RAMOS AIPAISHA REAL, RONALDO AZOMEWA!

==LEO EIBAR NA BARCA!
LALIGA-2016-17-2-3JANA Nahodha wa Real Madrid Vinara wa La Liga Sergio Ramos alifunga Bao 2 wakati Timu yake ikiichapa 2-1 Malaga huko Santiago Bernabeu kwenye Mechi ya Ligi ambayo Nyota wa Real Cristiano Ronaldo akizomewa na baadhi ya Mashabiki wa Timu hiyo.
Baada Mechi 18 kwa kila Timu Real wanaongoza La Liga wakiwa na Pointi 43 wakifuata Sevilla wenye 39, Barcelona 38 na kisha Atletico Madrid wenye 34.
Jana Ramos alifunga Bao la Kwanza Dakika ya 35 kwa Kichwa kufuatia Kona ya Toni Kroos na kisha kupiga la pili Dakika ya 43 huku Malaga wakifunga Bao lao moja Dakika ya 63 kupitia Juanpi Anor.
Kwenye Mechi hiyo Ronaldo alikosa nafasi kadhaa zilizookolewa na Kipa Kameni na moja kupiga Posti kitu ambacho kiliwachukiza Mashabiki ambao baadhi yao walimzomea.
Kitu hicho kilimsikitisha Meneja wa Real Zinedine Zidane ambae aliwaasa Mashabiki hao kuwapa moyo Wachezaji.
Leo Timu za Pili na za 3, Sevilla na Barca, zipo Ugenini kucheza Mechi zao za La Liga.
LA LIGA
Ratiba/Matokeo
**Saa za Bongo
Jumamosi Januari 21
Real Madrid 2 Malaga 1
Villareal 0 Valencia 2
Espanyol 3 Granada 1
Deportivo Alaves 2 CD Leganes 2
Jumapili Januari 22
1400 Osasuna v Sevilla
1815 Athletic Bilbao v Atletico Madrid
2030 Real Betis v Sporting Gijon
2245 SD Eibar v Barcelona

TUTA LA NEYMAR LAMALIZA UKAME WA MIAKA 10 BARCA KUTOIFUNGA REAL SOCIEDAD, ANOETA STADIUM!!

BARCA-NEYMAR-TUTAUKAME wa kutoshinda Miaka 9 dhidi ya Real Sociedada wakiwa Uwanjani kwao Anoeta Stadium ulimalizika Jana Usiku wakati Penati ya Staa wa Brazil Neymar kuipa Barcelona ushindi wa 1-0 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya Copa del Rey, Kombe la Mfalme huko Spain.

Penati hiyo ilipigwa Dakika ya 21 baada ya Neymar mwenyewe kuangushwa ndani ya Boksi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Barca kushinda hapo Anoeta Stadium tangu 2007 na tangu wakati huo Mechi 11 zishapigwa kati yao hapo hapo Anoeta huku Barca wakifungwa 5 na Sare 3 katika Mechi 8 zilizopita.

Mara ya mwisho kwa Barca kushinda, Mwaka 2007, Bao za Andrés Iniesta na Samuel Eto’o ndizo ziliwaibua kidedea.

Msimu huu, kwenye La Liga, Real Sociedad na Barca zilitoka 1-1 huko Anoeta Stadium.

Barca sasa wapo kwenye hatua nzuri ya kutinga Nusu Fainali ya Copa del Rey ambalo wao ndio Mabingwa Watetezi kwani watarudiana na Real Sociedad huko Nou Camp Alhamisi ijayo.

Barca wametinga Nusu Fainali za Copa del Rey kwa Misimu 6 mfululizo hadi sasa wakitwaa Kombe mara 3 na mara 2 kufungwa Fainali.

Fainali ya Copa del Rey ni Mei 27.

COPA DEL REY

Robo Fainali – Mechi za Kwanza

Matokeo:

Jumatano Januari 18

Alcorcon 0 Deportivo Alaves

Real Madrid 1 Celta de Vigo 2

Alhamisi Januari 19

Atletico Madrid 3 SD Eibar 0

Real Sociedad 0 Barcelona 1

Robo Fainali – Mechi za Pili

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumanne Januari 24

21:15 Deportivo Alaves v Alcorcon        

Jumatano Januari 25

21:15 SD Eibar v Atletico de Madrid      

23:15 Celta de Vigo v Real Madrid CF   

Alhamisi Januari 26

23:15 FC Barcelona v Real Sociedad

BAADA KUVUNJWA REKODI YAO MECHI 40 BILA KUFUNGWA, REAL WAPIGWA MARA YA PILI MFULULIZO!

