LA LIGA: KIPORO CHA REAL CHAPANGWA!

COPA DEL REY: LEO BARCA AU ATLETI NANI FAINALI?

LALIGA-2016-17-2-3-1WAKATI Mechi ya kiporo cha La Liga cha Real Madrid kikipangwa Tarehe mpya, Leo ni Marudiano ya Nusu Fainali ya Copa del Rey huko Nou Camp kati ya Barcelona na Atletico Madrid.

LA LIGA: KIPORO CHA REAL CHAPANGWA!

Mechi ya La Liga kati ya Vinara wake Real Madrid na Valencia sasa itachezwa Februari 22 Nyumbani kwa Valencia.

Awali Mechi hii ilikuwa ichezwe Desemba lakini ikifutwa kutokana na ushiriki wa Real huko Japan kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani.

Upangwaji upya wa Mechi hii unazidi kuwashushia Real mzigo mkubwa kwani sasa sasa watakuwa na Mechi 8 ndani ya Siku 25 zikiwemo Mechi 2 za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Napoli ya Italy.

Juzi Jumapili, Mechi nyingine ya Real ya La Liga Ugenini na Celta Vigo ilifutwa kutokana na Dhoruba iliyoharibu Paa la Uwanja wa Balaidos na hadi sasa Mechi hiyo haijapangiwa Tarehe mpya.

COPA DEL REY: LEO BARCA AU ATLETI NANI FAINALI?

Mabingwa Watetezi Barcelona wanachungulia Fainali ya 4 mfululizo ya Kombe la Mfalme wa Spain, Copa del Rey, wakati Leo wakicheza Mechi ya Pili ya Nusu Fainali na Atletico Madrid huko Nou Camp huku wao wakiwa mbele baada kushinda Mechi ya Kwanza 2-1.

Kwenye Mechi hii, Barca watamkosa Staa wao wa Brazil Neymar ambae yupo Kifungoni Mechi 1 na pia Nyota wao Lionel Messi anapaswa kujichunga hii Leo kwani akilambwa Kadi ya Njano tu hatacheza Fainali.

Copa del Rey

Nusu Fainali

Ratiba – Mechi za Pili

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

Jumanne Februari 7

Barcelona v Atletico Madrid [2-1]

Jumatano Februari 8

Alaves v Celta Vigo [0-0]

LA LIGA: BARCA WAISOGELEA KILELENI REAL AMBAO MECHI YAO YA LEO IMEFUTWA!

LALIGA-2016-17JANA huko Nou Camp, Barcelona waliitandika Athletic Bilbao 3-0 na kuwasogelea Vinara Real Madrid na kuwa Pointi 1 nyuma yao kwenye La Liga.

Leo Real Madrid walitakiwa kucheza Ugenini na Celta Vigo lakini Mechi hiyo imefutwa baada ya Uwanja wa Balaidos kupigwa na Dhoruba na kuharibu Paa ambalo linasemekana si salama kwa Washabiki.

Kufutwa kumeifanya Real iwe imecheza Mechi 2 pungufu ya Barca lakini bado wanaongoza La Liga.

Hapo Jana Bao za Barca zilifungwa na Paco Alcacer, Dakika ya 18, Lionel Messi, Dakika ya 40, na Aleix Vidal, Dakika ya 67.

LA LIGA

Ratiba/Matokeo:

Jumamosi Februari 4

Atletico de Madrid 2 CD Leganes 0

Valencia C.F 0 SD Eibar 4

Malaga 0 RCD Espanyol 1

Barcelona 3 Athletic Bilbao 0

Jumapili Februari 5

1400 Sevilla FC v Villarreal CF

1815 Sporting Gijon v Deportivo Alaves

2030 Real Sociedad v Osasuna

2245 Celta de Vigo v Real Madrid CF [IMEAHIRISHWA]

Jumatatu Februari 6

2245 Granada CF v Las Palmas

LA LIGA: REAL WAWAFATA TENA WABABE WAO CELTA VIGO, KULIPA KISASI?

