Januari 22
Osasuna 3 Sevilla 4
Athletic Bilbao 2 Atletico Madrid 2
Real Betis 0 Sporting Gijon 0
Real Sociedad 2 Celta Vigo 0
SD Eibar 0 Barcelona 4