REAL-ZIZOUREAL MADRID Janacwakiwa kwao Santiago Bernabeu wamepokea kipigo chao cha pili mfululizo baada kufungwa 2-1 na Celta Vigo katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali za Copa del Rey, Kombe la Mfalme wa Spain.
Real walikuwa kwenye mbio za Mechi 40 za kutofungwa lakini Wikiendi iliyopita zikamalizwa walipochapwa 2-1 na Sevilla kwenye La Liga.
Kifungo cha Jana ni mara kwanza kwa Real kuchapwa Mechi 2 mfululizo tangu Novemba 2015.
Jana Celta Vigo walifunga Bao lao la Kwanza Dakika ya 64 kupitia Iago Aspas aliewahi kuichezea Liverpool na Marcelo kusawazisha kwa bunduki kali Dakika ya 69.
Dakika 1 baadae Celta Vigo wakafunga Bao la ushindi kupitia Castro Otto.
Timu hizi zitarudiana huko Galicia Jumatano ijayo na Mshindi kutinga Nusu Fainali.
 
 

MBIO ZA MECHI 40 KUTOFUNGWA ZAISHA, REAL WACHAPWA DAKIKA ZA MAJERUHI!

LALIGA-2016-17-2VINARA wa La Liga Real Madrid Jana walichapwa 2-1 Ugenini na kuvunjwa mbio zao za kutofungwa kwa Mechi 40 baada ya Bao la Dakika za Majeruhi la Stevan Jovetic kuwapa Sevilla ushindi wa 2-1.

Real ndio waliotangulia kufunga Dakika ya 67 kwa Penati ya Cristiano Ronaldo iliyotolewa baada ya Dani Carvajal kuangushwa na Kipa wa Sevilla Sergio Rico.LALIGA-JAN16

Dakika ya 85, Sevilla walisawazisha kwa Bao la kujifunga mwenyewe Sergio Ramos na Dakika ya 91 Jovetic kuwapa ushindi Sevilla.

Matokeo haya bado yamewabakisha Real, ambao walikuwa hawajafungwa tangu Aprili 6, kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 1 mbele ya Sevilla huku Barcelona wakifuatia wakiwa Pointi 2 nyuma yao lakini Real wamecheza Mechi 1 pungufu kupita Wapinzani wao wote.

LA LIGA

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Jumamosi Januari 14

CD Leganes 0 Athletic de Bilbao 0

FC Barcelona 5 Las Palmas 0

Atletico de Madrid 1 Real Betis 0

Deportivo La Coruna 0 Villarreal CF 0

Jumapili Januari 15

Valencia C.F 2 RCD Espanyol 1

Celta de Vigo 1 Deportivo Alaves 0

Sporting Gijon 2 SD Eibar 3

Granada CF 1 Osasuna 1

Sevilla FC 2 Real Madrid CF 1

Jumatatu Januari 16

2245 Malaga CF v Real Sociedad

LA LIGA: BARCA YAINYEMELEA REAL KILELENI!

LALIGA-2016-17-2MABINGWA wa La Liga huko Spain, FC Barcelona, Jana waliifyeka Las Palmas 5-0 na kukamata Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 tu nyuma ya Vinara Real Madrid.
Lakini Real wana Mechi 2 mkononi na Leo wana nafasi ya kuliongeza pengo la Pointi kuwa 5 wakicheza Ugenini na Sevilla ambayo Juzi ilishindwa kuibwaga Real dhaifu iliyocheza bila Wachezaji kadhaa maarufu akiwemo Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo walipoumwaga uongozi wa 3-1 na Real kurudisha na kuwa 3-3 katika Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey.
Real, wakiwa pia na Timu dhaifu, waliinyuka Sevilla 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey.
Bao za Barca hiyo Jana zilifungwa na Luis Suarez, Bao 2, Lionel Messi, Arda Turan na Aleix Vidal.
Mapema Jana, Bao la Dakika ya 8 la Nicolas Gaitan liliipa Atletico Madrid ushindi wa 1-0 walipocheza na Real Betis.
LA LIGA
Msimamo
Timu za Juu:
1 Real Madrid Mechi 16 Pointi 40
2 Barcelona Mechi 18 Pointi 38
3 Sevilla Mechi 17 Pointi 36
4 Atletico Madrid Mechi 18 Pointi 34
5 Villareal Mechi 18 Pointi 31
6 Real Sociedad Mechi 17 Pointi 29
LA LIGA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Jumamosi Januari 14
CD Leganes 0 Athletic de Bilbao 0
FC Barcelona 5 Las Palmas 0
Atletico de Madrid 1 Real Betis 0
Deportivo La Coruna 0 Villarreal CF 0
Jumapili Januari 15
1400 Valencia C.F v RCD Espanyol
1815 Celta de Vigo v Deportivo Alaves
2030 Sporting Gijon v SD Eibar
2030 Granada CF v Osasuna
2245 Sevilla FC v Real Madrid CF
Jumatatu Januari 16
2245 Malaga CF v Real Sociedad