LALIGA-2016-17-2-3-1VINARA wa La Liga Real Madrid Wikiendi hii watacheza Ugenini na Celta Vigo ambayo Wiki mbili zilizopita iliitupa nje Real kwenye Robo Fainali ya Copa del Rey.
Kwenye Mechi 2 za Robo Fainali hiyo, Real ilichapwa 2-1 kwao Santiago Bernabeu na kisha kutoka 2-2 Nyumbani kwa Celta Vigo.
Mechi hii ni muhimu kwa Real kuzikimbia Barcelona na Sevilla ambazo zinaikimbiza kileleni mwa La Liga.
Real, waliocheza Mechi 19, wapo Pointi 4 mbele ya Barca na Sevilla zilizofungana kwa Pointi na zote zikiwa zimecheza Mechi 20.
Wikiendi hii Barca wapo kwao Nou Camp kucheza na Athletic Bilbao wakati Sevilla pia wapo Nyumbani kucheza na Villareal.
Kwenye Mechi yao hii, Real wanategemewa kuimarika kwa Majeruhi wao kadhaa kurejea na hao ni Pepe, James Rodriguez na Luka Modric.
Uimara huo unahitajika kwani Celta Vigo wameshaonyesha ugumu wao kwa Real licha ya kuwa Nafasi ya 8 kwenye La Liga kwani kwa Misimu Miwili iliyopita wamepoteza Mechi 3 tu wakiwa kwao.
LA LIGA
Ratiba
Ijumaa Februari 3
2245 Deportivo La Coruna v Real Betis
Jumamosi Februari 4
1500 Malaga CF v RCD Espanyol
1815 FC Barcelona v Athletic de Bilbao
2030 Atletico de Madrid v CD Leganes
2245 Valencia C.F v SD Eibar
Jumapili Februari 5
1400 Sevilla FC v Villarreal CF
1815 Sporting Gijon v Deportivo Alaves
2030 Real Sociedad v Osasuna
2245 Celta de Vigo  v Real
Madrid CF
Jumatatu Februari 6
2245 Granada CF v Las Palmas

COPA DEL REY – NUSU FAINALI: SUAREZ, MESSI WAIZAMISHA ATLETICO KWAO VICENTE CALDERON!

COPA-MESSI-SUAREZBARCELONA, Mabingwa Watetezi wa Kombe la Mfalme wa Spain, Copa del Rey, Jana wameichapa Atletico Madrid Bao 2-1 huko Estadio Vicente Calderon Jijini Madrid katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali.

Timu hizi zitarudiana Wiki ijayo huko Nou Camp na Mshindi kucheza na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine kati ya Deportivo Alaves na Celta Vigo ambao Leo wanacheza Mechi yao ya Kwanza.

Kwenye Mechi ya Jana, Luis Suarez ndie aliifungia Barca Bao la Kwanza katika Dakika ya 7 alipokokota Mpira toka Mstari wa Kati na kufunga kilaini.

Dakika ya 33 mzinga wa Lionel Messi kutoka nje ya Boksi uligonga Posti na kutinga na kuwapa Barca Bao la Pili.

Dakika ya 59, Antoine Griezmann akaipa matumaini Atletico baada ya kufunga Bao pekee kwao.

LA LIGA

Copa del Rey – Nusu Fainali

**Saa za Bongo

Jumatano Februari 1

Atletico Madrid 1 Barcelona 1

Alhamisi Februari 2

2300 Celta Vigo v Deportivo Alaves

Mechi za Pili

[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]

Jumanne Februari 7

2300 Barcelona v Atletico Madrid [2-1]

Jumatano Februari 8

2300 Deportivo Alaves v Celta Vigo

COPA DEL REY: LEO NUSU FAINALI ATLETICO NA BARCA HUKO VICENTE CALDERON!

IMG-20170201-WA0002LEO UWANJA wa Vicente Caldero  Jijini Madrid Nchini Spain ndio dimba la Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme wa Spain, Copa del Rey, kati ya Atlético Madrid na Barcelona.
Mechi ya Pili kati yao itachezwa huko Nou Camp Wiki ijayo.
Hali za Timu
Kwenye Mechi hii Barca hawatamtumia Kipa Marc-André ter Stegen ambae hucheza La Liga tu na badala yake langoni atakuwepo Jasper Cillessen.
Pia watawakosa Majeruhi Andrés Iniesta, Sergio Busquets na Lucas Digne.
Kwa upande wa Wenyeji Atlético Madrid walio chini ya Kocha Diego Simeone wao watamkosa José Giménez kwenye Difensi lakini nafasi yake itachukuliwa na Stefan Savic ambae atadabo na Diego Godín.
Wengine wanaotarajiwa kuanza pambano hili ni Kiungo Juanfran na pia wapo Ferreira Carrasco na Antoine Griezmann.
Nusu Fainali nyingine ya Copa del Rey itachezwa Kesho huko Estadio Municipal de Balaidos kati ya Celta Vigo na Deportivo Alaves.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Barcelona (Mfumo 4-3-3): Cillessen; Roberto, Piqué, Umtiti, Alba; Mascherano, Rakitic, Gomes; Messi, Suárez, Neymar
Atlético Madrid (Mfumo 4-1-4-1): Moyá; Vrsaljko, Savic, Godín, Luís; Gabi; Juanfran, Saúl, Koke, Carrasco; Griezmann